Rais Kikwete apangua Baraza la Mawaziri

Status
Not open for further replies.

kiparah

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,173
114
Hatimaye Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri ambapo mawaziri kadhaa wameondolewa, wapya wameingizwa na wengine kuhamishwa wizara huku kadhaa wakiendelea kushika nafasi zao.
[video=youtube_share;vLYw0ZkF_-g]http://youtu.be/vLYw0ZkF_-g[/video]​

- Rais amemteua mbunge mwingine mpya - Bi. Saada Mkuya Salum
- Imeelezwa kuwa tukio hili litakuwa LIVE kwenye vituo vya televisheni na baadhi ya redio.
- Wizara ya Nishati na Madini itaongezewa naibu waziri na ikibidi baadae itaweza kugawanywa...
- Mawaziri watawajibishwa kisiasa lakini waliosababisha waziri awajibike hawataachwa!
- Kuanzia sasa akiwajibishwa Waziri basi na watendaji wote walio nyuma yake watawajibishwa\

NAAM:
ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI


MAWAZIRI

1. OFISI YA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,


2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,


3. OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,


4. WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi
Dr. John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,


Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,


5. NAIBU MAWAZIRI


OFISI YA RAIS

HAKUNA NAIBU WAZIRI


6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,


7. OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,



8. WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
 
Muda wote wakuu tumekuwa tukisisitiza habari nyeti kama hizi muwe mnaweka source,nini chanzo cha habari yako mkuu isije ikawa unasema saa kumi atatanganza baraza la Mawaziri akaja tangaza jumatano week ijayo!
 
Hatimaye Rais Wenu Kikwete atatangaza Baraza la Mawaziri saa 10 Jioni ya leo Ijumaa.

SOURCE: Bigbro.
Mh.Bigbro,Kikwete ni Rais wetu mimi na wewe haijalishi ulimpigia kura au hukumpigia! Labda kama wewe ni raia wa marekani kama mnavyopenda mueleweke.Haina maana kama humpendi basi ndiyo anakuwa siyo rais wako
 
Hatimaye Rais Wenu Kikwete atatangaza Baraza la Mawaziri saa 10 Jioni ya leo Ijumaa.

SOURCE: Bigbro.

Jana asubuhi tumeambiwa atatangaza wakati wowote kuanzia sasa; akatangaza wabunge wa kuteuliwa. Leo asubuhi kuna mtu amekuja na thread hapa kwamba Baraza litatangazwa saa nne na sasa wewe unakuja na news kwamba litatangazwa saa kumi. Huenda wote mko sawa kwa kuwa kwa kizungu saa nne ni saa kumi na saa kumi ni saa nne.

Vipi ameitisha waandishi wa habari au itakuwa ni TBC1 peke yake?

Let us keep on waiting kwa kuwa lazima atatangaza wakati wowote!
 
Hebu rekebisha hivi: Hatimaye rais JK atatangaza "Baraza la mchwa wakeketaji"; sounds better kwa sababu bila kuwaadabisha hao wanaotuhumiwa hata hawa it is only a matter of time wataanza kukeketa mali ya umma; hebu kaa chonjo uone prophesy yangu inavyo-jimanifest.
 
Kweli Mtanzania Mtu Mzima ... kuna mweye shauku ya dhati kuhitaji kujua ..huo mkusanyiko mpya ..wa hao watu ..!! Kwani unatofauti gani na ule uliopita? Gari wabadili rangi au Dereva ili kupata safari yenye matumaini na neema????
 
Hamna taarifa ya ikulu isiyovuja, huenda hii pia ni kweli, maana tetesi nyingi tu za JK huwa zinakuwa kweli.

Jana kuna mtu alileta ya Mbatia na baada ya masaa kadhaa ikawa kweli.

Mimi naweza kuamini tu maana hakuna hata cha maana sana kwenye hilo baraza hata likifichwafichwa! Wanondoka wezi wazoefu wanaingia wezi trainee na baada ya muda tu tunaanza kulizwa kama kawaida. Hakuna ahueni tutakayoipata mpaka CCM ing'oke wandugu!

Hapa ni sawa na kutibu malaria kwa dawa ya kutuliza maumivu, kichwa kitapoa lakini baada ya muda kiataanza kuuma tena. Ni lazima upige dose ya malaria hakuna short cut!
 
Jana nimepita home, nikamkuta Dingi ameandaa sherehe. Sasa sijui na yeye ameteuliwa kuwa Waziri.
Nilipombana sana akaniambia nimepigiwa simu lakini usimwambie mtu.!!!
 
Hatimaye Rais Wenu Kikwete atatangaza Baraza la Mawaziri saa 10 Jioni ya leo Ijumaa.

SOURCE: Bigbro.

Wewe sio Rais wako?. Hii ndiyo hasara ya kula sana haadi unavimbiwa.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom