Crocodiletooth
JF-Expert Member
- Oct 28, 2012
- 20,053
- 23,499
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli,ameondoka majira ya saa nne asubuhi jijini Arusha nchini,kwenda Kampala nchini Uganda kuhudhuria kuapishwa kwa Rais mteule wa Uganda mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni,sherehe zinazotarajiwa kufanyika siku ya alhamisi tarehe 12 mwezi wa tano 2016.
Akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro,Rais Dkt John Pombe Magufuli,alisindikizwa na wakuu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na viongozi wengine wa mikoa hiyo wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa na viongozi wa dini wa mikoa hiyo.
Picha hizi ni Rais Magufuli alivyowasili na Kupokelewa Uganda.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, amewasiri Uganda katika Sherehe za kuapishwa Mteule Yoweri Museveni Hapo Kesho.
Museveni alichaguliwa na Wananchi wa Uganda katika Uchaguzi uliofanyika February 18 kwa Ushindi wa zaidi ya Asilimia 60 ya kura Zilizo pigwa. Mpinzani wake Mkubwa wa Kisiasa Kizza Besigye alipata asilimia 35 ya kula zilizopigwa, hii ni kwa mujibu wa tume ya Uganda ya Uchaguzi.