Rais Kabila aendelee kuweko DR-Congo

Rais Kabila aendelee kuweko DR-Congo

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,225
Reaction score
17,536
DRC bado hakuko shwari, nchi iko kwenye vita. Rais Kabila anaelekea kufanikiwa kuwafyeka wavamizi wa nchi ambao kimsingi ni majirani zake wanaopora ardhi na mali za Congo. Maandamano na kelele unazozisikia sasa kuhusu kabila ajiuzulu ni njia mbadala za magaidi kutaka kumuondosha Kabila pale ili uvamizi na uporaji chini ya Rais mpya ambae watampandikiza wao uwe rahisi.

Kanisa Katoliki kupitia Congo limeshindwa kufahamu kuwa DRC iko vitani na chini ya Rais Kabila DRC iko shwari zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma? Nia yao hasa ya kutaka kumtoa Kabila ni nini?

Huu sio wakati mwafaka kwa Rais Kabila kuendesha uchaguzi hadi hapo atakapoiweka salama mipika ya nchi zake dhidi ya mabeberu. Nchi jirani pengine wana hasira na Kabila na Tanzania kuwazuia kupora mali za DRC kama walivyozoea. Kanisa Katoliki lazima lituhakikishie namna mipaka ya DRC itakavyokuwa salama zaidi kama Kabila ataondoka madarakani, vinginevyo kanisa linawezekana kuwa sehemu kubwa ya tatizo la DRC.

Kwasasa Rais Kabila amtwange kila anaekatiza mbele yake kumpinga bila kujali nani ni nani maana nchi iko kwenye vita na vita haina macho, maadui wanaweza kushika misalaba na kujichomeka kwenye maandamano ya Wakatoliki.
 
Kwa Beberu la Kiuchumi kama mimi ningependa Kabila aendelee si kwa sababu eti nampenda sana au ndie pekee anayeweza kuleta amani DRC bali Joseph Kabila ni loyal kwa Tanzania na pia ni partner mzuri.

Nisingependa kuona anaingia Rais nisiye na uhakika nae ambae kuingia na kuingia tu anaanza kuzi-favor bandari za nchi jirani na kuiacha ya Dar es salaam!

So, Kabila Baba, nakuombea kwa Mungu utawale hata miaka 100 so long as unaendelea kuwa loyal kwa Tanzania! Hako kanchi kenu mambo ya demokrasia ni anasa isiyo na sababu yoyote!

Mimi sio Benjamin Mkapa aliyewahi kuiwekea vikwazo Burundi wakati anafahamu fika Burundi wanatumia bandari ya Dar es salaam!!
 
eti eeh leo ndo nimeanza kuwaza upande wa pili wa vitz za hili linchi likubwa lenye utajiri lukuki huwa nawaza sana mbona hawatulii
 
Kwa Beberu la Kiuchumi kama mimi ningependa Kabila aendelee si kwa sababu eti nampenda sana au ndie pekee anayeweza kuleta amani DRC bali Joseph Kabila ni loyal kwa Tanzania na pia ni partner mzuri.

Nisingependa kuona anaingia Rais nisiye na uhakika nae ambae kuingia na kuingia tu anaanza kuzi-favor bandari za nchi jirani na kuiacha ya Dar es salaam!

So, Kabila Baba, nakuombea kwa Mungu utawale hata miaka 100 so long as unaendelea kuwa loyal kwa Tanzania! Hako kanchi kenu mambo ya demokrasia ni anasa isiyo na sababu yoyote!

Mimi sio Benjamin Mkapa aliyewahi kuiwekea vikwazo Burundi wakati anafahamu fika Burundi wanatumia bandari ya Dar es salaam!!
Nadhani Tanzania ya sasa sio ile ya zamani ya umajumuni bila kujali maslahi yake. Tanzania tutakuwa wajinga wa kutupwa kama tutamuacha Kabila atiwe kishindo na kuondoka zake, itakuwa kama tumewasaliti watanzania wenzetu waliopoteza maisha yao DRC wakitafuta amani ya ndugu zao Congo. Tanzania itaendelea kubeba mzigo wa wakimbizi kutoka DRC kama Congo hakuko shwari.
 
Mabeberu Wa Nchi Za Magharibi Siku Wakiamua Amani Irejee Congo Hata Kesho Tu Panakuwa Shwari Rejea Angola Ya Savimbi Walipovuna Wakachoka Wakaona Sasa Kuwe Na Amani Mpaka Leo Kagame M7 Hawa Ni Vibaraka Wa Magharibi Na Ndiyo Maana Hawakomewi Siku Wakizingua Ni Kugeuziwa Kibao So Amani Ya Congo Iko Mikononi Mwa Mzungu Usa Ufaransa Ubelgiji Russia Germany Hawa Ndiyo Wameichafua Nchi Wavune Mali Kabila Naye Ni Kibaraka Tu
 
DRC bado hakuko shwari, nchi iko kwenye vita. Rais Kabila anaelekea kufanikiwa kuwafyeka wavamizi wa nchi ambao kimsingi ni majirani zake wanaopora ardhi na mali za Congo. Maandamano na kelele unazozisikia sasa kuhusu kabila ajiuzulu ni njia mbadala za magaidi kutaka kumuondosha Kabila pale ili uvamizi na uporaji chini ya Rais mpya ambae watampandikiza wao uwe rahisi.

Kanisa Katoliki kupitia Congo limeshindwa kufahamu kuwa DRC iko vitani na chini ya Rais Kabila DRC iko shwari zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma? Nia yao hasa ya kutaka kumtoa Kabila ni nini?

Huu sio wakati mwafaka kwa Rais Kabila kuendesha uchaguzi hadi hapo atakapoiweka salama mipika ya nchi zake dhidi ya mabeberu. Nchi jirani pengine wana hasira na Kabila na Tanzania kuwazuia kupora mali za DRC kama walivyozoea. Kanisa Katoliki lazima lituhakikishie namna mipaka ya DRC itakavyokuwa salama zaidi kama Kabila ataondoka madarakani, vinginevyo kanisa linawezekana kuwa sehemu kubwa ya tatizo la DRC.

Kwasasa Rais Kabila amtwange kila anaekatiza mbele yake kumpinga bila kujali nani ni nani maana nchi iko kwenye vita na vita haina macho, maadui wanaweza kushika misalaba na kujichomeka kwenye maandamano ya Wakatoliki.
Unamaanisha bila kabila hakuna congo?
 
Mabeberu Wa Nchi Za Magharibi Siku Wakiamua Amani Irejee Congo Hata Kesho Tu Panakuwa Shwari Rejea Angola Ya Savimbi Walipovuna Wakachoka Wakaona Sasa Kuwe Na Amani Mpaka Leo Kagame M7 Hawa Ni Vibaraka Wa Magharibi Na Ndiyo Maana Hawakomewi Siku Wakizingua Ni Kugeuziwa Kibao So Amani Ya Congo Iko Mikononi Mwa Mzungu Usa Ufaransa Ubelgiji Russia Germany Hawa Ndiyo Wameichafua Nchi Wavune Mali Kabila Naye Ni Kibaraka Tu
Jifunze kuzifahamu dalili na viongozi vibaraka Afrika. Dalili muhimu kupita zote ni kukaa muda mrefu madarakani, kubadilisha katiba ya nchi yake kwa manufaa yake, na kuvunja haki za raia wake bila kulaumiwa na mataifa makubwa ya kibeberu. Kabila anakumbana na shutuma nyingi, wamissionari hawamtaki waziwazi na mabeberu yanapaza sauti Kabila aondoke. Hii ni dalili tosha kuwa Kabila sasa hana maslahi kwao wanamtafuta "Mobutu mwingine" au nchi ikose uongozi unaoeleweka kama vile ilivyo Libya na Iraq baada ya kuuondoa uongozi makini wa Gadaffi na Sadam.
 
Back
Top Bottom