Rais aweza kuwa mwizi?

kabindi

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
333
120
Niambieni watanzania wenzangu maana inawezekana mkawa na ushahidi wa kutosha tangu JK hajaingia madarakani na hadi anaingia madarakani! kila kona sasa ni DOWANS! hata mtoto mdogo! ikiongezewa na majeraha ya nyuma kama vile RICHMOND, EPA/KAGODA, IMPORT SUPPORT COMMODITIES, MEREMETA, IPTL, RADA, na nyingine nyingi mnazozijua, inakifanya Chama Cha Mapinduzi Kionekane kama chama cha majambazi tena wenye roho mbaya ambao wakiwaingilia watawabaka, kulawiti na kuwaua na kuchukua kila kitu! Duh! mimi nimeogopa maana sasa watu wana hasira kwelikweli! Hebu niambieni, nipeni ushahidi wa kutosha huyu raisi wetu ni sehemu ya maovu haya niliyoyataja? lakini;
1. Mbona anaonekana mtu mwema?
2. Mbona anaonekana mpole na mwenye maadili?
3. Mbona anazungumza kwa upole na sauti nyororo?
4. Mbona hana makuu, watoto wake kusoma shule za kifisadi na majumba ya kifahari?

Mhh! jamani hasingiziwi??! Lakini;
1. Mbona Hazungumzii, DOWANS?
2.Mbona aliwapa muda EPAS kurudisha pesa baada ya kuwakamata mara moja na kuwafungulia mashitaka? na muda ulipofika alikaa kimya?
3. Mbona hazungumzii KAGODA na nyinginezo?
4.Mbona hawaongozi watanzania kuwapatia majibu kwa maswali magumu?
5. Mbona anapotezea mada kwa kuingiza topic ya udini baada ya uchaguzi wakati issues zilizopo ni wizi wa kura na DOWANS, EPA na nyinginezo?

Mhh! Jamani!!
1. Huyu JK si ndiye aliye kula kiapo cha kuilinda katiba ya nchi?! naambiwa pia alishika QUARAN?! Kwani humo kwenye quaran kunapindisha mambo?


NIPENI MAJIBU! USALAMA WA NCHI UPO MASHAKANI? CCM HAITASIMAMA KAMWE KAMA HAKUNA MAJIBU YA KINACHOULIZWA!

HAIWEZEKANI RAIS AKAONGOZA MAJAMBAZI KUIBIA NCHI! NAONA KAMA ANASINGIZIWA!!??
 
sasa kama anasingiziwa we unadhani ni kwanini hao wanaomsingizia rais hawafikishwi mahakamani? Au unafikiri yeye anapenda kusingiziwa?
 
Hili li nchi lina madudu bana..we acha tu. Huyu mkulu nilimsapot sana 2005 nikitarajia makubwa kwa manufaa ya nchi na watanzania...lakini now naona hafai kuwa hata diwani...kama rais unashindwa kutoa decision ngumu kwa manufaa ya wananchi wako..hivi huyu ni rais au???? U real disappoint us JK...ka unasoma JF..hayo ndo maoni yetu wananchi na tunavyofil.
 
  • Je inajalisha kuwa ameiba nini na lini, au kivipi?
  • Kwa bahati mbaya, au la? Kw mfano, kudai Hakuzijua sheria husika.
  • Na atafukuzwa vipi kazi, kwa nchi kama ya Tanzania?
 
  • Je inajalisha kuwa ameiba nini na lini, au kivipi?
  • Kwa bahati mbaya, au la? Kw mfano, kudai Hakuzijua sheria husika.
  • Na atafukuzwa vipi kazi, kwa nchi kama ya Tanzania?

Mod msiifute hii thread ni muhimu sana, ongezeo linakuja.

ignorance of law is not an excuse

jail him
 
Mwenyeti wa mtaa hawezi kuwa mwizi kama watu halmashauri si wezi
Ma DED hawawezi kuwa wezi kama mawaziri si wezi
Waziri hawezi kuwa mwizi kama Rais si mwizi
Wizi/rushwa ya mtu wa juu inalea wizi kwa watu wa chini yake.
Ngazi ya wizi hushuka taratibu hadi ngazi chini kabisa.
 
Mwenyeti wa mtaa hawezi kuwa mwizi kama watu halmashauri si wezi
Ma DED hawawezi kuwa wezi kama mawaziri si wezi
Waziri hawezi kuwa mwizi kama Rais si mwizi
Wizi/rushwa ya mtu wa juu inalea wizi kwa watu wa chini yake.
Ngazi ya wizi hushuka taratibu hadi ngazi chini kabisa.

Mkuu hiki ndicho watanzania wengi hawakioni. Utasikia wanawalamu polisi eti wanakula rushwa, eti Kova kasema uongo! Rais wa nchi na mawaziri wanapofanya haya inakuwa kama free ticket ya wadogo kufanya.
 
Katiba inasema nini? Hiyo katiba mpya inasemaje endapo rais ni.muongo na mwizi.....pesa za escrow si za umma....chemba anasema lipeni kodi....
 
kwa katiba iliyopo hilo tusahau na hata hii katiba 'nyemelezi' ingawa wao wanaidai ni pendekezwa hakutakuwa na kifungu cha kuweza kumtia hatiani kiongozi mkuu wa nchi cha msingi hapa ni kuipinga kwa nguvu zote hii katiba yao nyemelezi waniandaa kwa ajili yao tu na vizazi vyao.
 
mwenyeti wa mtaa hawezi kuwa mwizi kama watu halmashauri si wezi
ma ded hawawezi kuwa wezi kama mawaziri si wezi
waziri hawezi kuwa mwizi kama rais si mwizi
wizi/rushwa ya mtu wa juu inalea wizi kwa watu wa chini yake.
Ngazi ya wizi hushuka taratibu hadi ngazi chini kabisa.


umenena vyema kabisa
 
  • Je inajalisha kuwa ameiba nini na lini, au kivipi?
  • Kwa bahati mbaya, au la? Kw mfano, kudai Hakuzijua sheria husika.
  • Na atafukuzwa vipi kazi, kwa nchi kama ya Tanzania?

Mod msiifute hii thread ni muhimu sana, ongezeo linakuja.

Kinachohitajika hapo ni kuwa na Katiba nzuri ambayo ndani yake vipengele vyote hivyo vimeainishwa.
Kwanza, mamlaka ya kiti cha Rais yawe bayana, na mipaka yake iwe bayana.
Pili, Rais asiwe juu ya sheria, na kuwe na chombo kilichowekwa kikatiba kufuatilia kuhusu hilo (mfano Bunge)
Tatu, Chombo kilichowekwa kikatiba (mfano Bunge ambalo wabunge wote wawe wametokana na kura za wananchi) kiwe na mamlaka ya kumwajibisha Rais anapovunja sheria za nchi.

Haya yote yalipendekezwa kwenye mchakato wa kukusanya maoni wakati wa zoezi la Tume ya 'Warioba', na kwenye rasimu iliyopelekwa kwenye Bunge la Katiba yalikuwamo. Wote tunajua yaliyojiri kwenye Bunge hilo la Katiba na hatimaye maoni ya wananchi yakatupiliwa mbali na ccm, ambao hawataki kuona Rais anawajibishwa!

Kwa kifupi, tunachohitaji sasa ni Katiba mpya!
 
  • Je inajalisha kuwa ameiba nini na lini, au kivipi?
  • Kwa bahati mbaya, au la? Kw mfano, kudai Hakuzijua sheria husika.
  • Na atafukuzwa vipi kazi, kwa nchi kama ya Tanzania?

Mod msiifute hii thread ni muhimu sana, ongezeo linakuja.

Rais mwizi,
Mke mwizi
Mtoto mwizi
Mjukuu mwizi (watakuwa wezi)

Waziri mkuu Mwizi,
Mawaziri wezi,
Naibu mawaziri wezi
Katibu mkuu mwizi
Naibu katibu mkuu mwizi

Maaskofu wezi.......................................

unategemea nini? Nchi nzima ni wezi labda asiye na nafasi ya kuiba!
 
Sasa hili jukwaa linakuwa la kitoto,yan mtu ana acha kunyonyesha mtoto analia anakurupuka kuposti vitu vya kijinga hata asieenda shule anavijua.havina kichwa wala miguu!!!!
 
ATL ie the president is above the law, he can steal,he can maim whenever and wherever.
 
A gangster president invariably leads a gangster nation!! Rais mwizi ataongoza taifa la wezi!!
 
Rais akichukia wizi atahakikisha Waziri mkuu anachukia wizi,
Waziri mkuu akichukukia wizi atahakikisha mawaziri wanachukia wizi,
Mawaziri wakichukia wizi watahakikisha watendaji chini ya wizara zao wanachukia wizi,
Kwa Tanzania wizi umeazia juu ndo maana waliochini hawaoni aibu kuiba kwa sababu wanajua wizi wa mabosi wao.

Tanzania kuibia Serikali siyo dhambi tena.
 
Back
Top Bottom