Rais Kikwete Awashangaa Waliompokea kwa Vilio. Baadhi yao Wakamatwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete Awashangaa Waliompokea kwa Vilio. Baadhi yao Wakamatwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Jan 15, 2012.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Keneth Goliama
  RAIS Jakaya Kikwete jana alipokewa kwa mabango na vilio kutoka kwa wakazi wa Mabwepande walioondolewa kwenye maeneo hayo ili kuwapisha waathirika wa mafuriko, Dar es Salaam.Kilio kikubwa cha wananchi hao ni kuondolewa kwenye maeneo hayo bila kulipwa fidia, jambo ambalo wanalitafsiri kuwa ni dhuluma na uonevu.Mara baada ya Rais Kikwete kuwasili eneo hilo majira ya saa tano asubuhi, watu hao waliokuwa wameandaa mabango waliyanyanyua juu ili kiongozi huyo wa nchi ayaone. Hata hivyo, wakati wakinyoosha mabango hayo, polisi waliokuwa kwenye maeneo hayo waliwanyang'anya.

  Kutokana na tukio hilo, polisi walikamatwa watu tisa kwa kitendo hicho cha kuonyesha mabango hayo kwa madai ya kutaka kusababisha vurugu kwenye ziara hiyo ya Rais.Baadhi ya mabango yalisomeka; “Tumekuwa wakimbizi, tumekuwa waathirika wapya wa maafa badala ya kuwakaribisha wageni wetu (waathirika wa mafuriko).” Hata hivyo, nguvu ya polisi iliyotumika kuwanyang'anya mabango, ilizima mpango huo wa kufikisha ujumbe kwa Rais. Kuona hivyo, baadhi yao, wake kwa waume walianza kuangua kilio kiasi cha ambacho pia kilimshutua Rais Kikwete.Wananchi hao walilalamika kwamba waliwasilisha kilio chao katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam lakini hawakusikilizwa na kushangaa kuona greda likiingia kwenye viwanja vyao na kutengeneza barabara.

  Hata juhudi za Katibu Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye za kuwatuliza wananchi hao hazikufua dafu kwani walisisitiza kutaka kuonana na Rais Kikwete. Baadaye Rais aliwaendea na kuwahoji viongozi wa mkoa sababu za kilio cha wananchi hao. Baada ya malalamiko ya wananchi hao kuelekezwa kwa viongozi wa mkoa, Rais Kikwete aliwaagiza wapeleke vielelezo vya viwanja vyao kwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa ili kutatua tatizo hilo. Walimweleza Rais Kikwete kwamba walivunjiwa nyumba zao za kuishi eneo hilo ili kupisha waathirika... “Mheshimiwa Rais sisi tupo hapa kwa miaka mingi. Tunashangaa Serikali kuja na kuanza kuvunja nyumba zetu bila hata kutulipa fidia.”Wapangaji watambuliwe . Akiwa katika eneo hilo, Rais Kikwete alipingana na uamuzi wa Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Dar es Salaam inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadiki ya kutowatambua wapangaji waliokumbwa na mafuriko mabondeni na kutaka watu hao kufikiriwa na kupatiwa viwanja akisema nao ni Watanzania kama wengine.

  Rais alisema hayo wakati akipokea taarifa kutoka kwa Sadiki aliyemweleza kwamba kulikuwa na mahema 300 yaliyokuwa tayari kwa ajili ya kukabidhiwa kwa waathirika wa mafuriko.Hatua hiyo ya Rais Kikwete inakuja baada ya waliokuwa wa wapangaji walioathiriwa na maafa hayo kukataliwa na kamati hiyo kupewa viwanja. Rais Kikwete alisema kamati hiyo ya maafa inatakiwa kutafakari kwa kina na kwamba hakuna mtu aliyepanga maafa lakini kutokana na kitu hicho kuja ghafla, lazima Serikali isimamie shughuli ya kuwatunza waathirika na kwamba waathirika ambao ni wapangaji lazima wawekwe katika makundi maalumu kwa ajili ya kupewa viwanja.

  “Ili kuondokana na usumbufu na wapangaji, Mkuu wa Mkoa nakuagiza kutengua maamuzi yenu hasa ya kutowapa viwanja wapangaji, maana hawa wote ni Watanzania wenzetu ambao hawakutamani kuishi hivyo,” alisema. Aliwaonya viongozi wanaotaka kujilimbikizia viwanja akisema kazi hiyo inatakiwa kufanywa kwa makini ili kuhakikisha kuwa lawama hazitokei katika ugawaji wa maeneo hayo. Alisema viongozi wote wanatakiwa kuweka mazingira maalumu ili waathirika kujiwezesha badala ya kuitegemea Serikali. Alisema kazi ya kuwatambua na kuwahamisha waathirika inatakiwa kufanywa kwa umakini ili kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza.

  “Kazi hii ifanyike kwa umakini ili kuondoa migogoro. Nyumba zote zihesabiwe na kila mtu apewe namba kabla ya kufika Mabwepande. Baada ya kupewa namba ahamishwe na nyumba ibomolewe ili kuondoa migogoro ya kulipwa mara mbili,” alisema.
  Aliwataka wathamini kuzipiga picha nyumba zote na kuziweka katika kumbukumbu ili kuhakikisha kila anayedai fidia au kutopewa kiwanja ana takwimu ambazo zinaonyesha makazi yake.

  Maji na Umeme
  Rais Kikwete alionyeshwa kusikitishwa kwake na takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) juu ya upatikanaji wa maji. Alionekana kukerwa baada ya kuwauliza maswali viongozi hao ambao walishindwa kumpa majibu kwa ufasaha na kuonekana kutupiana mpira. Alisema majibu waliyokuwa wanayatoa hayaonyeshi kwamba kuna hatua za haraka za kutatua tatizo la maji. Alisema kila siku lazima lita 50,000 za maji zijazwe kwenye matanki kutokana na mahitaji muhimu ya wananchi na kuwataka wahusika kuwa makini.

  Aliuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Mipango Miji, kutenga maeneo ambayo yatatumika kwa ajili ya masoko, viwanda na huduma muhimu ili kuzuia msongamano mjini. Alisema neno dharura lisitumike kuweka miundombinu mibovu na badala yake Mabwepande itumike kama mfano katika kuliweka jiji la Dar es Salaam katika mpangilio wa kisasa.Kuhusu umeme, Rais Kiwete alisema Serikali kupitia ofisi ya mkoa itahakikisha wananchi hao wanapatiwa huduma ya umeme. Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa kupitia kwa Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud, Sh550 milioni zinahitajika ili kufanikisha huduma ya umeme eneo hilo.Alisema kazi hiyo inatarajia kuanza wiki ijayo na kukamilika baada ya wiki mbili.

  Mvutano Msalaba Mwekundu na CCM
  Mvutano uliibuka kati ya Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania baada ya kutakiwa kuondoa bendera na alama zilizofungwa katika mahema kilichoyajenga kwa ajili ya waathirika hao.Mvutano huo ulianza juzi baada ya uongozi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam kutaka mabango hayo kuondolewa lakini uongozi wa Msalaba Mwekundu ulikataa.

  Mmoja wa maofisa wa Msalaba Mwekundu alisema hatua hiyo ya kukataa kutoa alama hizo inatokana na ubaguzi uliofanywa wa kutotaka kukihusisha chama chake kwenye ziara ya Rais Kikwete.Alisema chama hicho ndicho kilichokuwa na mamlaka ya kukabidhi mahema hayo kwa Rais au kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.Taarifa zilizopatikana eneo hilo zilieleza kwamba kulikuwepo na njama za kuonyesha kwamba mahema hayo hayakujengwa na Msalaba Mwekundu, bali ni juhudi za Serikali. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Msalaba Mwekundu kilitumia karibu Sh70 milioni kwa ajili ya ujenzi wa mahema hayo.

  CHANZO MWANANCHI
   
 2. I

  Imurumunyungu Senior Member

  #2
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tubadilisheni safu nzima ya uongozi.Jk anaweza kuwa ni kiongozi mzuri lakini yumo ndani ya chama kisicho watakia mema wananchi.CCM yoote ni corrupt na haina tena huruma na wananchi,viongozi wake wote si watendaji tena bali ni wachumia tumbo.CCM haina budi kung'olewa madarakani through violence sababu non-violence tayari imesha prove failure.
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Tutaendelea kulia na kusaga meno...waulize wale wananchi nani hakumchangua JK na viongozi wengine wa CCM?
   
 4. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Safi sana hii style nimeipenda,nadhani wananchi wa Dar nao wataamka kwani hao ndio wamekuwa mtaji wa ccm,kuliko mikoa mingine.
   
 5. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Good job bro jk!!ni vihereher vyao hao umesahau kuwaambia kuwa kama ungekuwa jua ungewaka kichizi kuzuia mafuriko.
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Watanzania tunaishi kwenye nchi yetu kwa taabu mno


  RIP Dada Regia Mtema
   
 7. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  na tutalia sana. mpaka 2015 ifike? tutalia mpaka machozi ya damu
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  lieni mpaka mkome tena lieni hadi mtapike mlichokula, lieni hadi makamasi yawateremke km maji MANA MLIYATAKA WENYEWE, mi ninalia kwa kusalitiwa na wananch wezangu walioichagua ccm hivyo kilio changu si cha majuto kwani sikuchagua ccm
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo kosa wananchi kulia, wasingesikilizwa!!
   
 10. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #10
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hapana, Kikwete siyo kiongozi mzuri hata kidogo; ni mbabaishaji tu. Angekuwa Kiongozi mzuri katika kipindi cha miaka sita iliyopita, leo chama chake kingekuwa kizuri kwa vile kinafuata uongozi wake. Tanzania tuna ombwe kubwa sana la uongozi ambalo huenda linasababishwa na msimamo wa Nyerere kuwa lazima kiongozi atoke CCM. Kosa kubwa sana la Nyerere ni lile alilofanya la kusahau kuwa chama ni kundi la watu tu, na CCM aliyokuwa nayo haingekuwa sawa na CCM ambayo ingefuatia. Viongozi wengi tulio nao nchini (including Kikwete) wako pale kwa sababu ni wanachama wa CCM tu, siyo kutokana na uwezo wao.
   
 11. T

  TUMY JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vitendo vya hawa polisi maranyingi vimekuwa vikinisikitisha sana, wanahasau kwamba kuna haki ya mtu kutoa maoni, lakini pia kesho yatawakuta wao ama ndugu zao pia, maadamu watu hawakuwa na lengo la kufanya fujo kwanini wasitumie nafasi hiyo kumueleza mkuu wa nchi kero zao ili wasaidiwe sasa wakamlilie nani ambaye atawasikiliza.

  Nitakuja nimtandike polisi makofi siku moja mpaka ajute.
   
 12. Pelekaroho

  Pelekaroho JF-Expert Member

  #12
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,502
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red, Mwenyekiti wa CCM ni huyohuyo JK , haiwezekani wacheza ngoma wakacheza tofauti na midundo ya mpigangoma ambaye ni JK, ki ukweli huyu mganga(Doctor) JK ameshindwa kuweza kuongoza nchi labda tumjaribishe uenyekiti wa kitongoji.
   
 13. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #13
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ninahisi polisi wetu mafunzo yao hayawasaidii,hivi kumuonyesha bango jk ni kosa la kufanya mtu akamatwe?aisee yaani hili kweli ni jeshi la chama wala si la wananchi.Mbona obama, bush, sarkozy,zuma na marais wengine wengi wanabebewa mabango kila siku na wananchi wao sembuse huyu mganga(dokita).Ila natoa angalizo kama kuna mtu ataona hii positi yangu ni ya kichochezi naomba asiisome.
   
 14. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #14
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  JK haeleweki!
  Hao askari walidhani watamfurahisha kwa kukamata hao raia;hawakujua kwamba mwenyekiti wa CCM ni kigeugeu!!!
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Jan 15, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  siku atakayoacha kushangaa basi ndio utakua mwisho wa maisha yake

  yawezekana ana genes za kushangaa za nchi nzima
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Jan 15, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  The President of Tanzania is a demigod, how dare you mere mortal defecate his unquestionable holiness?

  ARREST!!!
   
 17. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #17
  Jan 15, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Loooh!! Umeongea kwa hisia saaaana, Mkuu!!! Ni kweli wasaliti wakubwa ni wananchi wenyewe, wao hawaamini kuwa maovu mengi yanasababishwa na viongozi wabovu wa kisiasa wanaowachagua..!! Hata wakimwaga damu kwa kilio Mungu hatawasikia kwa haki kamwe, bali ni kwa huruma ya hao wanadamu katili ambao ni viongozi wao, tena huyo JK hujitoa ktk lawama ili asionekane mbaya dhidi ya watu wake. Je, inakuja akilini ktk jambo kubwa kama la mafuriko kuwa kamati ya Maafa Dar ilifanya maamuzi ya kwenda huko Mabwepande pasipo Mh. Rais kujua hata chembe ya kile kitakachofanyika juu ya waathirika.......???? I dont believe in that fiction...sijui nyie wenyewe mnaoamini kila kitu cha huyu Mkulu na viongozi wengine.....!!

  Anyways, watz wacha tupate shida mpaka tutakapoona inatosha, maana hatuwezi kulaumu Mungu hatujalii ktk dhiki zetu wakati ni sisi wenyewe ndio tunaojichagulia watawala hovyo,wezi, na wasio na hofu ya Mungu.

  Watz tubadilike na tusikie sauti ya Mungu juu ya kulitendea mema taifa hili, kama tutaendelea na tabia hii ya kuchukulia kila kitu saaawa tuuu, basi hatutafika kokote na tutakufa maskini na wasio na baraka kwa watoto na wajukuu zetu.

  Mungu ni bariki Mimi na Tanzania yangu.
   
 18. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #18
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Thubutu!!! kikwete ndio tatizo kubwa ktk nchi hii. mfano hapohapo kwenye ishu ya mabwepande eti anaonesha kukerwa; hatuitaji kiongozi anayeonesha kukerwa tunataka kiongozi anayewajibika. hapo alitakiwa kuwajibisha wahusika wote na sio porojo tu.
   
 19. Kibona

  Kibona JF-Expert Member

  #19
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 1,021
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Wengi hawakukuangusha ndugu! bali ni watu wanojiita usalama wa taifa ndio waliiba kura, kwahiyo walilie hao walioibiwa kura zao na wanaendelea kunyanyaswa. Cha msingi tutafute njia mbadala ya kuwaondoa ccm maana naanza kupoteza imani ya kuwaondoa ccm kwa sanduku la kura ila nafikiri kwa staili ya misri, Tunisia na hata libya hapa itakuwa rahisi sana maana hata wanajeshi nao wameichoka ccm.
   
 20. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #20
  Jan 15, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hilo la Nyerere ndo limetufikisha hapa, imani aliyokuwa nayo juu ya watu ndani ya CCM ndo imeleta umasikini wa kutupwa, hasa wa ki-fikra. Ni vile tu Mungu hakupenda, ila kama angali kuwepo na kushuhudia BWM alivyomsaliti, asingali tamani tena kuwa mwana-CCM.

  RIP Nyerere, shida hii ya CCM ulotuachia si sawa na kifungo juu ya wa-TZ.
   
Loading...