GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 309
JK si tu JEMBE, bali ni JEMBE NA SULULU au SHOKA kama ukipenda. Kwa maana nyingine ile alama iliyoko kwenye bendera ya CCM ndio JK. Ukitaka kumjua zaidi JK muulize MO Ibrahim, kwani yeye ndio kamaliza.
Ndugu MJENGA, mada kama hizi CHADEMA hawawezi kujibu kwa hoja, angalia ukurasa wa 3 hakuna aliyejibu hoja. Tafsiri fupi ya hali hii ni kuwa hila na vitimbi vyao vimeshindwa, kwani wao wangependa kuiona nchi haitawaliki na Tanzania inaingia katika VITA. Dua zao zote zimeshindikana, na kibaya zaidi watanzania wamekielewa CHADEMA kama chama chenye nia mbaya na WATANZANIA. Na hii imejionyesha wazi katika matokeo ya UDIWANI kama ulivyoainisha katika mada yako.
Tatizo la CHADEMA ni kushindwa kukubali hata katika yale mazuri ambayo yanaonekana wazi kwa wananchi yaliyofanywa na serikali. Kitendo hiki ndicho kitachoiua CHADEMA, kwa sababu watanzania ni watu wenye akili sana na kuelewa ni nini kinawezekana na nini ni Propaganda.
Katika mafanikio yote umeyasema, lakini kubwa lililowafunga mdomo wapinzani ni la kufanikisha UCHAGUZI MKUU WA CHAMA KATIKA NGAZI KUU MBALI MBALI MJINI DODOMA hivi karibuni. Wengi walifikiri ngumi zitapigwa na chama kitachanika vipande vidogo vidogo kama chembe za mtama. Hilo halikutokea, na ni kwa juhudi na umakini mkubwa wa Mwenyekiti, JK. Safu ilivyojipanga inaitisha CHADEMA na iaashiria mwisho wa mbio zao kuelekea IKULU. Kama kuna CHAMA kinachofahamu umahiri wa JK, basi ni CHADEMA.
Naweza kubet kuwa JK atapata zawadi ya MO Ibrahim mwaka 2016/2017, kwa ufanisi wake mzuri wa kujenga Demokrasia Tanzania ikiwa pamoja na uhuru wa kusema, kuunda urafiki na vyama vyote nchini, kukuza elimu na kuijenga Tanzania yenye matumaini.
Ukitaka kujua mafanikio ya Tanzania katika demokrasia, tathmini hali ya demokrasia katka nchi jirani kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ethiopia na Kongo. Ukipata jibu rudi mtandaoni.
JK ni historia kwa Tanzania.
Vilevile mpaka sasa kunamiradi mbali mbali nchini inayoendele chini ya uongozi uliotukuka wa JK. Pia kumbuka tanzania imewekwa kuwa mwenyekiti wa SADC katika mambo ya siasa na ulizi. Vilevile kipindi cha JK hata JKT imerudishwa kwa nguvu ili kuwajengea vijana uzalendo.Na katika ishara nyingine kuwa yeye ni jembe ni uhuru mkubwa na usio na mipaka wa kutoa maoni. Sasa hivi kila mtu anaongea kwa uwazi na uhuru tofauti na serikali zote zilizopita. Ingekuwa wakati wa Mwalimu kwa uhuru huu wakuongea hivi sasa, watu wangekuwa wameisha wekwa kizuizini
Kwa mtazamo wako Jemga, JK ni jembe, lakini kwa uelewa wangu naona kama unakejeli. Ironic presentation'.
Unataka watu waangalie kwa upana migogoro iliyotokea wakati wa utawala wa JK. Kapata uraisi kwa mizengwe kisha kaa kimya akisikilizia upepo. Huo kwa mtazamo wako ni ujanja. Madaktari wamegoma, wananchi wengi wakafa, yeye kaenda zake ng'ambo akiacha nyuma sakata la madaktari. Baada sakata kutulia akatoa hotuba kama vile mfiwa anayelia baada ya kuanua matanga kwako wewe, mheshimwa Mjenga huo ndiyo ujembe. Badala ya kujibu hoja za wanachi anawateka, anawapiga, anawaumiza anawatupa Mabwepande, kwako wewe mheshimiwa Mjenga, vitendo hivi nivya kutukuka.Katika nchi za kistaarabu hata tawala za kistaarabu vitendo kama hivi ni ndra kuvisikia, kwako wewe mheshimiwa Mjenga nchi hizo na tawalahizo hazina viongozi jembe isipokuwa kinyume chake.
Mjenga, sidhani kama unamaanisha unachosema ila kinyume chake. Kama kweli una maana ya unachosema, basi sio mtanzania aliyezoea ustaarabu na kulelewa katika mazingira ya AMANI. Umetokea nchi ya wahuni fulani wanaoendesha mabo yao pasi na kufikiri, kujali maisha na haki za wengine. Nchi ambayo wasio na madaraka hawana nafasi ya kusema hiki hapana kile sawa. Una fikira zakitumwa ambaye kila anachosema bwana mkubwa kwako ni hewala, hakuna kupinga chochote, hata akisema ni baba yako, mume wa mama yako, hata kama unamjua babayako mzazi, maskini utasema sawa. SIAMINI, lazima utakuwa unatania
kweli ni historia rais aliyeingia madarakani kwa rushwa(epa)
akafadhili rushwa(richmond,dowans)
akawatetea wala rushwa(kagoda na kumrudisha Menji Mang'ula wajipange kwa wizi chaguzi zijazo)
Akiwa mwenyekiti akaachia rushwa itawale kwenye chaguzi zake(mwenye vyombo vya kulalamika bila kuchukua hatua)
kavifungia vyombo vinavyoanika uozo wake(mwanahalisi)
kuua na kujaribu kuua watetezi wa haki za binadamu wa makundi jamii(Mwangosi,Ulimboka)
kwa hayo machache kwa nini jk asiwe history hapa tz?
Asungwilmwaifungaaaaaaaa,
ninamaanisha ninachokisema. Nashukuru hata Mbowe aliwahi kusema hayahaya
tena mbele ya J.K hamkumtukana. Kwakuwa nimeyasema mie basi
mwanishushia mitusi ya kila aina. Matusi yanawaponzeni daily.
rais jembe ni yule
ambaye anayatekeleza yale ambayo ameya ahidi kwa wananchiwake but jk
akili yake yote imehamia chini na kusababisha chama ikawa nyufa
zisizozibika hata angefanyeje,
Anaongoza nchi kwa udini, uswaiba, ubinafsi, ufisadi uliokithiri bila
kujali maslahi ya wananchi waliompatia ridhaa ya kuwa kiongozi wa nchi
wew mleta mada akili yako imehamia chini kama ya jk
JK si tu JEMBE, bali ni JEMBE NA SULULU au SHOKA kama ukipenda. Kwa maana nyingine ile alama iliyoko kwenye bendera ya CCM ndio JK. Ukitaka kumjua zaidi JK muulize MO Ibrahim, kwani yeye ndio kamaliza.
Ndugu MJENGA, mada kama hizi CHADEMA hawawezi kujibu kwa hoja, angalia ukurasa wa 3 hakuna aliyejibu hoja. Tafsiri fupi ya hali hii ni kuwa hila na vitimbi vyao vimeshindwa, kwani wao wangependa kuiona nchi haitawaliki na Tanzania inaingia katika VITA. Dua zao zote zimeshindikana, na kibaya zaidi watanzania wamekielewa CHADEMA kama chama chenye nia mbaya na WATANZANIA. Na hii imejionyesha wazi katika matokeo ya UDIWANI kama ulivyoainisha katika mada yako.
Tatizo la CHADEMA ni kushindwa kukubali hata katika yale mazuri ambayo yanaonekana wazi kwa wananchi yaliyofanywa na serikali. Kitendo hiki ndicho kitachoiua CHADEMA, kwa sababu watanzania ni watu wenye akili sana na kuelewa ni nini kinawezekana na nini ni Propaganda.
Katika mafanikio yote umeyasema, lakini kubwa lililowafunga mdomo wapinzani ni la kufanikisha UCHAGUZI MKUU WA CHAMA KATIKA NGAZI KUU MBALI MBALI MJINI DODOMA hivi karibuni. Wengi walifikiri ngumi zitapigwa na chama kitachanika vipande vidogo vidogo kama chembe za mtama. Hilo halikutokea, na ni kwa juhudi na umakini mkubwa wa Mwenyekiti, JK. Safu ilivyojipanga inaitisha CHADEMA na iaashiria mwisho wa mbio zao kuelekea IKULU. Kama kuna CHAMA kinachofahamu umahiri wa JK, basi ni CHADEMA.
Naweza kubet kuwa JK atapata zawadi ya MO Ibrahim mwaka 2016/2017, kwa ufanisi wake mzuri wa kujenga Demokrasia Tanzania ikiwa pamoja na uhuru wa kusema, kuunda urafiki na vyama vyote nchini, kukuza elimu na kuijenga Tanzania yenye matumaini.
Ukitaka kujua mafanikio ya Tanzania katika demokrasia, tathmini hali ya demokrasia katka nchi jirani kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Ethiopia na Kongo. Ukipata jibu rudi mtandaoni.
JK ni historia kwa Tanzania.
wanachedema bana wanamambo ya kikatuni sana.
Mtu akishawazidi hoja wakiona hawana cha kujibu wanaanza kuhesabu idadi ya posts zake na amejiunga lini.
What has the number of posts got to do with the content ?
Jipangeni mjibu hoja hatutaki vioja
Vilevile mpaka sasa kunamiradi mbali mbali nchini inayoendele chini ya uongozi uliotukuka wa JK. Pia kumbuka tanzania imewekwa kuwa mwenyekiti wa SADC katika mambo ya siasa na ulizi. Vilevile kipindi cha JK hata JKT imerudishwa kwa nguvu ili kuwajengea vijana uzalendo.
Nchi nyingi sana Africa hata asia na ulaya zinatamani sana uongozi wa kikwete.
JK ndiye aliyeruhusu mabadiliko ya katiba.
Hivi hamuyaoni hayo yote?