Rais John Pombe Magufuli tunaomba msamaha

Rais John Pombe Magufuli tunaomba msamaha

Visingizio muhimu kutoka nyumbani Bukoba:
Vita vya Kagera
Ukimwi
Migomba na mibuni ilishambuliwa na "mnyauko"
Tetemeko
JPM katutenga kisa tulichagua UKAWA.

Ukweli:
Nyumba zilizobomolewa na tetemeko 97% zilikuwa za urithi, angalia zilivyozeeka...yaani wanaojiita waathirika wengi walikuwa wanaishi kwa babu zao.

Hakuna familia hata moja iliyopoteza akiba ya chakula... hakuna hata media moja iliyoripoti uharibifu wa chakula. Mhaya Hana utamaduni wa kuweka akiba ya chakula iwe mahindi au maharage.

Mh. JPM umefanya mengi Kama rais kwa ajili ya ndugu zetu hawa ila tatizo lao sio tetemeko, Uvivu, uvivu, uvivu (Obunafu endya' mazi, pamoja na kupenda umaarufu wa kijinga.
Wewe ni mkurya au mjaluo, ,mbona ni kama matani kwenye msiba wa kihaya?
 
Poleni sana Mkuu. Wiki ya tatu sasa bado hataki kutia mguu Kagera bila ya kuwepo sababu zozote zile za msingi. Itafika wakati wa kuja kuomba kura msihudhurie hadhara hizo.

Mh rais sisi marafiki zako wahari yachini huku bukoba tumelazimika kukuomba msamaa make niwazi kabisa una kisasi na sisi ndani moyo wako.

Tunaamini kosa letu kubwa kwako nikitendo cha sisi kuto mpigia kura ndg khamisi suedi kagasheki ambae alikua mgombea umbunge kupita ccm jibo la bukoba mjini pamoja na madiwani wa ccm nao hatukuwapigia kura hali ilio pelekea jimbo la bukoba mjini kuongozwa na upinzani, mh raisi sisi wana bukoba hasa wa hari yachini tunaamini hilo ndilo kusa letu kubwa lililo pelekea wewe kututelekeza kiasi hiki, Mara kadhaa tumekuwa tukishuhudia na kusikia misaada ikitolewa ili tusaidie sisi tulo adhiriwa na tetemeko lakini tumeshudia misaada hiyo ikitupitia pembeni na kwenda kwa matajili wano jiweza huku nyumba za makada wa ccm zikipewa kipaumbele cha kwanza na sisi raia wakawaidi tuki wekwa pembeni.

Mh raisi tulijawa na Matumaini tulipo sikia kwenye vyomba vya habari kuwa umearisha safari ya kwenda kuhudhuri sherehe za kuapishwa kwa raisi frani hivi ambae jina lake limetutoka kidogo kwa kusema unashugulikia tetemeko, tukadhani ungekuja kujionea hali na maisha tunayo ishi lakini hukutokea, tukaendelea kujipa moyo na tuka frai zadi tuliposikia tena kuwa umeairisha safari ya kwenda ulaya kuhudhuria mkutano wa umoja wa mataifa na ukatoa sababu zile zile za kushug'ulikia tetemeko bukoba lakini napo hukuonekana mpaka Leo.

Mh Mara kadhaa tumekuwa tukisia kuwa wewe huna mausiano mazuri na viongozi wa upinzani na tulijiridhisha tulipo kusikia huko zanzibar ukisema kuwa kwenye selikali yako hukuweka wapinzani na hawato kaa waingie kamwe, ivyo tunaamini wewe kutokuja bukoba na kujionea maisha tunayo ishi ni muendelezo wa chuki dhi ya upinzani ambapo chuki hiyo inatuadhiri sisi raia wa kawaida na kama hiyo haitoshi juzu tumeumia zaidi wakati ukizindua ndege pale ulipo sema unampango wa kununua mandege mengine mkubwa mawili na ukasema fedha zipo zimesha tengwa, kiukweli tumeumia miyoni mwetu kuaona tuna teseka na kulala nje lakini selikali yetu ina ela za kununua ndege, huku tukiambulia misaada ya maneno tu.

Mh raisi baada ya kukuomba msamaa tunauomba uje ujionee mwenyewe maisha tunayo ishi sisi raia wako ikiwezekana kwaba babu nchi yetu haiko vitani basi tuletee wanajeshi na wafungwa waje watujengee nyumba zetu, MUNGU AKUBARIKI MTUKUFU RAISI WETU.
 
Lowasa ni tajiri wa kuondoa umasikini ndani ya siku 30, mwambieni awasaidie, hasa ikizingatiwa kuwa mlideki barabara kwelikweli
 
Ukiwa na watoto watatu, mmoja anaPhD, Mwinine Diploma na darasa la saba, baba au mzazi mwenye hekima atamwangalia kwa jicho la ziada huyu wa darasa la saba. vivyo vyo hivyo kiongozi mwenye hekima ataangalia masikini kuliko wenye uwezo


Yesu alimalizia kwa kusema " mwenye sikio na asikie"
 
Sherie nasalakimosooo.. Ngo ya mbongoo... mwasimobimbaa nabibaliyeleeee.... Ferre gola ni fundi sana.
 
Lowasa ni tajiri wa kuondoa umasikini ndani ya siku 30, mwambieni awasaidie, hasa ikizingatiwa kuwa mlideki barabara kwelikweli
Siku zote kuni ya akiba huicheka kuni inayoteketea motoni.
 
Mhh inaumiza post yako kwa mwenye akili na uwezo wa kufikili na si kufikiliwa amewasilisha mengi polen mola yu pamoja nanyi kwani imeandikwa alaaniwe amtegemeaye mwanadamu
Andika kiswahili sanifu tafadhali....kunawatu wanamtegemea Rais Nao vipi?walaaniwe?
Kumsemea Mkuu anakisasi na watuflani ni uchochezi mbaya sana,jiandae!
 
Sasa hao wenyekiti wa halmashali na mbunge wenu anakua wapi had I msaada uende sivyo kama ulivyo kusudiwa
Wakati umese huko kwenu ndio mnaoiogoza serikali,
Sijui sasa kwann kama rawama zako zinamlenga Rais Magufuli badala ya kuwaraumu viongozi wako kwa sababu hakuna kitu kinaweza kufanyika bila kushilikishwa mwenyekiti wa halmashauri
 
Pole sana ndugu .....

Inauma sana kuona mkuu wa nchi anakuwa na visasi......

Kafanikiwa kuonyesha real image yake....
Rais wetu hana kisasi wala chuki na mtu. JPM ni rais wa watanzania wote. Na kwa tukio la maafa ya Bukoba nadhani watanzania wote ni mashuhuda jinsi alivyolichukulia uzito na hata kufikia kuwawajibisha baadhi ya viongozi. Acheni uchochezi.
 
Nawakubali sana watu wa bukoba ila hawapo kama wewe unaetaka kutuaminisha kuwa bukoba inapiga magot, kwa lipi?

Au hujui maana ya demokrasia

Bukoba sio watumwa wa fikra
 
mtukufu rais ona kwa macho yako kijana wako alivyo na machungu mpaka kaamua kuandika kiswahili kwa shida.
anaumia kuona serikali yako japo anaiita selikali haijawajali kama inavojali ndege japo yeye anayaita mandege.
anasema ulipoahirisha japo kasema ulipoarisha kuhudhuria zambia na UN alijua ungewatembelea ila ulikacha.
analalamika na kulaumu zaidi kiasi kwamba anasema matajili badala ya matajiri.
anasema mtukufu rais waone wananchi wa hari ya chini japo alipaswa aseme hali
huyu jamaa ana hasira sana.
mkuu pole kwa masahibu, Mungu awatidd nguvu. Msitegemee sana jipya maana mlishaambiwa serikali haikuleta tetemeko. mfanye kazi.
 
Mtoa mada umetumwa si bureee. ...nimependa ulivyopanga hoja zako....na pia nimependa ulivyomtega mkulu. Aje kagera kukuonyesha kuwa hana kisasi na hachukii kunyimwa kura na kupeaa upinzani...au asije kudhibitisha kweli ana chuki na watu wa kagera kwa kumnyima kuwa.....daaah kweli hata mie natamani urais ingekuwa miaka 2.
 
Msaada umeruka kutoka uwingereza mpaka Ikulu kwa ajili ya kuwasaidia wahanga lakini mwenye nchi bado hajatia hata mguu kwa ajili ya kwenda kuwajulia hali wahanga.
 
Kagera tatizo mna haraka sana, Mkuu atakuja tu kuwaona mbona bado mapema.. Kwani? mmesahau kuwa alihairisha safari mbili kwa ajili yenu?
 
Poleni sana Mkuu. Wiki ya tatu sasa bado hataki kutia mguu Kagera bila ya kuwepo sababu zozote zile za msingi. Itafika wakati wa kuja kuomba kura msihudhurie hadhara hizo.
Makamanda mnaanzisha mada za kutunga halafu mnakaaa kutwa nzima kuchangia. Ha ha ha.
 
Back
Top Bottom