Rais Dr. John Pombe Magufuli na mwendelezo wa kutokuhudhuria vikao vya Kimataifa nje ya nchi

Medicci

JF-Expert Member
Dec 26, 2016
553
915
Rais Magufuli amekosa kikao kingine cha United Nation General Assembly (UNGA) kinachofanyika New York kuanzia Leo tarehe 18 Sept mpaka tarehe 20.

Na katika kikao hicho Rais Magufuli anawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Dr. Augustine Mahiga na kati ya hoja nyingi za Msingi zitakazo ongelewa moja inahusu kuchunguzwa kwa nchi chache za kiafrika moja wapo ikiwa Tanzania for violation of sanctions imposed on Korea Kaskazini.

Vikao vingine alivyokosa ni pamoja na UNGA kilichofanyika Nov 2015, SADC Meeting na vingine vingi. Na kwa niaba yake amekuwa akiwatuma\kuwakilishwa na Vice Pres.

Samia Suluhu, Waziri Mkuu Majaliwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje.
Swali ni Je...??

1. Kama nikubana matumizi mbona anatuma wawakilishi.

Wadau
Au kuna sababu nyingine za msingi zaidi..
 
Anaogopa mtamuita vadco dagama

Tatizo vikao vingi havina lolote la maana. Ni kula posho tu. Ukweli acha uitwe ukweli. Africa wanaoiangamiza ni viongozi wasiojari waafrika maskini wanaendeleaje. Wao ni kujipa uteule na kula bata tu.
Acha JPM akae magogoni mpaka kieleweke...hata hivyo yule mwingine bado mbona anasafiri sana. Halafu siku hizi ni mtunzi mzuri wa nahau na methali baada ya kuachia madaraka. Naye alikuwa baba haambiliki amesahau tu
 
Sasa kuna haja gani anatuma mwakilishi huko si aache
 
Kwani kuna ubaya akitumwa mwakilishi???

Wewe umeposa mke, umeshakubaliwa kuchukua mke, si inabidi uende mwenyewe. Kila siku utatuma mshenga? Halafu kuna mambo ambayo yanahitaji maamuzi ya rais personal na sio makamu, PM au foreign minister. Kumbuka nchi yetu sasa hivi haina picha nzuri nje ya nchi japo wazalendo uchwara hawataki kusikia ukweli huu. Hivyo kwa sasa inatakiwa aende yeye mwenyewe akakabiliane na baadhi ya maamuzi face to face.
 
Tatizo vikao vingi havina lolote la maana. Ni kula posho tu. Ukweli acha uitwe ukweli. Africa wanaoiangamiza ni viongozi wasiojari waafrika maskini wanaendeleaje. Wao ni kujipa uteule na kula bata tu.
Acha JPM akae magogoni mpaka kieleweke...hata hivyo yule mwingine bado mbona anasafiri sana. Halafu siku hizi ni mtunzi mzuri wa nahau na methali baada ya kuachia madaraka. Naye alikuwa baba haambiliki amesahau tu

Ni kweli hata mimi nakubaliana hivyo vikao havina lolote, je ni kwanini anatuma mwakilishi kwa vikao visivyo na tija?
 
Back
Top Bottom