Rais Kikwete ateua wakuu wa mikoa mipya

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Channel Ten, Rais ameteua wakuu wa mikoa mipya minne.

Wamo Msangi na Magadura.
==============

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Wakuu wa Mikoa.

Dkt. Rajab Mtumwa RUTENGWE ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa KATAVI. Kabla ya hapo Dkt. Rutengwe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.

Ndugu Magalula Saidi MAGALULA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Ndugu MAGALULA alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi.

Ndugu Paschal Kulwa MABITI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU. Kabla ya hapo Ndugu MABITI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.

Kapt. Asery MSANGI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE. Kabla ya hapo Kapt. MSANGI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.

Uteuzi huu unaanza tarehe 15 Machi, 2012. Wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam, Jumatano tarehe 21 Machi, 2012 saa 04:00 asubuhi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Machi, 2012
 
Hongera wakuu wapya wa mikoa. Nasubiri kwa hamu katiba mpya, tuachane kabisa na huu mfumo wa kugawana vyeo mezani.
 
hongera wakuu wa mikoa sasa tunasubiri wakuu wa wilaya maana wakuu hawa wa wilaya hawaelewi hatima yao na wanachokifanya ni kuchukua chao mapema.
 
Kazi kubwa ya Kikwete ni kuteua. Hata juzi alisisitiza 'nileeteni mapendekezo niteuwe wajumbe wa Tume ya Katiba'! Hakai chini na kutathmini, tangu aanze kuteua imeleta impact gani? Au hadhani wakati umefika wa kubadili mfumo?
 
naona lile picha letu la uswahiba linaendelea tuuu...huyu ndo Baba Mwanaasha
 
Mkuu, hebu nipe essence ya kuwa na mkoa wenye wilaya mbili!


MASIKINI KIKwete, hata MABITI? Huyu mtu alitakuwa kupumzika zamani. Amekuwa serikalini taangu mimi nasoma akiwa mbunge wa Mwanza. Lakini kubwa ni mtuhumiwa mkubwa wa ukiukwaji wa haki za binadamu. Mnafahamu ili ishu ya Nyamongo? Alichoma nyumba za watu moto na hata kuuwa.

Tume ya haki za binadamu na utawala bora imemtaja mara nyingi kuwa ni mtu anayestahili kufikishwa mahakamani. Si bora angemchukua SELELII au anataka kumpa ukuu wa wilaya. Haya yetu macho...
 
Hali ilivyo ni mbaya sana kifedha katika mikoa iliyopo, fedha za mafuta ya magari, vifaa vya ofisi na uendeshaji
wa ofisi zilizopo ni kama vile hakuna...sijui hizi za wakuu wapya wa mikoa zitatoka wapi??? Eee Mungu ibariki Tanzania!!
 
unaweza ukasikia ridhiwan kapewa ukuu wa wilaya.. Usishangae sana jiulize vigezo gani vinatumika??
 
Kweli tutafika 2015 hoi kama wanaoteuliwa wote ni maswahiba wasio na vision namna hii
 
Hongera sana mkuu wangu kapteni Msangi! Unastahili kwa kweli. JK nione namimi basi ukuu wa Wilaya, lol.
 
Wamefanya nini cha maana katika wilaya walizotoka mpaka wamepandishwa daraja?hakuna innovation wala creativity hapo
 
Atapeta kwenye ukuu wa wilaya. We subilia utaona na hapo ndipo nyie wenye loho mbaya mtajibeba!!!

Mkuu kwa jinsi ninavyojua utamaduni wa CCM mtu akishakuwa Waziri au Naibu Waziri huwa wanampa Ukuu wa Mkoa. Kwa Masha hana chake tena. Labda asubiri Wakuu wa Mikoa na Mabalozi wanaostaafu anaweza akapata nafasi. Kinachonisikitisha ni kwa nini JK kamdisi kiasi hiki wakati yeye ndiye aliyempandisha vyeo haraka haraka hatimae leo anashindwa pa kumchomeka!
 
Back
Top Bottom