Rais Kikwete ateua wakuu wa mikoa mipya

Rais Kikwete ateua wakuu wa mikoa mipya

Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Channel Ten, Rais ameteua wakuu wa mikoa mipya minne.

Wamo Msangi na Magadura.
==============
​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Wakuu wa Mikoa.

Dkt. Rajab Mtumwa RUTENGWE ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa KATAVI. Kabla ya hapo Dkt. Rutengwe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.

Ndugu Magalula Saidi MAGALULA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Ndugu MAGALULA alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi.

Ndugu Paschal Kulwa MABITI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU. Kabla ya hapo Ndugu MABITI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.

Kapt. Asery MSANGI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE. Kabla ya hapo Kapt. MSANGI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.

Uteuzi huu unaanza tarehe 15 Machi, 2012. Wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam, Jumatano tarehe 21 Machi, 2012 saa 04:00 asubuhi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Machi, 2012

Hongera zako mzee P Mabiti..
 
Kwa nini anafanya uteuzi nusunusu? kwa nin i hakuteua wa kuziba nafasi za hao walioteuliwa kwenye nafasi nyingine? Hivi anafikiria maendeleo ya sehemu hizo zilizoachwa wazi? Au anataka mpaka watu waanze kupiga kelele tena ndo afanye uteuzi mwingine?
 
Maskini Ole Njolay. wananchi wote wa mikoa uliyopita wanajua utendaji wako wa kazi haswa mkoa wa mwanza. Hapa nimeamini huyu mzee hawezi kukuacha hata siku moja mkipishana..
anaandaliwa madaraka makubwa zaidi!
 
ama kweli kama ni raisi Tanzania tunaye, tena anayeyajua vizuri maswala ya centralization na decentralization, kweli kweli nazi ni nazi tu haiwezi kuwa juicy ya nanasi...
RIP JK
 
inasikitisha sana tunapoambiwa kila siku kuwa serikali haina fedha na inashindwa kulipa japo mishahara kwa watumishi wake kwa wakati unaotakiwa lakini rais anaamua kugawa nchi vipande vipande. Leo unaambiwa mkoa mpya wenye wilaya mbili; kama sio kukosa uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi tuelewe nini kwa hilo.

Hivi kama taifa hatuna mambo ya msingi ya kufanya ama viongozi wetu wanajikita katika kupeana nafas na kulitafuna taifa kwa faida yao na familia zao?

inauma sana
 
Kazi ipo nami mnikumbuke japo uafisa fulani katika wilaya hizo mpya maana doro imenichosha akina mbiti nipeni mazee tugawane kilichopo!!!!!!!
 
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Channel Ten, Rais ameteua wakuu wa mikoa mipya minne.

Wamo Msangi na Magadura.
==============
​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Wakuu wa Mikoa.

Dkt. Rajab Mtumwa RUTENGWE ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa KATAVI. Kabla ya hapo Dkt. Rutengwe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.

Ndugu Magalula Saidi MAGALULA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Ndugu MAGALULA alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi.

Ndugu Paschal Kulwa MABITI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU. Kabla ya hapo Ndugu MABITI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.

Kapt. Asery MSANGI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE. Kabla ya hapo Kapt. MSANGI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.

Uteuzi huu unaanza tarehe 15 Machi, 2012. Wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam, Jumatano tarehe 21 Machi, 2012 saa 04:00 asubuhi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Machi, 2012

Pale kwenye majina ya Red ndipo nataka kupasemea: Kwamba Mkuu wa Mkoa mpya wa Simiyu Bwana Paschal Mabiti anaendelea kuula tu kutokana na uteuzi wa Kiwete. Kwa sifa gani hasa huyu Paschal Mabiti ni yeye tu siku zote mara Ukuu wa Wilaya mara ukuu wa Mkoa. Hivi katika Watanzania zaidi ya 40 millioni hakuna Watanzania wengine wanaoweza kuteuliwa kuwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa kweli???? Tanzania hii ina mikoa siyo zaidi ya 30, sasa sielewi ni kwanini Kiwete huwa anarudiarudia walewale wa tangu enzi za Mwalimu Nyerere. Kwa kazi nzuri ipi hasa? Je ni hii ya kutisha na KUWAFUKUZA WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU KWENYE MAENEO YAO WALIMOZALIWA KWA KISINGIZIO CHA KUWAPISHA WAWEKEZAJI??? Kwa kweeri sielewi mura!

Kuna hili la mgogoro wa MAKAO MAKUU ya Mkoa mpya wa Simiyu. Hivi karibuni wakti wa ziara ya PM Pinda vyombo vya habari vililonga kuwa kuna mvutano wa wapi yawe Makao makuu ya mkoa Simiyu. Wakazi wa wilaya kongwe ya Maswa wakidai Makao makuu yawe Maswa kwa vile wilya hiyo ndiyo imezaa wilaya mpya za Meatu na Bariadi lakini Serikali ina mpango wa kupeleka Makao makuu wilaya ya Bariadi ambako Bwana Mabiti atakuwa akivinjari. PM Pinda alikutana na mvutano huo hata akatishia kwamba atamshauri Rais Kiwete aufute Mkoa wa Simiyu au Kiwete ndiye atakayeamua wapi yawe Makao makuu ya Mkoa huo!

Ili kuondoa utata wa wapi Makao Makuu ya Mkoa wa Simiyu yatakuwa,uteuzi wa Wakuu wapya wa Mikoa ukiwemo Simiyu ulipaswa kwenda sambamba na TANGAZO LA OFISI YA RAIS/IKULU kuwa Makao Makuu ya Mkoa huo ni MASWA au BARIADI kuliko kuwaacha Wananchi wa Mkoa huu mpya na mkanganyiko wa mawazo. Hili ndiyo tatizo kubwa la Serikali ya Kiwete na safu yake ya Uongozi. Kwamba yeye kama Rais ni mwoga wa kuchukua maamuzi na Washauri wake wakiwemo Waziri Mkuu/Mawaziri husika wakiwa wanashindwa kumshauri ipasavyo!



DC Mabiti Aamuru Wachimbaji Dhahabu Waondoke


Views

​
Mkuu wa wilaya Singida Paschal Mabiti akizungumza na wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu kijiji cha Sambaru wilayani humo, ambapo aliwapa siku tatu hadi ijumaa wiki hii kuhakikisha wameondoka kwenye eneo hilo ili kumpisha mwekezaji kampuni ya Shanta.

​
Mchimbaji George Stiven,kwa niaba ya wenzake akiomba waongezewe muda ili waondoke kwenye eneo hilo kama ilivyoamuliwa na serikali kwa ajili ya kumpisha mwekezaji anayetarajia kufungua mgodi,baada ya kukamilisha kazi ya kutafiti madini ya dhahabu.
​
Baadhi ya askari kikosi cha kutuliza ghasia waliofuatana na mkuu wa wilaya ya Singida Paschal Mabiti, wakiwa kwenye eneo la mkutano, tayari kudhibiti lolote linaloweza kuhatarisha uvunjifu wa amani
 
Kweli tutafika 2015 hoi kama wanaoteuliwa wote ni maswahiba wasio na vision namna hii

JK mwenyewe hana vision sasa anawezaje kuteuwa watu wenye vision..yaani yeye hapo ndo kaona kateuwa kweli kweli ..yaani hao ndo top layer kama lile la maharage kule MKWAWA kwa mzee wangu CHALE...
 
hongera wakuu wa mikoa sasa tunasubiri wakuu wa wilaya maana wakuu hawa wa wilaya hawaelewi hatima yao na wanachokifanya ni kuchukua chao mapema.

hata wasipokuwepo kwani wana kazi gani hasa? mzigo kwa walipa kodi tuuu!!!
 
Kuna hili la mgogoro wa MAKAO MAKUU ya Mkoa mpya wa Simiyu. Hivi karibuni wakti wa ziara ya PM Pinda vyombo vya habari vililonga kuwa kuna mvutano wa wapi yawe Makao makuu ya mkoa Simiyu. Wakazi wa wilaya kongwe ya Maswa wakidai Makao makuu yawe Maswa kwa vile wilya hiyo ndiyo imezaa wilaya mpya za Meatu na Bariadi lakini Serikali ina mpango wa kupeleka Makao makuu wilaya ya Bariadi ambako Bwana Mabiti atakuwa akivinjari. PM Pinda alikutana na mvutano huo hata akatishia kwamba atamshauri Rais Kiwete aufute Mkoa wa Simiyu au Kiwete ndiye atakayeamua wapi yawe Makao makuu ya Mkoa huo
Mbona makao makuu ya mkoa wa Simiyu ni Bariadi tayari washasema kwenye Tangazo lao la mikoa mipya.
 
Huyu Pascal Kulwa Mabiti alikuwa madarakani tangu nikiwa Darasa la kwanza ndie aliyekuwa kijana Machachari waliyesema tamridhi Paul Bomani Mwanza, na alikuwa Mbunge wa Mwanza Mjini kwa kipindi kimoja tu, na kupotelea Dar kwenye hivyo Viwanda TEXCO ulaji ulikuwa bora kuliko Ukuu wa Mkoa.

Angalia, Sasa ni Mkuu wa Mkoa Tena, Mimi sio mtoto Ni Sio Kijana, bado wanapeana Vyeo; Lini watatukumbuka Sisi??

Kweli Rais hakuona Kijana yoyote???
 
Back
Top Bottom