Sifa ya kazi siyo kisomo peke yake au uwezo wa kufanya kazi kitu kikubwa kinachofanya wafanyabiashara kuajiri wafanyakazi toka nje ya nchi ni uaminifu, kitu tunatakiwa tujenge tabia ya kuwa waaminifu watanzania ili kujenga imani na wafanya biashara. Mwekezaji anafungua Hoteli mtu anaajiriwa anajisikia ni haki yake kumwibia tajiri na wageni wanaofikia hotelini kwa kisingiziyo ugumu wa maisha, kufanya starehe zake au mshahara hautoshi, hayo pia yanafanyika katika maduka sasa kuna mfanya biashara atakubali kufanya biashara huku akipata hasara. Mpaka pale tutapokua tunaheshimu kazi zetu na kujenga tabia ya kuwa waaminifu wafanya biashara wakilazimishwa kuajiri wananchi watafunga biashara zao.Mbele ya macho yetu tunaona mtu anaajiri dereva wa Prado yake akimwachia gari peke yake kosa atapakia abiria hata watu kumi na tano kuwapeleka tandika na anarudi haraka, kwa kweli tutakuja fikia hata madereva watatoka nje, kwasababu watu hawana pesa lakini tamaa na starehe wameweka mbele kwahiyo wanatafuta pesa kwa njia yeyote.