Rais kikwete angalia ulipotoka

Grader

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
445
64
WILAYA ya Bagamoyo Mkoani Pwani inadaiwa kuongoza kwa ulimaji wa zao haramu la majani aina ya bangi.
Hayo yalithibitishwa na Mkuu wa Upelelezi Mkoani Pwani, Bw.Alfonse baada ya kufanya mchakato wa kutokomeza mashamba hayo wilayani humo zoezi ambalo linaendelea.

Amesema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu wameshateketeza zaidi ya hekari 15 ya zao hilo haramu wilayani humo.

Amesema wameshatekeza mashamba hayo ambayo waliyagundua katika maeneo tofauti mkoani humo na wakiyakuta wanayateketeza.

Amesema mkoa huo unafanya operesheni maalumu ya kuteketeza zao hilo ambalo wakazi wa mkoa huo hulima katika mashamba yao wakichanganya na mazao mengine ya chakula.

Juzi Mkuu huyo alisema waliteketeza heka mbili ya shamba ambalo lilikuwa limepandwa zao hilo la bangi peke yake katika kijiji cha Kibindu wilayani humo.
 
Yeye mtu wa Dar ngudu yangu. Chalinze Bagamoyo hapajui mpaka akistaafu akaishi zake upepo unakovuma, USA RIVER AREAS Arushaaaaa!
 
Back
Top Bottom