Lakini tukumbuke hakujiendea tu huko, bali kaalikwa jamani, huwezi kuacha kuendelea kutafuta eti kwa vile unadai 400M.....sidhani kama marekani ni mbaya kwa kila taifa, kuna nchi kibao zimenyookewa kwa sababu ya marekani, mfano S. korea, Taiwan, China yenyewe nk...wachina walikuwa na kasumba hiyo ya kumuona kila mtu adui au anahira, lakini baadaye wakagundua kuwa huwezi kundelea bila marekani...Tatizo sisi weusi hatujui tumia nafasi za wazi wanazotupa hao watasha kufunga magori, na tatizo la kupaisha mipira halipo kwa viongozi tu, hata sekta binafsi, mbaya zaidi kila mtu kageuka kuwa mwanasiasa, mpondaji, do we really analyse issues at au ndio JF imekuwa attacking machine dhidi ya JK au serikali? Let us be creative...tuambiane jamani isije ikawa huu nao ni mtandao wa mtu mwenye malengo ya 2010....
Nina imani tunachebwachebwa kuhusiana na lile dili la AFRICOM. Tusipokuwa macho na kuuliza right questions, pengine tunaweza kuuvaa mkenge. Au ni mimi tu?Baada ya uhusiano wa karibu na Uingereza, Israeli, nadhani Tanzania ni ya TATU sasa!
Nini kinaendelea hapa? hatuna mafuta, hatumo kwenye ukanda wa UGAIDI au tunayo URANIUM?
Ameshafika. Atakuwepo mpaka jumamosi August 30.
Siamini kama mkuu huwa anapata hata muda wa kupitia mafile kwa kuwa kila siku youko on board. Kwa hali hii hawezi tambua kama kuna matatizo ya wananchi, ndiyo maana alipofanya ziara huko mombo (kama mmoja wetu hapo juu alivyotuambia) aliuliza juu ya shida za wananchi. Hivi kweli mkuu hajui kwamba kuna inflation karibu katika kila kitu, barabara mbovu, Less than ten percent ya watanzania ndio wanapata huduma ya nishati ya umeme, bara bara ni mbovu na kwamba watanzania wanasubili maamuzi ya serikali juu ya Richmond, EPA, etc. Hoja za kujibu anazonnyingi, ila hawezi kukata mti aliokalia na ndo maana anauliza wananchi kama wana matatizo wayataje ingawa yote anayajua. Born voyage mwanakwetu, NY.. hiyo ni asili yako. Mbona Sarajevo huendi?