Rais atakaye tuletea Katiba ya Warioba ya maoni ya Wananchi nitamchagua

Mahweso

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
1,098
1,501
Haiwezekani Kiongozi tunamchagua, akipotea miaka yote tusihoji au kumwondoa na kuchagua mwingine, tunataka kuwawajibisha viongozi, hatutaki watawala, tunataka Viongozi.

Tunaka Elimu ya Uraia, haiwezekani Raia asiwe anahoji haki zake za msingi.
 
Mchakato wa Katiba ulianza na utakamilika kisheria. Wagombea hawawezi kutudanganya kuleta katiba ya Warioba. Katiba ya warioba italetwa na sisi wananchi, kwa kuikataa katiba pendekezwa kura ya maoni itakapopigwa. Tukiikataa maana yake tunarejesha utaratibu wa kisheria mchakato kurudiwa katika kufanyiwa marekebisho tunayoyahitaji.
 
Mabadiliko kwanza, ukawa kwanza, Lowassa kwanza mengine baadaye

Siku ukiwa unapanga utumbo wako panga juu ya familia yako ili hata kama ni madhara yaipate familia yako 'mwenyewe' ..nchi yetu tutapanga mambo yetu kwa akiri tulivu, bila mihemko, bila uchovu, bila ushabiki na kwa kuchukua tahadhari zote kwasababu hapa ndo kwetu na kwingine pa kwenda hatuna ..ni hatari kama kufanya upasuaji wa moyo, unahitaji utulivu mkubwa sana, nchi yetu ndo moyo wetu.
 
Mchakato wa Katiba ulianza na utakamilika kisheria. Wagombea hawawezi kutudanganya kuleta katiba ya Warioba. Katiba ya warioba italetwa na sisi wananchi, kwa kuikataa katiba pendekezwa kura ya maoni itakapopigwa. Tukiikataa maana yake tunarejesha utaratibu wa kisheria mchakato kurudiwa katika kufanyiwa marekebisho tunayoyahitaji.

Sheria yenyewe ilishakiukwa (asomaye na afahamu). Hata hivyo, sheria siyo msahafu!
 
Tutolee majibu yanayojitosheleza, 'sheria sio msahafu' kwa hiyo? Unanatuambia rais ajaye aanze na kutengeneza mswada wa kubadili sheria?
 
Huwezi kuzungumzia katiba mpya halafu suala la muungano ukaliweka pembeni.

Ili katiba mpya iweze kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadae ni lazima kwanza kuitishwe kura ya maoni kuhusu muungano. Baada ya hapo ndiyo mchakato wa katiba mpya uendelee.

Hii katiba inayopendekezwa pamoja na kule kuondolewa kipengele cha muungano kwenye hadidu za rejea za tume ya Warioba ni upungufu mkubwa ambao hauwezi kutupatia katiba mpya.
 
Siku ukiwa unapanga utumbo wako panga juu ya familia yako ili hata kama ni madhara yaipate familia yako 'mwenyewe' ..nchi yetu tutapanga mambo yetu kwa akiri tulivu, bila mihemko, bila uchovu, bila ushabiki na kwa kuchukua tahadhari zote kwasababu hapa ndo kwetu na kwingine pa kwenda hatuna ..ni hatari kama kufanya upasuaji wa moyo, unahitaji utulivu mkubwa sana, nchi yetu ndo moyo wetu.

Utumbo wako na wewe.
 
Back
Top Bottom