Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Rais John Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na mafanikio ya Mbwana Samatta. Ni jambo jema kumsifia kiongozi wa nchi akiutambua uwezo wa mwanamichezo. Rais Magufuli anazitambua jitihada za wanamichezo wa nchi hii. Lakini yapo mambo ambayo kimsingi yanakwamisha kuibuka na kufanikiwa kwa wanamichezo.
Serikali izitazame upya BMT na TOC, haya ni majipu yanapaswa kutumbuliwa mapema iwezekanavyo. BMT halina ubunifu wa aina yoyote ile ambao unalingana na sababu za chombo hicho kuwepo, BMT inashindwa kuutetea uwepo wake, vilabu vya Yanga, Simba vinafanya mambo mengi tu ambayo hayakemewi na BMT. Vyama vingi vya michezo vinaendeshwa na watu wale wale miaka nenda miaka rudi, BMT hawana ushawishi wowote ule wa kuleta mabadiliko ndani ya vyama hivyo.
TOC inapata fedha nyingi kutoka kamati ya olimpiki ya kimataifa, fedha hizo zinatumika vipi?. Ipo haja kwa waziri Nape Nnauye kutoa agizo la ukaguzi wa fedha ndani ya TOC. Majirani zetu wakienda kwenye olimpiki wanakuwa wamefuata medali, sisi tunaenda kuuza sura na tukirudi nchini, yule mkuu wa msafara anaanza kutoa rundo la visingizio. TOC ifumuliwe na kuundwa upya kabisa, hili ni jambo linalowezekana na lipo ndani ya mipaka ya waziri Nape. Tuliwahi kupelekea waogeleaji kwenye olimpiki wakati mabwawa ya kuogelea karibu yote hayana hadhi ya olimpiki. Waziri Nape anayo kazi ya kujenga hoja ili fedha inayotengwa kwa ajili ya michezo iongezwe. Mahitaji ya michezo ni mengi, lakini kwa sababu wale wenye dhamana ya michezo wanashindwa kujenga hoja, michezo inabaki kuwa duni kila mwaka.
Nimefurahi kusikia kuwa Rais Magufuli kafurahishwa na mafanikio ya Mbwana Samatta, lakini serikali kwa ujumla wake ijipange zaidi kwenye michezo. Kuna fursa nyingi za ajira kupitia michezo, lakini inahitajika elimu ya michezo kuweza kuzibaini na kuzifanyia kazi. Serikali ya awamu ya tano iwekeze nguvu nyingi katika kuijenga michezo. Serikali ijipange ili taaluma iheshimike miongoni mwa jamii ya wanamichezo. Natumaini ujumbe utawafikia walengwa.