kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,199
- 16,868
Nchi yetu ni maskini sana, hatuna pesa za kutosha kugharamia mahitaji ya msingi kama vile afya, elimu, maji, umeme, ulinzi, mahakama n.k.
Hivyo tungependa kuelekeza kila shilingi katika kusukuma mbele upatikanaji wa mahitaji haya ya msingi kwa wananchi badala ya kugharamia utunzaji wa marais wengi wastaafu kwa muda mrefu. Inajulikana kuwa mwisho wa urais ni miaka 10 tu baada ya hapo kiongozi huyo atastaafu na mtamtunza kama rais mstaafu hadi mwisho wa uhai wake.
Sasa hali itakuwaje kama mtamchagua rais mwenye umri mdogo?. Kwa mfano, mkichagua rais mwenye miaka 35 au 40 atamaliza vipindi 2 vya urais akiwa na miaka 45 au 50 tu, hivyo kodi zetu zitatumika kumtunza mtu huyo kwa kipindi kirefu sana cha kuazia miaka 20 - 40 hadi hapo atakapofariki dunia.
Hili sio jambo jema kwa nchi maskini kama sisi kuwa na msururu mrefu wa marais, makamu, mawaziri wakuu wengi kwa wakati mmoja watakahitaji kulipwa, kutunzwa, kulindwa na kusababisha foleni ndefu wanapopita barabarani.
Umri wa kuwa rais uwe angalau kuanzia miaka 45 ili tuokoe kodi zetu kwa kugharamia utitili wa VIJANA wastaafu wengi kwa gharama kubwa kwa muda mrefu.
Mimi binafsi siwezi kutoa consent yangu kuruhusu kodi yangu itumike kugharamia rais mstaafu mwenye miaka 45 au 50 labda ipelekwe huko bila ridhaa yangu.