Rais Dkt. Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu na Jaji mkuu Ikulu

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo na Rais Dkt. Magufuli.PICHA NA IKULU



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman Ikulu jijini Dar es Salaam.
 
Tatizo lenu hamtaki kuukubali ukweli wa hali halisi. Mtu mpaka anafikia kutamka hadharani kwamba anajuta kuchukua form ya kugombea Urais. Huwezi kuiongoza Tanzania ya 2016 kwa sera za kukurupuka na udikteta lazima ajutie uamuzi wake wa kuchukua form.

UKIWA KWA UKAWA!
 
Leo nilisikia bungeni kuwa mheshimiwa waziri yupo ziarani nje ya nchi au mwenyekiti wa bunge alitudanganya?

Hili ndilo tatizo la kukuombea au/na kufikiria mabaya tu...PM alikuwa Dodoma, sasa kuna ubaya gani wakati akijiandaa na safari siku hiyo kwa muda fulani pengine usiozidi saa moja au mbili akafanya mazungumzo na boss wake kabla ya safari kwa kuteta kuhusu hali ya nchi na pia kwa safari hiyo anayokwenda?
 
Tatizo lenu hamtaki kuukubali ukweli wa hali halisi. Mtu mpaka anafikia kutamka hadharani kwamba anajuta kuchukua form ya kugombea Urais. Huwezi kuiongoza Tanzania ya 2016 kwa sera za kukurupuka na udikteta lazima ajutie uamuzi wako wa kuchukua form.

Kwa hiyo wewe ndugu yetu unasemaje kuhusu ufumbuzi wake kwa unachokiamini wewe?
 
Mtu katamka hadharani kwamba anajuta kuchukua form, huhitaji kuwa nabii ili kuelewa kwamba kazi ya Urais anaijutia tena hata kabla ya mwaka ameanza kulalama hadharani. Kipi kinachokushindwa kuelewa hapa?

watu kujifanya manabiii
 
Mtu katamka hadharani kwamba anajuta kuchukua form, huhitaji kuwa nabii ili kuelewa kwamba kazi ya Urais anaijutia tena hata kabla ya mwaka ameanza kulalama hadharani. Kipi kinachokushindwa kuelewa hapa?
kinachonishinda kuelewa ni jinsi wewe unavosema eti nchi itamshinda kwa lipi??kwani muelekeo wake sasa hivi upoje na unataka abadili mwelekeo uweje?
 
Back
Top Bottom