RAIS John Magufuli: Tanzani na Afrika kwa ujumla ni tajiri na hakuna kinachoshindikana

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1572163557838.png

RAIS John Magufuli amesema Tanzani na Afrika kwa ujumla ni tajiri na hakuna kinachoshindikana isipokuwa kikubwa kinachohitajika ni matumizi mazuri ya fedha za walipa kodi. Akizungumza kwenye hafla ya mapokezi ya ndege aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali na kuikabidhi Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Magufuli alisisitiza kuwa mkakati wa kufufua shirika hilo si wa kubipu kama ilivyodhaniwa na baadhi ya watu.

Aidha Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk Inmi Pat- terson amepongeza ununuzi wa ndege unaofanywa na serikali akisema Tanzania ni nchi yenye uwezo usio na ushindani. Tujipongeze Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwamo wawakilishi na mabalozi zaidi ya 30 wa nchi mbalimbali, Rais Magufuli aliwataka Watanzania kutembea kifua mbele na kujipongeza kwa mafanikio yanayotokana na fedha zao.

“Tuna kila sababu za kujipongeza...yamezungumzwa na Kaimu Balozi wa Marekani (Patterson) sitaki kuyarudia maneno mazuri aliyozungum- za...vyombo hivi vilivyosi- mama (ndege) vimeshushwa hapa na Watanzania,” alisema Rais Magufuli. Katika salamu zake, Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Patterson alipongeza Tanzania na kusema safari za ndege za ndani na nje ya nchi zitasaidia kuongeza shughuli za kiuchu- mi, kuchochea mzunguko wa kimtaji, kuongeza uwekezaji na kuongeza watalii.

Akipigilia msumari kauli hiyo ya Balozi, Rais Magufuli alisema: “Kwa hiyo fedha zenu zinajulikana hata kule Marekani kwamba Watan- zania ni matajiri wanaweza kununua kitu kizito kama hiki. Mtembee kifua mbele... Watanzania tunaweza na Waafrika tunaweza, hakuna kinachoshindikana kikubwa kinachohitajika ni matumizi mazuri ya fedha kutoka kwa wananchi.

“Kwangu mimi najisikia raha kuwa kiongozi wa Tanzania na zaidi kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu hayo yalizungumzwa kwenye Ilani ya Uchaguzi na mimi na viongozi wenzangu ni watekelezaji.” Waliobeza Akizungumzia mkakati wa kufufua ATCL, alisema kawaida serikali ilipoanza na mpango wa kununua ndege aina ya Bombadier, baadhi ya watu walidhani inabipu na wengine walipiga kejeli za chinichini.

Aliwahakikishia Watanza- nia kuwa serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria na imejizatiti kuhakikisha shirika linafufuliwa kama ilivyo katika ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015. Alisema ndege mpya saba kati ya 11 zilizonunuliwa na serikali tayari zimewasili ambapo mbili ikiwamo iliyowasili jana yenye uwezo wa kubeba abiria 262, ni ya masafa marefu. Mbili ni za masafa ya kati aina ya Airbus 220 yenye uwezo wa kubeba watu 132 na tatu ni za masafa mafupi aina ya Bombadier Dash Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja.

Ndege nyingine nne zina- tarajiwa kuwasili nchini kwa nyakati tofauti ambapo moja ya masafa mafupi bombar- dier itawasili mwezi ujao, na nyingine ya aina hiyo itawasili Juni 2020 na nyingine mbili aina ya Airbus 220 zinatara- jiwa kuwasili kati ya Juni na Julai 2021. Kibano ATCL Rais Magufuli alitaka ATCL kuchapa kazi na kutu- mia ndege hizo kufanya bi- ashara inayozalisha. Baada ya kuhoji kiasi ambacho shirika hilo linacho tangu lianze uzalishaji, alijibiwa kuwa lina dola milioni 14 na akaahidi leo kufuatilia kwenye akaunti kubaini kama ni kweli.

Akisisitiza kufanya kazi kwa ufanisi na weledi, Rais Magufuli alitaka shirika hilo kukabili ucheleweshaji wa safari na kauli mbovu za baadhi ya maofisa. Alitaka shirika kuendelea kupanua mtandao wa safari za ndani nan je ya nchi.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwelwe alisema ununuzi wa ndege ni mawazo ya Rais Magufuli ambayo wao ni wasimamizi. Alisema watahakikisha mawazo hayo aliyoanzisha yanafikia mahali alipotarajia.

Sifa za ndege iliyopokewa Akizungumzia sifa za ndege iliyopokewa jana, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamriho alisema inabeba abiria 262 ambao kati yao, 22 ni wa daraja la biashara na 240 ni daraja la kawaida. Ina uwezo wa kusafiri kwa saa 18 namatangi yake yana uwezo wa kubeba mafuta tani 125.

Alisisitiza kuwa hadi sasa zipo ndege sita mpya zilizoka- bidhiwana yajananiyasaba. Mikataba mingine ya ndege imekamilishwa kwa ajili ya Bombadier Q4 102 ambayo moja itawasili mwishoni mwa mwezi ujao na nyingine Juni mwakani. Alisema ipo mikataba ya Airbus mbili ambazo zi- tawasili Juni na Julai, 2021.

Alisema vile vile ATCL inatarajia kutumia ndege mbili aina ya Fokker ifikapo Machi mwakani na kwamba hadi kufikia Juni 2022, shirika linatarajia kuwa na ndege 14. Nane ni za ujazo mdogo, nne ujazo wa kati na mbili za ujazo mkubwa.

Kabla ya ndege hiyo mpya iliyotua jana mchana na kupokewa na mamia ya watu katikakiwanjacha ndegecha Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, zilizokuwapo ni Airbus A220-300 iliyopokewa Januari mwaka huu. Nyingine ni Bombardier Dash8Q400tatu zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja; Boeing 787-8 Dreamliner moja yenye uwezo wa kubeba abiria 262 na Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132 kila moja.
 
Angesema tutembee VIFUA MBELE, sasa anaposema tutembee kifua mbele ina maana tutumie kifua kimoja, sasa hicho kifua kimoja tutumie cha nani?, kama.ni kifua cha kuheshimu katiba sawa
 
Chapa kazi Mh. Hakika Tanzania ilichelewa kupata mtu mwenye maono na mapenzi ya kweli kwa taifa hili.

Hakika ni muda wa kutembea kifua mbele.
 
I find this silly.

Yani madini yetu tumewapa Barrick na Ashanti wachimbe na wauze halafu chenchi ndo tupewe sisi.

Halafu hizo chenchi tunazitumia kununua ndege kutoka kwa wao wenyewe.

Wanazidi kutunyonya aisee. Halafu tutembee kifua mbele?

We should take control of our natural resources. Mikataba yote tuivunje tuchimbe wenyewe. Halafu tutembee kifua mbele tukipokea oda kubwa ya madini kutoka Marekani.
 
Back
Top Bottom