Rais Kikwete awaonya UVCCM kuacha ukuwadi

Rais Kikwete awaonya UVCCM kuacha ukuwadi

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
123,250
Reaction score
98,243
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM Taifa,amewaonya baadhi ya wanachama wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi kuacha kuwa makuwadi wa baadhi ya viongozi wanaotaka urais kupitia chama hicho.

Duu! Kumbe hata Rais wa nchi amewagundua hawa vijana wanaotumika kisiasa ?

==============================

Dodoma. Rais Jakaya Kikwete amewataka vijana wa CCM kutokuwa makuwadi na madalali wa wagombea urais katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba, mwaka huu.

Rais Kikwete aliyasema hayo mjini hapa jana alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa kwanza wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu wa CCM.

"Vijana wasigeuke kuwa makuwadi wa kuwahonga vijana wenzao ili wamchague mtu fulani. Kwa kufanya hivyo watakuwa wametoka kabisa nje ya mstari.

"Tunataka vijana watakaosema tunatafuta viongozi wa Taifa hili, ila watu wa aina hii hapana," alisema Rais Kikwete.

Alisema lengo la kuanziasha shirikisho hilo ni kuwaandaa vijana hao ili waujue uongozi na waweze kuwa viongozi wazuri katika siku za baadaye.

"Viongozi wa vijana wanasafirishwa wanaletwa hapa Dodoma kwa ajili ya kumsikiliza mzee fulani, ndiyo maana siku hizi hoja ya vijana siyo tishio kwa mtu yeyote kwa sababu hawana mawazo ya kutoa kwa ajili ya kukijenga chama na Taifa," alisema Rais Kikwete.

Pia, aliwataka vijana hao kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola katika Uchaguzi Mkuu ujao kwa kuwa hilo ndilo jukumu lao.

"Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi tunachotaka sisi ni CCM iendelee kuongoza Tanzania na wapinzani waendelee kuisoma namba kama ilivyokuwa kwa miaka mingine, nawaamini, nina matumaini na nyie pia CC ina matumaini makubwa ya kukivusha chama hiki katika Uchaguzi Mkuu ujao," alisema Rais Kikwete.

Chanzo: Mwananchi
 
Source??!!!

If so. . . .kuwa kuwadi kuna adhabu yeyote??!!
 
akumbuke na alichofanya makonda kuhusu lowasa wakati akiwa uvccm mbona hatukusikia anatoa kauli
 
mbona na yeye aliwatumia hao makuwadi uvccm alipokuwa anautaka urais!!!!!huyu jk ni mnafiki sana,miaka yote kumi amezurura dunia nzima kuombaomba,leo hii mwisho wa utawala wake umefika anawatukana wafadhi...ni wa kudharau tu huyu.

wewe unataka upewe msaada kwa masharti kuwa ukitaka usaidiwe lazima upitishe sheria ya ushoga
 
Na uhuru wa Habari pia, kajidai uongozi wake umetupa sana uhuru alafu mwisho anasaini sheria za kipumbavu
 
wewe unataka upewe msaada kwa masharti kuwa ukitaka usaidiwe lazima upitishe sheria ya ushoga

sharti hilo wote tulimuunga mkono,tatizo lake ni kwamba masharti ya kupambana na ufisadi ndio anayoyakataa yeye sababu chama chake na ufisadi ni damdam...misaada imesitishwa sababu ya ufisadi unaoigusa hadi ikulu!!!!!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM Taifa,amewaonya baadhi ya wanachama wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi kuacha kuwa makuwadi wa baadhi ya viongozi wanaotaka urais kupitia chama hicho.

Duu! Kumbe hata Rais wa nchi amewagundua hawa vijana wanaotumika kisiasa ?

hawa ndio wale wanaohongwa mudaa wa maongezi ya laki mbili, matokeo yake wanakuwa makuwadi wa wagombea urais
 
sharti hilo wote tulimuunga mkono,tatizo lake ni kwamba masharti ya kupambana na ufisadi ndio anayoyakataa yeye sababu chama chake na ufisadi ni damdam...misaada imesitishwa sababu ya ufisadi unaoigusa hadi ikulu!!!!!

tatizo hata tafsiri ya fisadi hujui
 
DSC02968.jpg
 
hawa mabwana wadogo Mara nyingi wamejigeuza miungu watu,kuzungumza chochote apendacho bila haya wala Aibu / kibaya zaidi kuwateta hata wanaokifahamu chama kwa kina /
 
Rais Kikwete amewalenga akina HAMY - D, MUSSA ALLAN, laki si pesa, Mingoi, Mzee, FaizaFoxy, Ocampo four, Ruttashobolwa, Ritz na wengine ndani ya UVCCM ambao wameamua kuwa makuwadi wa fisadi Lowasa
 
hawa mabwana wadogo Mara nyingi wamejigeuza miungu watu,kuzungumza chochote apendacho bila haya wala Aibu / kibaya zaidi kuwateta hata wanaokifahamu chama kwa kina /
Kweli kabisa aisee. Hawa jamaa wanakera sana
 
Hivi ni kweli el alijimilikisha jengo la umoja wa vijana makao makuu?
 
mbona na yeye aliwatumia hao makuwadi uvccm alipokuwa anautaka urais!!!!!huyu jk ni mnafiki sana,miaka yote kumi amezurura dunia nzima kuombaomba,leo hii mwisho wa utawala wake umefika anawatukana wafadhi...ni wa kudharau tu huyu.

Ameona madhara yake, kuwa wanakuchezea tu..
 
Ahya bwaana sisi yetu ni macho kwa sasa wacha mtoane ngeu,mkishatoana macho ndio tunamalizia kazi ndogo sana ya kuwaelekeza kibra
 
Rais Kikwete amewalenga akina HAMY - D, MUSSA ALLAN, laki si pesa, Mingoi, Mzee, FaizaFoxy, Ocampo four, Ruttashobolwa, Ritz na wengine ndani ya UVCCM ambao wameamua kuwa makuwadi wa fisadi Lowasa

mkuu kumbe faiza ni uvccm?
 
this guy is creating more enemy that he wont be able to handle akitoka kwenye urais, cjui kwa nn anadhan akitoka kwenye urais ataendelea kua na power izi izi.... he will know better akitoka
 
this guy is creating more enemy that he wont be able to handle akitoka kwenye urais, cjui kwa nn anadhan akitoka kwenye urais ataendelea kua na power izi izi.... he will know better akitoka

Watu kama nyie ndio mmetufikisha hapa, Yaani Mtu asiseme jambo kisa eti akitoka yatamkuta!!! kwani ni uongo kuwa UVCCM, wamekuwa makuwadi?
 
Back
Top Bottom