Its Tesha
Senior Member
- Oct 6, 2025
- 168
- 604
Shirikisho la vyama vya wachimbaji wa madini nchini Tanzamia (FEMATA), lenye wanachama takribani Milioni sita, limeahidi kura zote kwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakishukuru kwa maboresho na uwezeshaji mkubwa wa sekta ya madini pamoja na wachimbaji wadogo.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Kahama kwenye Viwanja vya Magufuli Mkoani Shinyanga leo Jumamosi Oktoba 11, 2025, waliohudhuria kampeni za Dkt. Samia, Rais wa Shirikisho hilo Bw. John Bina amesema Serikali ya Rais Samia imefanikiwa kutengeneza mabilionea wengi wanaotokana na madini katika kipindi kifupi cha miaka yake minne madarakani, akisema kwa dunia nzima, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zenye kumthamini mchimbaji wa madini.
Bina Akimtaja Dkt. Samia kama chaguo sahihi la Watanzania katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, amezungumzia pia kile alichokiita chokochoko za mtandaoni dhidi ya Dkt. Samia, akiwataka watu hao ikiwa wameshindwa siasa wajielekeze kwao ili kufundishwa namna ya kutafuta fedha kupitia uchimbaji wa madini.
"Wachimbaji pia wamenituma, juzi wameona kwenye mitandao kuna watu wanakuletea chokochoko. Kuna wachimbaji milioni sita hapa wameniambia hao watu kama hawana kazi, wameshindwa siasa waje tuwape kazi wachimbe wajue namna ya kutafuta hela badala ya kumsumbua Rais anayefanya kazi kubwa kumsimamia Mtanzania maskini." Amesisitiza Rais huyo wa FEMATA.