Rais Banda amtimua waziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Banda amtimua waziri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Apr 27, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Kiongozi mpya wa Malawi Joyce Banda amemtimua Waziri wake wa mashauri ya kigeni, Peter Mutharika, nduguye Rais aliyefariki akiwa afisini.

  Bw.Peter Mutharika alitazamiwa kama mrithi wa marehemu kakake katika uchaguzi wa mwaka 2014 wakati ikitazamiwa kua Rais aliyetoweka angestaafu.


  Mabadiliko haya ya baraza la mawaziri linatokea siku chache baada ya mazishi ya aliyekua Rais.
  Bibi Banda alikua ni makamu wa Rais kuanzia mwaka 2009 lakini baadaye akakosana na Rais na kujitokeza kua mkosoaji wake mkali.
  Bi Joyce Banda alilazimika kujiuzulu kutoka chama cha Democratic Progressive mwaka 2010 alipokaidi amri ya kumkubali Peter Mutharika awe mrithi wa rais.
  Kufuatia kifo cha Bw Mutharika tareh Aprili, kulikuepo na tetesi kua washirika wa waziri wa mashauri ya kigeni wangejaribu kuzuia mkondo wa katiba wa kumkabidhi madaraka Bi Banda,ambaye tangu hapo alikua ameisha unda chama chake.

  bbcswahili
   
 2. Y

  Yasser5 JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 207
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu amasaidie bib joyce banda
   
Loading...