Rais Kikwete hamjui tena Salmin Awadh

Rais Kikwete hamjui tena Salmin Awadh

albuluushiy

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2013
Posts
1,404
Reaction score
687
salmin-awadhi.jpg

Hata Kikwete ‘hamjui' tena Marehemu Salmin Awadh

Wiki hii, Rais Jakaya Kikwete amezungumza na wananchi kupitia kutoa hotuba yake ya kila mwezi kwa njia ya televisheni – dasturi aliyoirithi kutoka kwa mtangulizi wake, Benjamin Mkapa, ya kila mwisho wa mwezi (anaopata wasaa) kuzungumzia masuala, matukio, na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika nchi yetu kwa mwezi uliokwisha.

Lakini kwa mara nyengine tena, akiwa ni kiongozi mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyongeka kwa nchi mbili – Tanganyika na Zanzibar, Rais Kikwete alizungumzia mambo mbali mbali yanayoihusu Tanzania ya upande mmoja wa Tanganyika, akipuuzia kabisa kuzungumzia matatizo, matukio na changamoto mbalimbali zilizotokea katika visiwa vya Zanzibar.


Labda ni kwa kuwa kuwa Zanzibar hakukuwa na uporaji wa silaha kwa mwezi wa Febuari, hakukuwa na mauwaji wala ukataji viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi na mengine kama hayo, ndio maana Rais Kikwete hakuona umuhimu wa kuiangazia sehemu hii muhimu ya Jamhuri ya Muungano anaioitawala.

Lakini kuna mambo mengine kadhaa ya Tanganyika ambayo Rais Kikwete aliyazungumzia ambayo pia yalitokezea Zanzibar. Hilo linatufanya sisi Wazanzibari tujiulize ikiwa kweli tuna nafasi kwake, na ikiwa kweli anajihisi yeye mwenyewe, ndani ya nafsi yake, ikiwa rais wetu ni mmoja?

Nisieleweka kuwa nina wivu. Lakini kitendo cha Rais Kikwete kumtaja kwa namna ya kipekee na kumtukuza aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi na mpigadebe wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Marehemu Kapteni John Komba, kwenye hotuba yake kama kwamba ni mtu pekee muhimu aliyefariki dunia ndani ya Tanzania nzima tangu atowe hotuba yake ya mwisho kwa taifa, huku akipuuzilia mbali kifo cha Mnadhimu Mkuu wa CCM na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Salmin Awadh Salmin, ni cha kushangaza sana.

Katika hotuba yake, Rais Kikwete alisema:

"Wakati tulipokuwa tunajiandaa kurekodi hotuba hii tukapata habari ya huzuni na majonzi makubwa ya kifo cha Mbunge wa Mbinga Magharibi, Mheshimiwa Capt. John Damian Komba. Kifo chake kimeliondolea taifa letu mmoja wa viongozi wake wazuri, msanii mahiri, raia mwema na mzalendo wa kweli. Marehemu alitumia muda mwingi wa maisha yake kuelimisha jamii kuhusu mambo mema, amefanya hivyo akiwa mwalimu na baadaye Kiongozi wa Kikundi cha Sanaa cha JWTZ na hapa mwishoni kiongozi wa kikundi cha Tanzania One Theatre cha Chama Cha Mapinduzi.

Kwa kutumia kipaji alichojaaliwa na Mola wake ametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi yetu na ustawi wa Chama Tawala. Daima tutamkumbuka kwa mambo mengi mema aliyoifanyia jamii ya nchi yetu na taifa kwa jumla.

"Katika salamu zangu za rambirambi kwa Spika wa Bunge na Katibu Mkuu wa CCM niliwaomba kupitia kwao salamu ziwafikie Wabunge wote na viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi. Hali kadhalika, niliomba kupitia kwao salamu ziwafikie familia ya marehemu Capt. John Komba. Kwa familia ya ndugu yetu mpendwa, napenda kuwahakikishia kuwa tuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na maombolezo.

Tunawaombea kwa Mola awape moyo wa subira na uvumilivu. Wananchi wa Wilaya ya Nyasa tunawapa pole nyingi kwa msiba mkubwa uliowakuta na pengo kubwa mlilolipata.

Nawaomba watambue kuwa namna bora zaidi ya kumlilia Mbunge wao aliyewapenda ni kudumisha mema yote aliyofanya na kukamilisha zile kazi ambazo alikusudia kuzifanya lakini hakuweza kufanya hivyo kwa sababu ya kukutwa na umauti. Mwisho nawaomba, Watanzania wote tuungane na familia yake kumwombea marehemu Capt. John Damian Komba mapumziko mema. Amin."

Kwa nukuu hii, inaonyesha dhahiri kwamba Rais Kikwete alikuwa na nia ya kudharau kifo cha Salmin Awadh kwa kuwa yeye alifariki dunia mwanzo kuliko Kapteni Komba lakini hakupata nafasi ya kutajwa na kukumbukwa kwenye hotuba hiyo muhimu kwa taifa.

Kipande hicho cha rambirambi ya maneno 250, kisingeharibika kama mungelikuwa na maneno 50 tu ya kumtaja Marehemu Salmin Awadh na muda wa kuwekwa maneno hayo ungelikuwepo kama angelitaka, maana kama alivyosema Rais Kikwete mwenyewe kwamba taarifa ya kifo cha Kapteni Komba ilimfikia akiwa anaandaa hotuba hiyo.

Swali la awali linarudi tena kichwani mwa Mzanzibari na hasa hasa mwana-CCM: ipi nafasi yako kwenye Muungano? Ipi nafasi yako kwenye vichwa na nyoyo za wenye Muungano huo?

Tafakari. Fanya maamuzi sahihi.

Chanzo: zanzibardaima
 
Zanzibar kuna Rais wake na Awadhi alikuwa ni mwakilishi wa baraza la wawakilishi. Usitake Kikwete aingilie masuala yenu ya ndani

lizaboni kuwa neutral soma makala uielewe
 
BY SHEILA MBAGA Sheila Mbaga is offline
Sheila Mbaga

Join Date : 27th February 2015

Default Re: Taarifa sahihi kuhusu ulinzi wa Dk. WillibrodSlaa dhidi ya upotoshwaji unaoenezwa

[h=1]Ukweli wa Mauaaji haya hapa: Membe, Gotham na Ridhiwani wahusishwa [/h]
Ni kwa kipindi chamuda mrefu kumekuwepo na kikundi kinachoratibu mauaji ya watu mbali mbali. hayatunayoyasikia kwa Dr. Slaa siyo mageni masikioni mwetu bali ni muendelezo wakile kinachoratibiwa na kundi hilo. Ni wazi kuna mipango yaliyoanza kutekelezwakwa baadhi ya wana CCM na baadhi wa wapinzani, leo hii naomba niwatelee ukweliwa haya mauaji yote na mipango ya kuuwa watu wengine....

1. Mjumbe wa NecLudewa: Huyu ndiyo alikuwa mhanga wa kwanza katika mauaji ya hivi karibuni,mjumbe huyu wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, aliwekewa sumu katika kikao chaNEC kilichofanyika mwezi wa 11 mwaka jana katika mji wa Dodoma, bila kupepesamacho uratibu wa kumwekea sumu uliratibiwa na bwana moja anayejulikana kwa jinala Jack Gotham, ambaye ni kada wa Chama cha Mapinduzi.

2. Mjumbe wa Nec waCCM kutoka Kahama: Huyu ni mjumbe wa NEC wa chama cha mapinduzi kutoka wilayaya Kahama, ambaye ni mdogo wake waziri Marry Nagu, naye ni muanga wa kuwekewasumu, ambapo aliwekewa sumu katika kikao hicho hicho kilichoketi Dodomamwishoni mwa mwaka jana.

3. BeatriceShelukindo: Huyu ni mbunge wa Kilindi kupitia chama cha mapinduzi, na ni mjumbea halmashauri kuu ya Taifa kupitia wilaya ya kilindi, ni kwa muda mrefu sanaMama Beatrice amekuwa akiugua na kutibiwa India. Beatrice aliwekewa sumubungeni na wahusika hawahawa ambao nitawataja hapa chini. kama unakumbukaBeatrice Shelukindo alikuwa moja wa wabunge waliokuwa wakali sana kuhusu swalala Richmond ila baadaye alipogundua ukweli akaamua kuwakimbia na kusimama katikaukweli. Ni jambo la kumshukuru Mungu ya kwamba kwa sasa Beatrice yuko nchini naanaendelea vizuri baada ya juhudi kubwa za madaktari wa India kuweza kuondoasumu aliyowekewa.

4. Kapteni Komba:Komba amekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi na mjumbe wa NEC kupitia Nyasa, baadaya mazishi yake yaliyofanyika wiki iliyopita sasa ni wazi kilichomuuwakimejulikana. Komba aliwekewa sumu na hao hao wahusika sababu kubwa sikiwambili, mosi ni ahadi aliyopewa Stella Manyanya kuhusu jimbo husika na pili niwazi Komba alikuwa instrumental katika siasa za Edward Lowassa ambaye anawatoaroho huko CCM katika kinyanganyiro chao cha uchaguzi wa ndani. Ni Komba sikuchache kabla ya kuwekewa sumu alisema wazi wazi kwamba anamuunga mkono Lowassakuwa mgombea wa chama cha mapinduzi.

5. Salum Awadh: Huyualikuwa ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi, kifo chakehakikupishana na cha Komba, pamoja na sifa zote ila alikuwa na sifa moja kubwaambayo ni ujasiri, Ni Awadh aliyediriki kusema mbele ya Mkt Jakaya kwamba kamani kosa la maadili basi wagombea wote ndani ya CCM wana kosa hilo la maadili nasiyo wachache kama tunavyoaminishwa, pili ni Awadh aliyetoa hoja binasfi ndaniya kamati kuu kwamba Nape Nyauye ambaye ni mwenezi wa chama afukuzwe ndani yachama na anyanganywe kadi yake mara moja kwa sababu alishakisaliti CCM na kuwamoja wa waanzilishi wa CCJ, vile vile Awadh aliongezea hoja yake kwamba kwasasa Nape yupo kwa ajili ya kukibomoa chama badala ya kukijenga...

Bwana Awadh aliwekewasumu na ndugu Issa Gavu katika ofisi ya Kisiwandui, siku mbili kabla; nduguGavu alifanya kikao cha pamoja katika hoteli ya Serena akiwa na RidhiwaniKikwete na Jack Gotham ambaye ni consultant kwenye mradi wa vitambulisho vyaTaifa {NIDA), na ndiyo meneja kampeni wa Bernard Kamilius Membe..

Gotham mnano tarehe22.04. 2014 alienda Nchini Bulgaria kupata mafunzo ya kuuwa watu kwa njia yasumu na kisha akarudu na sumu aina ya CYNIDE ikiwa ni sumu mahsusi kwa ajili yakumaliza wale wote wanaoona ni kizingiti kwao katika kukamata dola. hii sumu nikwa ajili ya kuwamaliza wale waliovizingiti kwao ndani ya chama chao na nje yachama chao, ndiyo mana leo hii kusikia kuhusu Dr. Slaa kutaka kuuwawa ni swalaambalo ni serious na la ukweli. Katika hili la Dr. Slaa msimamizi mkubwa niMangula ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho (kama mlivoona kwenye vyombovya habari vya leo), na ni Membe aliyeenda kusini kumfata Mangula....

Mkakati huu unarudinyuma alivyouwawa kijana moja wa Kinyakyusa kisha wakasema ni ajali ya gari(stori hii ilikuwa reported kwenye vyombo mbali mbali vya habari). Kijana huyualiuwawa baada ya kutoa siri za Home Shopping Centre na Ridhiwani kutoa watuSouth Africa kwa ajili ya kumuuwa Bwana Masamaki ambaye ni kamishna wa Tax TRA.

Huu mchezo wa kuuwawatu haujaanza leo, hawa mabwana walianzisha utaratibu wa kutoa watu SouthAfrica na Kenya kwa kazi hiyo tu. wamefanya hivyo kwa Ulimboka Steven ambapowatu walitolewa Kenya na kushirikiana na Ramadhani Ighodu, wakafanya hivyo kwaAbsolom Kibanda (kama unakumbuka kati ya maadui 11 aliyowataja Membe, KIbandaalikuwa moja wao kama mwandishi)...

Mwaka 2012 RidhiwaniKikwete alichukuwa watu kutoka Kenya kwa ajili ya kufanya kazi maalumna mpakasasa watu hao bado wapo nchini ambapo wamepangishiwa nyumba mitaa ya Masakieneo maarufu kama Kilimanyege karibu na Jacks Bar.... Mauaji haya yamekiwayakisimamiwa na Membe na kuratibiwa na Ridhiwani pamoja na Gotham...

Nina uhakika kwambahaya yanafanyika bila Rais Jakaya kujua, hata hapa idara yetu hakuna wanaojuahili swala zaidi ya watu wa karibu wa Membe. Ridhiwani amekuwa akifanya hayayote na hao washirika wake hata bila baba yake kujua na hii ni kwa sababu dogokashaingizwa kwenye biashara haramu mbalimbali likiwemo na la kuuza madawa yakulevya. Kwa sasa ni wazi hawa watu wanafanya jitiada zozote zile waingiemadarakani ili kulinda dhambi zao, na wanafanya kila jambo ili washindeuchaguzi wa mwaka huu, kwa hali hiyo tutegemee mauaji mengi na makubwa kutokeakuanzia sasa.. Na kwa sasa bila kuwaficha ila nafanya haya kwa neema za Mungukuna mpango wa kuangusha helcopter ya Chadema... hawa watu wamekuwa wakipangakufanya haya mambo na kujadili hali ya siasa katika hoteli zifuatazo 1). Serena2). Protea na 3). Collesium Oysterbay...

Ila kwa wale mabibiwa umri kama wangu watakumbuka kifo cha kutatanisha cha Padre Serapius Kombaambapo Membe wakati huo alihusishwa. Komba aliuugua ugonjwa wa kufa ubongo polepole. Komba alikuwa Gombare wa seminari kuu Peramiho, mwandishi mahiri na mtualiyejaliwa upendo ila kwa unyama wa Membe na ushirika wake na Padre SebastianNepachichi walidiriki kukatisha uhai wa padre Komba... Hata hivyo kifo chabalozi wa Libya aliyeuwawa yasemekana kuna mkono mkubwa wa MEMBE..... Membe nimtu hatari sana na kama Taifa tusikubali kurudi kwenye zama za mauaji yakikatili....

Asanteni
Mtoto Sheila.....

like

Pasco, ocampo four and jme like this.

Toa upuuzi wako hapa, hizo habari zenu za kizushi pelekeni TDaima.
 
kwani hadi lini mtajua wazinzibar hamna uzito bara?idadi yenu na square meter zenu zina support hilo mwisho kabisa unafiki wenu ndo unawatafuna mara mtake muungano mara hamtaki....kwa hili mmekua kanyagio la CCM
 
membe akizidi tutaenda kuchoma moto hoteli yako kule mtwara hata sisi umafia tunauweza
 
Kwani hotuba ya rais imegeuka kuwa matangazo ya vifo?
 
gize umeweka mambo mazito sana hapa,haya sie ni wasomaji tu
 
Last edited by a moderator:
Nyie Zanzibar mtabaki kuwa ni koloni la Tanganyika tu! isitoshe mwakilishi wa zanzibar ni sawa na mwenyekiti wa mtaa/kijiji huku Tanganyika kwa idadi ya watu anaowaongoza!
 
mnataka kukumbukwa na mkoloni wenu haha
 
Zanzibar kuna Rais wake na Awadhi alikuwa ni mwakilishi wa baraza la wawakilishi. Usitake Kikwete aingilie masuala yenu ya ndani

Kama zanzibar wana taifa lao inakuaje unashindwa kutambua taifa lako la tanganyika?
 
Zanzibar kuna Rais wake na Awadhi alikuwa ni mwakilishi wa baraza la wawakilishi. Usitake Kikwete aingilie masuala yenu ya ndani
Baraza la Wawakilishi si suala la Muungano, walitaka Rais aseme kisha waanze kulalama kwamba wanaingiliwa na Wabara!
 
Zanzibar kuna Rais wake na Awadhi alikuwa ni mwakilishi wa baraza la wawakilishi. Usitake Kikwete aingilie masuala yenu ya ndani

usiseme hivyo, Kikwete ni mwenyekiti wa CCM, na huyo mzanzibar ni kionogz mwandamiz wa CCM, lazima pawe na ukakasi kutokumbukwa ktk hotuba ya rais, lkn kubwa zaid kama rais wa jamhuri hakutakiwa kutuma salamu za pole kupitia hotuba yke ikiwa huyo mzanzibar hakuwa muwakilishi tu, bali ni mnadhimu na mjumbe wa CC ya CCM.

 
Back
Top Bottom