Rais, hawa wanakuumbua, wanakuaibisha. Kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya mnavuliwa nguo, mwasubiri kuchutama?

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Kwanza nianze kama kawaida ya Mtanzania yoyote tunavyo takiwa kukumbushana kuwa kunawa mikono ni mhm sana, kujipaka senitaiza, pasipo kusaau Nyungu pia ni Muhimu.

Hakika naungana na Viongozi wangu wa nchi kutii ushauri walio tupatia dhidi ya kujikinga na corona, nazingatia nawaomba na wana JF basi tuzidi kuzingatia tusikate tamaa hili nalo litapita. Kwa wakiristu, tusome KUTOKA SURA YA TATU ina majibu ya haya yote yanayojiri. HILI NALO LITAPITA.

Kabla ya kujikita kwenye uzi wa wangu wa leo, sina budi kuwashukuru Wakurugenzi wa JF kwa kutupatia nafasi ya pekee sisi tusio na kisemeo hapa tumeweza kusema na kupaza sauti zetu.

Nina kumbuka niliwahi kumsikia Mh Rais siku moja akiomba Malaika ashuke afungie mitandao hii ya kijamii kwani ilimnyima amani ya moyo wake yeye kama Rais maana tulimsema sana.

Ninamshukuru Mungu hakuweza kupokea maombi yake, kwa kumshusha malaika huyo ili afungie mitandao ikiwemo JF, hapo ndipo nilipoamini ya kuwa kumbe hata wale waitwao wateule wa Mungu vipo waombavyo na kunyimwa.

Ikiwa imebakia miezi kadhaa tuingie kwenye uchaguzi lazima tukubaliane kuwa huu ndio muda ambao Rais wetu tumwelezee ukweli ambao hama hakika ni mchungu au mtamu ili endapo atapewa ridhaa tena hasiweze rudia makosa aliyoyatenda kwa kipindi cha nyuma.

Tangu limeingia janga la corona limeingia nilifuraishwa sana jinsi ambavyo Rais alikuwa akikemea baadhi ya matendo ya baadhi ya viongozi mfano Matendo ya mkuu wetu wa mkoa wa Dsm alikuwa akiyafanya, kumkemea hadharani kulidhihirisha kabisa kua mteule yule kuna pahala alipwaya sana na pengine alistaili kutenguliwa ila wapo uliowapa nafasi za ukuu wa wilaya

Kwa historia ya nafasi hizi nchini Tanzania huwa ni nafasi za shukrani kwa wale wanaokuunga mkono ni nafasi za ajabu kabisa katika nchi. Nina sema ni nafasi za ajabu kwa sababu zifatazo:

Nitatoa mfano,

Mtu kama Julius Mtatiro alipewa ukuu wa wilaya uko Ruvuma, jana kwenye vyombo vya habari analitangazia taifa kuwa ndani ya miezi mitatu watoto zaidi ya 30 wamepewa mimba katika wilaya ambayo yeye anaiongoza.

Hivi umemteua mtu, umempa wilaya, gar zuri, ulinzi yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya bado yeye anachoweza kukifanya ni kututangazia tu na si kutwambia amekamata washutukiwa wangapi kwa kutumia kamati yake ya ulinzi na usalama aliyonayo?

Labda ili halieleweki vyema, sisi wachaguaji hatuchagui kiongozi aje kututangazia matatizo tuliyonayo sisi wanachi, tunamchagua ili tuweze shirikiana nae kutatua kero zetu tafadhali.

Hivyo hivyo, Rais hateui mkuu wa mkoa au wilaya ili akatangaze uvunjifu wa sheria unaotendwa na wanachi ili hali kiongozi huyo ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya au mkoa.

Tunatambua kuwa mpo wenye viti mlioteuliwa na mkuu wa nchi muwe wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama hamjapita hata kwenye jeshi la Akiba yaani mgambo. Isiwe tatizo mnao waongoza ni wabobevu, watumieni.

Mnao ongozwa na wateule wa Rais hasa kwenye kamati za ulinzi na usalama tafadhali jiazalini mnadhamana na viapo vya kulinda nchi hii kama alie wateua hao mabosi wenu wa muda, tunatambua changamoto zenu tafadhali pambaneni kuondoa aibu hizi.

Inapotokea Mkuu wa Wilaya anautangazia umma kuwa kuna wavunjifu wa sheria kadhaa katika eneo fulani na nyie mpo wanao zalilika ni nyie.

Msikubali kuvuliwa nguo na hao wateule pambananeni kwa kuzingatia viapo.
 
Kwanini wafute uzi si ushaponda vyeo vya wakuu wa wilaya kuwa wengine hawana akili au? na ni kweli kuna wengine ukiacha kuwa ni vilaza wengine ni wahuni na cheni zao!! kuna Rais flani wa Banana Rep atafuta cheo hiki kwa bandiko lako huwezi jua!!

Na mengineyo je hujaona umesema kitu kikubwa sana kuwa JF ni jukwaa la kutukuzwa na kulindwa milele? manake watu wakikandamizwa wasiseme madukuduku wanakufa haraka kwa kihoro!! Ahsante sana Maxence.

Huoni pia umeamsha popo hasa kwa wazazi na serikali kuwa mimba za ‘Corona girls’ ( watoto wa kike waliofunga shule na kujiunga na masharobaro mitaani ili kujiepusha na Covid19) zitakuwa za kutosha!!na shule zikifunguliwa tena mabinti watarudi skuli nusu na nusu ingine ya mabinti watakuwa Clinics wakipimisha uzito vitoto vyao!! anaenibishia na hili la mimba aje na mkakati kuwaokoa wanetu!! wapi Waziri wa Elimu??!!amejipangaje? au yuko bize anajifukiza manake wiki ya vyungu hii!!!

Mbona unaogopa tena kuna mtu kakutisha nini?
 
Kwanza nianze kama kawaida ya Mtanzania yoyote tunavyo takiwa kukumbushana kuwa kunawa mikono ni mhm sana, kujipaka senitaiza, pasipo kusaau Nyungu pia ni Muhimu.

Hakika naungana na Viongozi wangu wa nchi kutii ushauri walio tupatia dhidi ya kujikinga na corona, nazingatia nawaomba na wana JF basi tuzidi kuzingatia tusikate tamaa hili nalo litapita. Kwa wakiristu, tusome KUTOKA SURA YA TATU ina majibu ya haya yote yanayojiri. HILI NALO LITAPITA.

Kabla ya kujikita kwenye uzi wa wangu wa leo, sina budi kuwashukuru Wakurugenzi wa JF kwa kutupatia nafasi ya pekee sisi tusio na kisemeo hapa tumeweza kusema na kupaza sauti zetu.

Nina kumbuka niliwahi kumsikia Mh Rais siku moja akiomba Malaika ashuke afungie mitandao hii ya kijamii kwani ilimnyima amani ya moyo wake yeye kama Rais maana tulimsema sana.

Ninamshukuru Mungu hakuweza kupokea maombi yake, kwa kumshusha malaika huyo ili afungie mitandao ikiwemo JF, hapo ndipo nilipoamini ya kuwa kumbe hata wale waitwao wateule wa Mungu vipo waombavyo na kunyimwa.

Ikiwa imebakia miezi kadhaa tuingie kwenye uchaguzi lazima tukubaliane kuwa huu ndio muda ambao Rais wetu tumwelezee ukweli ambao hama hakika ni mchungu au mtamu ili endapo atapewa ridhaa tena hasiweze rudia makosa aliyoyatenda kwa kipindi cha nyuma.

Tangu limeingia janga la corona limeingia nilifuraishwa sana jinsi ambavyo Rais alikuwa akikemea baadhi ya matendo ya baadhi ya viongozi mfano Matendo ya mkuu wetu wa mkoa wa Dsm alikuwa akiyafanya, kumkemea hadharani kulidhihirisha kabisa kua mteule yule kuna pahala alipwaya sana na pengine alistaili kutenguliwa ila wapo uliowapa nafasi za ukuu wa wilaya

Kwa historia ya nafasi hizi nchini Tanzania huwa ni nafasi za shukrani kwa wale wanaokuunga mkono ni nafasi za ajabu kabisa katika nchi. Nina sema ni nafasi za ajabu kwa sababu zifatazo:

Nitatoa mfano,

Mtu kama Julius Mtatiro alipewa ukuu wa wilaya uko Ruvuma, jana kwenye vyombo vya habari analitangazia taifa kuwa ndani ya miezi mitatu watoto zaidi ya 30 wamepewa mimba katika wilaya ambayo yeye anaiongoza.

Hivi umemteua mtu, umempa wilaya, gar zuri, ulinzi yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya bado yeye anachoweza kukifanya ni kututangazia tu na si kutwambia amekamata washutukiwa wangapi kwa kutumia kamati yake ya ulinzi na usalama aliyonayo?

Labda ili halieleweki vyema, sisi wachaguaji hatuchagui kiongozi aje kututangazia matatizo tuliyonayo sisi wanachi, tunamchagua ili tuweze shirikiana nae kutatua kero zetu tafadhali.

Hivyo hivyo, Rais hateui mkuu wa mkoa au wilaya ili akatangaze uvunjifu wa sheria unaotendwa na wanachi ili hali kiongozi huyo ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya au mkoa.

Tunatambua kuwa mpo wenye viti mlioteuliwa na mkuu wa nchi muwe wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama hamjapita hata kwenye jeshi la Akiba yaani mgambo. Isiwe tatizo mnao waongoza ni wabobevu, watumieni.

Mnao ongozwa na wateule wa Rais hasa kwenye kamati za ulinzi na usalama tafadhali jiazalini mnadhamana na viapo vya kulinda nchi hii kama alie wateua hao mabosi wenu wa muda, tunatambua changamoto zenu tafadhali pambaneni kuondoa aibu hizi.

Inapotokea Mkuu wa Wilaya anautangazia umma kuwa kuna wavunjifu wa sheria kadhaa katika eneo fulani na nyie mpo wanao zalilika ni nyie.

Msikubali kuvuliwa nguo na hao wateule pambananeni kwa kuzingatia viapo.
Bla bla tupu..
 
Back
Top Bottom