Rais Dkt. Magufuli ahudhuria ibada ya Christmas mjini Singida, atoa Siri ya Ushindi wake wa 2015

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Mheshimiwa Rais yuko Mjini Singida kuhudhuria ibada ya CHRISTMASS.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.
Hapa wakiwa katika sala.

Rais Magufuli na mkewe wakisilkiliza neno

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya kushiriki Misa ya Krismasi katika kanisa hilo mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Baba Askofu wa Jimbo la Singida Askofu Edward Mapunda akimuombea na kumbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Ibada ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakisalimiana na waumini wa Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida mara baada ya ibada ya Krismasi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakipunga mkono wakati wakitoka kwenye Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida.


Rais JPM ametoboa siri ya ushindi wake kuingia Ikulu mwaka 2015 wakti akiwa kwenye sherehe za Krismasi mjini Singida! Rozari hiyo alipewa na sista wa Kikatoliki ambaye hamkumbuki!

Je, hii kauli ya Rais ina ukweli wowote? Kwamba Rozali ambayo ni sawa na tasbihi ya Kiislamu ndiyo ilimpa kweli ushindi wa kuingia Ikulu? Je, kwanini isiwe Tume ya Uchaguzi( NEC) ambayo siku na miaka yote huwabeba wagombea wa CCM?

Tujadili.



========

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli,amefichua siri ya kusali Krismasi kwenye kanisa la Parokia ya Moyo wa Yesu, mjini Singida mwaka huu.

Ametaja siri hiyo kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, aliwahi kusali kwenye kanisa hilo na wakati akitoka, alikutana na sista mmoja (hamkumbuki jina) ambaye alimzawadia rozali, na kumwahidi kuwa itamsadia kushinda uchaguzi huo.

Rais Magufuli ametoa siri hiyo jana wakati akizungumza kwenye sherehe ya Krismasi iliyofanyika kwenye kanisa la Porokia ya Moyo wa Yesu, na kuhudhuriwa pia na mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli.

Akifafanua, alisema kuwa rozali hiyo amezunguka nayo kwenye kampeni yake, na mwisho wa siku, alifanikiwa kupata kura za kutosha na hivyo kuwa mshindi.

“Hiyo ndio sababu kubwa au siri ya mimi kufika mjini Singida, na kuungana na wakazi wa mkoa wa Singida na Watanzania kwa ujumla, kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu kristo,” alisema na kusababisha mamia ya waumini kushangilia kwa nguvu.

Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania wote kutumia sikukuu hii ya Krismasi kuimarisha upendo, kuvumiliana na wala wasibaguane ,na kwa njia hiyo,Tanzania itaendelea kupaa kimaendeleo.

Katika hatua nyingine, alisema kuwa Watanzania na hususani wakulima, wahakikishe wanazitumia vizuri mvua zinazonyesha kwa sasa nchini kwa kuchapa kazi ya kilimo kwa nguvu zote na kulima mazao yanayostahimili ukame.

“Ndugu zangu waumini na Watanzania kwa ujumla, acheni kulialia kuwa fedha zimepotea … fedha hazijapotea isipokuwa ninyi wenyewe hamfanyi kazi. Vitabu vyote vya madhehebu ya dini vinasisitiza wajibu wa kuchapa kazi … na vinasema asiyefanya kazi na asile,” alisisitiza.

Akiijengea nguvu hoja yake ya hapa ni kazi tu, alisema kuwa Yesu kristo amezaliwa na fundi mchapa kazi kweli kweli seremala, na hivyo tunaposherehekea Krismasi Watanzania wote wenye uwezo wa kufanya kazi, wafanye kazi huku wakijua hakuna cha bure.

Aidha, Rais Magufuli, aliwataka wakazi wa mkoa wa Singida, kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti, ili kukiwezesha kiwanda kikubwa cha kukamua mafuta ya alizeti cha Mount Meru kupata mbegu za kikudhi mahitaji ya kiwanda.

Awali askofu wa kanisa katoliki jimbo la Singida, Edward Mapunda, alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wakazi wa mkoa wa Singida, kutunza mazingira, ili yaweze kuwatunza na wao.

Alisema hivi sasa hali ni mbaya kutokana na binadamu kuongeza kasi ya kuharibu mazingira, kitendo kinachochangia madhara mengi ikiwemo uhaba wa mvua.

“Mimi nashangaa sana, watu wanaendelea kuzaa huku wakiendelea kuharibu mazingira na kutishia nchi kuwa jangwa. Tuna zaa watoto waje wateseke kutokana na uharibifu wa mazingira. Kama tunaendelea kuharibu mazingira, ni vema tuache kuzaa”, alisema Mapunda.

Chanzo: Dewjiblog

 
Merry Christmas Mheshimiwa

At Least Tumeiona Siku Hii Njema

Mungu Ibariki Tanzania


Rais ana Uhuru wa kusheherekea popote ndani ya nchi

Ni Uzalendo kusherehekea nasi hapahapa Tanzania

Kuliko angeenda Ulaya kwa gharama kubwa za walipa kodi

Kwa hili nimemuunga mkono, Hata kama angeenda Mwanza au Mtwara au popote ndani ya Nchi.

Naunga mkono maamuzi yako Mh Rais

Merry Christmas!


At least tuache siasa leo

Na tuwaunge mkono wakristo pote duniani katika siku yao tukufu.


Merry Christmas JF!


Forever JF!
 
Mheshimiwa Raisi yuko Mjini Singida kuhudhuri ibada ya CHRISTMASS.

Ikizingatiwa hana shughuli nyingine ya kitaifa/kikazi, Nilifikiri angesalia Dar angeokoa matumizi yasiyo ya lazima.!
Ingependeza angesali Christ the King Cathedral Moshi
 
Lini Raisi atafanya maadhimisho Kusini mwa Tanzania maana naona kila ziara na adhimisho ni Kaskazini tu
 
Back
Top Bottom