Rais anaitumia IKULU kufanya siasa...

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
11,410
7,493
Watanzania wenzangu tunashuhudia namna ambavyo nchi yetu inavyoendeshwa hovyo-hovyo ambapo hali za wananchi kimaisha zinazidi kuwa mbaya na kutisha.

Rais wetu, yeye yupo 'bize' katika kuimarisha chama na kukesha kutengeneza strategies za kupambana na vyama pinzani badala ya kutumia nguvu hizo hizo kuondoa ama kupunguza matatizo ya nchi.

Mfumuko wa bei, Wanasiasa kufanya biashara kwenye ofisi za umma, Wizi na usimamizi mbovu wa mali za umma, mikataba ya kipuuzi, madudu ya forodha dhidi ya watanzania ni sehemu ndogo ya matatizo makubwa yanayoikabili Tanzania.

Kupitia hotuba yake ya Mkutano mkuu wa CCM, alitamka kwamba wanaCCM wasitegemee tena kusaidiwa na polisi kupambana na CHADEMA (ndo adui yao mkubwa kuliko ufisadi), ni wazi kwamba shughuli kubwa inayofanywa na jeshi la polisi ya kusigina Katiba ya nchi kwa kunyonga haki za binadamu kwenye utekelezaji wa kazi zao ni baraka kutoka JUU (ninaposema juu ninamaanisha uongozi wa juu wa CCM naam EC!).

Pamoja na mengine mengi, hivi sasa CCM imeamua kuwatumia watumishi wa uuma (mawaziri) kwenye mikutano ya kuimarisha chama mikoani ambapo ni dhahiri kwamba serikali nzima inapiga siasa badala ya kufanya kazi za umma. Kauli za wakuu wa vyombo vya usalama Jeshi (Rtd- Shimbo) na polisi dhidi ya upinzani nchini ni ushahidi wa namna rais anavyoongoza nchi kisiasa.

Matamshi ya Waziri Wassira dhidi ya upinzani hususani aliposema kuwa CHADEMA wataisambaratisha ni mwendelezo wa mbinu za ofisi kuu ya nchi kufanya siasa badala ya kazi. Tumeshuhudia wachumia tumbo wengi wanaojitokeza na kujipendekeza kwake wanavyoinuliwa na kuwekwa nafasi za juu kiutawala kwa sababu ni wanasiasa (wachochezi) hodari.

Tulitegemea Rais awe mlezi na msimamizi mweledi wa Katiba, sheria na kanuni zilizopo lakini yeye na Vyombo vyake wanaamua kufanya siasa inapelekea imani za raia kwake kuporomoka.

Ndugu zangu, kuna hatari kubwa endapo tutaendelea kushangilia mwenendo wa rais wetu huyu wa kuamua kuweka shughuli za kisiasa ktk vipaumbele vya kwanza badala ya kuutumikia umma kama Katiba inavyomtaka.

Washauri wake mnapaswa kumsaidia kutekeleza majukumu yake ya kiofisi zaidi ya kisiasa. Chuki ya umma inavyozidi kuongezeka kwa kutojali kwake na namna anavyowakumbatia MAFISI wanaolitafuna taifa (mf. Kinana, Rostam, Jeetu Patel, EL. n.k.) itapelekea mlipuko utakaoitikisa nchi.

Kuendekeza siasa badala ya kazi za umma ni upungufu wa maono na hekima
 
Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
11,410
7,493
Kinachostua zaidi ni kwamba rais anatumia madaraka yake isivyo hekima.
Ukiangalia kesi nyingi zinazohusu masuala ya kisiasa huamuliwa mahakamani ku-influence utashi wa CCM. Mfano kesi ya mgombe binafsi ambapo serikali ilijikita kutetea utamalaki wa kisiasa na hata kufikia kukata rufaa nyingi isivyo kawaida ili kutengua hukumu ya Mahakama kuu iliyozingatia matakwa ya Katiba.

Bunge nalo limekuwa mhuri wa CCM badala ya kutekeleza majukumu yake kikatiba. Hoja zinazotolewa na wabunge wasio wa-CCM hupokelewa kwa kejeli na mashambulizi na hatimaye kukataliwa na wabunge wa CCM, hata kama hoja iwe na mashiko vipi lakini wabunge wa chama tawala wameridhia kumpendezesha mwenyekiti wa CCM badala ya kuzingatia uwepo wa bungeni. Hatujasikia rais kukemea kauli za wabunge wanaposema wanasimamia maslahi ya CCM kwanza (rf. Kingunge- alipokuwa waziri wa nchi [nafasi anayoishikilia Wassira]).

#JustSaying
 
Ame

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
4,908
3,262
Msanii EL alipokuwa mkweli (japo kwa faida binafsi) kutaka kutenganisha kiti cha urais na uenyekiti wa chama wengi wenu mlikuja juu..Sasa anagalieni faida ya ubinafsi....Rais akiwa ndiyo mwenyeketi atatenganishaje utendaji wake? Its practically impossible so acheni malalamishi ya bila sababu....Mambo objective yanapotolewa na watu hata kama ni selfish hatuamui kupinga tu bali tunatafuta jinsi ya kuondoa selfishness ya mtoa mada na kubakia na objectivity yake...

EL is right kama kweli was the one behind kutenganisha siasa na utumishi wa umma; kwani aliona kisiasa hatapata fair deal katika kushinda mbio zake kama mtu huyo huyo ni yes and amen (Mkuu wa siasa na amiri jeshi mkuu) wa kila kitu hapa Tanzania...Inamaana yule anayemtaka yeye ndiye atakayeshinda kwani akishindwa kiasiasa atatumia kofia ya serikali na nguvu za dola kum-dhibiti is that fair? Hata kama hatumpendi lakini si haki yake kama raia wa Tanzania? I myself simuungi mkono kwa wazi na hata sirini lakini when it comes to somebody's right my hands are always off! Na tutashindana katika ground sawa na hapo tukimshinda basi hata ushindi wetu unatupa confidence wa kutenda kwa usawa maana hakukuwa na biases....
 
Last edited by a moderator:

Ame

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
4,908
3,262
Kinachostua zaidi ni kwamba rais anatumia madaraka yake isivyo hekima.
Ukiangalia kesi nyingi zinazohusu masuala ya kisiasa huamuliwa mahakamani ku-influence utashi wa CCM. Mfano kesi ya mgombe binafsi ambapo serikali ilijikita kutetea utamalaki wa kisiasa na hata kufikia kukata rufaa nyingi isivyo kawaida ili kutengua hukumu ya Mahakama kuu iliyozingatia matakwa ya Katiba.

Bunge nalo limekuwa mhuri wa CCM badala ya kutekeleza majukumu yake kikatiba. Hoja zinazotolewa na wabunge wasio wa-CCM hupokelewa kwa kejeli na mashambulizi na hatimaye kukataliwa na wabunge wa CCM, hata kama hoja iwe na mashiko vipi lakini wabunge wa chama tawala wameridhia kumpendezesha mwenyekiti wa CCM badala ya kuzingatia uwepo wa bungeni. Hatujasikia rais kukemea kauli za wabunge wanaposema wanasimamia maslahi ya CCM kwanza (rf. Kingunge- alipokuwa waziri wa nchi [nafasi anayoishikilia Wassira]).

#JustSaying

CCM haijabadili mandate yake.....Bado kinashika hatam whether you people like or not...Hizi nyingine ni hadithi tu za paukwa pakawa......Mpaka CCM iondoke madarakani ndipo tutaweza kutengeneza system mpya inayojali maslahi ya wengi bila kuingiza siasa....Nchi yetu from top to a foot ni siasa...Ukitaka kuangalia vizuri angaliwa hata re-wards...Wanaopewa nafasi za uongozi ni kina nani? Wote ni makada wa vyama...Je uje kwenye mishahara nani wanapata fungu kubwa? Unaona ni wanasiasa ndiyo maana wasomi wote wameamua kujazana kwenye politics then what do you expect? Ni siasa chai, siasa lunch and siasa dinner nothing less or more...MPaka story za mitaani ni siasa tu....Uzalishaji na wazalishaji wote wana operate at negative marginal returns then mnataka miracle kwenye development? Whatever you plant that is what you reap!
 
Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
11,410
7,493
..... Its practically impossible so acheni malalamishi ya bila sababu....Mambo objective yanapotolewa na watu hata kama ni selfish hatuamui kupinga tu bali tunatafuta jinsi ya kuondoa selfishness ya mtoa mada na kubakia na objectivity yake........
Mkuu mimi sijalalamika hapo kama umesoma vyema.
nimetoa tahadhari na kupiga mbinja kwa raia wenzangu wajue kinachoendelea kwenye medani ya uongozi wa nchi yetu.

Lowasa alikuwa sahihi lakini je, dhamira ya alichosema ni kwa ajili ya usafi wa chama au kujiwekea mazingira mazuri kwa upande wake.

Inawezekana kabisa, rais akawa mwenyekiti wa chama cha siasa, lakini akatumikia umma kwa nafasi yake ya urais kuliko nafasi yake ya uenyekiti (gumu hili kweli kweli), lakini lililojema ni kuhakikisha chama hakinyooshewi vidole na kushuka hadhi kwa matendo wanayoyafanya viongozi wa serikali ambao wanaweka ukada kwenye kazi zao za umma.

Hebu iangalie hii.
CCM imerekebisha katiba yake ambapo pamoja na mengine wameweka clause kwamba Makatibu wakuu wa jumuiya za Chama watokane na wakuu wa wilaya... Hii ni pure UPUMBAVU kwa sababu inaonesha kwamba nafasi ya ukuu wa wilaya ni ya kichama zaidi ya umma. Kwa nini basi wanalipwa kutoka pesa za umma? ikitokea upinzani ukashinda na kuchukua uongozi wa nchi je watatumia hii clause? maana lazima rais atakayekuwepo atateua watu anaowaamini na wasio makada wa CCM kuwa wakuu wa wilaya...
 
mtapikanyongo

Member
Nov 27, 2012
12
3
Wewe edward lowasa ana nini mbona mumemshilkilia sana na hana mpango wowote! Unajua kwa nini tanzania mpaka leo suala la upatikanaji dawa unakuwa mgumu mahospitalini?

Sababu ni huyu edward lowasa ambae ameingia mkataba feki na taasisi ya msd ya kusambaza dawa hospitali zote za tanzania. Mkataba huo hauruhusu shirika lolote kuingiza dawa tanzania kama hazijatoka msd. Matokezeo yake wanafanya ubabaishaji tu, serikali inalipa hela cash msd matokeo yake dawa zinachelewa na ukiritimba uliokuwepo hapo haifai. Serikali imeshindwa kujitoa mpaka leo kwa kuwa ni mkataba wa miaka 50, mimi na wewe tutakufa huu mkataba unaendele kututafuna. Huo ni mkataba mmoja tu, richmond yeye ndo muhusika pamoja na memorandum of understanding pia ni yeye. Yaani huyu jamaa ana madudu hafai hata kuwa diwani.

Ni myama mkali, ila ccm kama kawaida yao wanamtaiming tu akikaa sawa wanamwaga!

Hana loloooote huyu na siku zake zinahesabika. Ndo wakati mwengine nakuoneni nyinyi munaomshabikia mmejawa na ukabila na ni watoto wa shule tu hamna kazi mukitoka shule munakuja jf kuchukua dozi ya majungu! Sasa naona bora niingie kuokoa kizazi kinachopotoka.
 
Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
11,410
7,493
rais mwanasiasa wanalalamika asifanye siasa! ikulu ameingia kwa siasa,sasa eti hawataki rais asifanye siasa ikulu!
Mkuu bado umelala. Aliingia kupitia siasa pale Ikulu kwa kazi zisizohusu siasa. Rais ameonesha udhaifu mkubwa ktk hili

Hivi mnataka rais akafanyie wapi siasa wakati hapo Ikulu kaenda kwa siasa..
Akishachaguliwa kuwa rais na kuapishwa anapaswa kujikita kuiletea maendeleo nchi na si chama. Matokeo ya kuchanganya siasa na kazi ndo haya tunayaona ya kulitumia jeshi la polisi kama chombo cha chama tawala na kuitumia dola ktk kujihakikishia utamalaki wa nchi daima dumu
 
arinaswi

Senior Member
Sep 25, 2010
183
94
wewe edward lowasa ana nini mbona mumemshilkilia sana na hana mpango wowote! Unajua kwa nini tanzania mpaka leo suala la upatikanaji dawa unakuwa mgumu mahospitalini?

Sababu ni huyu edward lowasa ambae ameingia mkataba feki na taasisi ya msd ya kusambaza dawa hospitali zote za tanzania. Mkataba huo hauruhusu shirika lolote kuingiza dawa tanzania kama hazijatoka msd. Matokezeo yake wanafanya ubabaishaji tu, serikali inalipa hela cash msd matokeo yake dawa zinachelewa na ukiritimba uliokuwepo hapo haifai. Serikali imeshindwa kujitoa mpaka leo kwa kuwa ni mkataba wa miaka 50, mimi na wewe tutakufa huu mkataba unaendele kututafuna. Huo ni mkataba mmoja tu, richmond yeye ndo muhusika pamoja na memorandum of understanding pia ni yeye. Yaani huyu jamaa ana madudu hafai hata kuwa diwani.

Ni myama mkali, ila ccm kama kawaida yao wanamtaiming tu akikaa sawa wanamwaga!

Hana loloooote huyu na siku zake zinahesabika. Ndo wakati mwengine nakuoneni nyinyi munaomshabikia mmejawa na ukabila na ni watoto wa shule tu hamna kazi mukitoka shule munakuja jf kuchukua dozi ya majungu! Sasa naona bora niingie kuokoa kizazi kinachopotoka.

aisee sikujua !!!!!! Ni kweli uyasemayo? Mbona hata watakaozaliwa watamlaani yeye na wanawe wote!!!
 
manduchu

Member
Apr 2, 2012
84
13
huwezi ingia ikulu bila siasa, na ikulu si sehemu ya kulala bali ni sehemu ya siasa kuhakikisha ilani ya chama inatekelezwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

8 Reactions
Reply
Top Bottom