Naunga mkono hii. Si sawa kuwa na wafanyakazi wageni hata kwa kazi ambazo wananchi wanziweza.
Binafsi nafanya kazi katika kampuni za kigeni, tatizo hilo ni kubwa. Sioni hata haja ya Rais kuangalia kama kuna umuhimu wa HR's kutoka nje!
Kuhusu mamlaka za kutoa vibali, nadhani hatuhitaji mabadiliko. Kama ni mabadiliko ya sheria, labda tuwe na sheria ya kulazimisha makampuni haya kutangaza kazi nchini kwanza, kwa maana ya Watanzania kuwa kipaumbele, kabla ya kuleta wageni. Wizara na idara hazina tatizo kwa maana ya utaratibu. Hata kama vibali vingetolewa na nani kama Idara imeamua kutokuwa na uadilifu na uzalendo (of which ndiyo tatizo kubwa sasa) bado vibali vitatolewa holela tu. Na naweza kusema mpaka sasa Tanzania ni kati ya nchi ambazo ni rahisi kuingia, hata kama unaenda kuuza kandambili Kariakoo! Hatuhitaji kufanya comparison na nchi yoyote, siyo EA au wapi?