Rais Dkt. Hussein Mwinyi: Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kuhurumiana ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wanyonge na Wajane

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,984
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kuhurumiana ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wanyonge wakiwemo wajane, mayatima na mafakiri.

Alhaj Dk Mwinyi aliyasema hayo leo wakati alipokuwa akiwasalimia Waumini wa dini ya Kiislamu huko katika Masjid Tawba maarufu Jongeyani uliopo Malindi kwa Tausi, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi mara baada ya kumaliza Sala ya Ijumaa.

Katika salamu zake hizo, Alhaj Dk. Mwinyi alisema kwamba kila mmoja kwa nafasi yake ni vyema akaona haja ya kuyasaidia makundi hayo katika jamii ili na wao waweze kuitekeleza ibada ya funga ya Ramadhani ipasavyo.

Pia, Alhaj Dk. Mwinyi alitoa wito kwa wafanyabiashara wote kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kuhurumiana hivyo, mfanyabiashara anatakiwa kupata faida ya kiasi na sio kupata faida mara mbili kwani hilo si jambo la busara.

Kutokana na hilo, Rais Dk. Mwinyi alizitaka Taasisi za Serikali zenye kushughulika na kuhakikisha kwamba bei elekezi zinafuatwa wafanye wajibu wao kuzuia wimbi la wafanyabiashara kupandisha bei mara kadhaa katika kipindi hichi cha mwezi wa Ramadhani.

IMG-20210416-WA0020.jpg
IMG-20210416-WA0017.jpg
IMG-20210416-WA0019.jpg
IMG-20210416-WA0018.jpg
IMG-20210416-WA0021.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom