kavulata
Umejadili jambo la mmsingi sana ila sasa umesimamia msingi dhaifu.
The delicacy of the issue inabebwa zaidi na instability na wala si pesa za kujikimu hao wastaafu vijana. Ikumbukwe kuwa nchi nyingi za africa si imara kitaasisi hivyo misingi/mifumo yake ni rahisi sana kuyumbishwa na influential individuals. Sote tunafahamu uzito wa nafasi ya rais wa nchi kimamlaka na kimadaraka. Haiwezekani kwa mtu aliyepata kufikia ngazi hiyo kupata fursa yenye madaraka makubwa ya jinsi hiyo baada ya kustaafu, madaraka matamu jamani, ataishije katika "ujana" wa muda mrefu thereafter pasipo hayo makuu?
Ndiyo haya sasa tunayaona ya kina Kagame, Kabila, Nkurunziza na "vijana" wote waliopata kuukwaa huo u-mungu mtu mapema kubaki waking'ang'ania madarakani kila kukicha. Naaam wakafanye kazi gani tena? Na bora tu waking'ang'ania hapo maana wakiwa pembeni ni hatari zaidi kwa stability ya serikali yoyote sababu yeyote aliyepata kuwa rais wa nchi anabaki kuwa an influential figure so ukiongeza na mentality ya "bado nimo" ni hatari kubwa.