Rais amchagua Abdala Mtonga kuwa Internal Auditor General

Bila kubadili katiba, tutaendelea kushuhudia uteuzi madudu! Wenzetu wakenya post kama hizi lazima mtu aombe na afanyiwe usaili.
 
Nilitaka kuchangia Kuhusu katibu Mkuu Kiongozi ajae nikamsahau jina nilipo anza kuandika tu Jamaa alikuwa RAS Morogoro majuzi kabla ya kupewa Katibu Mkuu TAMISEMI kabla ya hapo alianzia DED Masasi, anapanda vyeo kwa kasi ya ajabu sana hongera yake.
 
Ndugu zangu watanzania hivi tunachojadili hapa kweli kinaashiria "great thinking". Hatuwezi kweli kujadili sifa za mtu/kiongozi bila kugusia dini yake?

Nchi hii ni ya kila mtu na kuna mamilioni ya wananchi ambao hawaamini katika hizi dini mbili tunazopoteza muda mrefu kuzijadili.

Mimi nadhani huyu IAG anastahili kwa kuzingatia elimu na uzoefu alio nao. Tutampima kwa utendaji wake na siyo dini yake. Na ameteuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kuhusu uwezo wa raisi na utaratibu uliotumika haya hayamhusu mteuliwa bali ni mfumo wetu wa kikatiba na kisheria.
 

Mbona hawajasema alisoma lini, haswa hiyo Msc? Nafikiria uwezo wake wa kutafsiri hizo IFRS maana experience yake haionyeshi kama alikuwa ana-deal na IFRS - ama nakosea?
 
Mbona hawajasema alisoma lini, haswa hiyo Msc? Nafikiria uwezo wake wa kutafsiri hizo IFRS maana experience yake haionyeshi kama alikuwa ana-deal na IFRS - ama nakosea?


Ama huu ukumbi wakati mwengine ni kichekesho kitupu.

Hivyo ni nani alieteuliwa, ikatolewa maelezo ya anachoweza kufanya?

Na hii Mkuu, wewe itakusaidia nini?

Wacheni hizo.
 

Mbona yamesemwa sana toka vyama vingi vianzishwe? Tatizo ni mfumo wa katiba yetu unaompa madaraka Rais kuteua kila kitu. Haya ni madai ya muda mrefu ya kumpunguzi Rais madaraka. Tatizo hizo dini zenu mlizorithi( maana hakuna aliyechagua kwa hiali yake kuwa na hiyo dini, inategemeana BABU wa Babu zenu walikutana na nani) zimewapumbaza. Ni ukoloni huo pia.
 
...yangu macho tu, tusubiri utendaji wake ndio tujadili vizuri.

Tusipoipigania katiba kwa nguvu zetu zote,basi huku kote itabaki kupiga domo tu kama kijiwe.
 
mbona wakichaguliwa wakristo sisi huwa hatusemi wala hakuna anayeandika ujinga unaohusiana na dini ya mtu.? kuweni wastaarabu kwani mawaziri na makatibu wakuu wapi ni wengi kati ya waisalm na wakristo? Nachukizwa na udini halafu mtu anajiita great thinker.
 
ha ha eti mbona mkapa aliongozwa na maaskofu watu hawakusema?ni zamu sasa ya mashehe nao kujitanua ikullu
 
Congratulations,

However, I have doubts on his anticipated performance! Sehemu zote alizopita zina madudu yake na kama ni muadilifu angekuwa ashatupwa. Nina uhakika PS na wakubwa wengine walikuwa wanafanya madudu na yeye anayakagua na kupitisha. Ndiyo sababu tuko hapa leo. Anyway, hata kwenye vilaza kuna aliye na afadhali.
 
Jamani, hii nchi siyo ya Waislamu na Wakristo pekee! Sisi tusio kwenye makundi hayo tutakwenda wapi? Idadi yetu inaongezeka kila kukicha kwani Ulokole na U-Ansar Sunna unasababisha wenye vichwa kujiuliza usahihi wa hizi "conventional religions" na hatima ya ubinadamu.
 

ndugu naomba nikubaliane nawe japo tupishane kidogo. Profession ya uhasibu imegawanyika sana,kuna kazi ndogo ndogo kuanzia petty cash book management,journal entries n.k mpaka consolided financial statements. Ivi yote haviwezi kuangaliwa na mtu mmoja,hata ikiwa ivo ndo balaa maana uozo utafichuzwa na uyo uyo mmoja. Lakini kwa kuweka checks and balances inakuwa rahisi kumanage fedha. Ni kama kazi za kisheria,haiwezekani kuwe na jaji katika ngazi ya kata au mahakama ya wilaya,huko kuna mahakimu. Sasa na uhasibu uko ivo,ili kupunguza errors CAG anakuwa na wawakilishi kila ngazi ktk ofsi za serikali hasa level ya mkoa,hapa hawa ukagua hesabu za ndani kabisa,na huitwa Internal auditors, hawa wanasimamiwa na Chief Internal auditor,huyu ndo mkuu,ila hawa wote wanawajibika kwa Chief ambaye ni CAG,yan controller and Auditor General. Kwa ivo ivo kazi zaenda. Naomba kusema kuwa hamna kazi isiyogawanyika,huwa kuna Delegation of powers. Hata rais mwenyewe ana wawaziri,msikitini kuna sheikh,imam n.k kanisani kuna askofu mkuu,maaskofu na mapadre/wachungaji,n.k n.k . Nadhan nimejaribu kueleza kwa uwezo wangu. Mwisho tumwombee bwn Mtongo aweze kuwa na maamuzi. Auditing is all about drawing conclusion whether statements show a true and fair view. Ts making a decision. All the best bwn mtonga.
 
Nimeisoma hii thread kwa makini sana nilichokiona ni chuki walionayo Wakristo dhidi ya Waislam sijui kwa nini, mnasema Waislam awajasoma kazi yao kuuza kahawa, akitokea mwenye elimu akachaguliwa mnasema kachaguliwa kwa Uislam wake.
Kweli sasa naweza kuamini ni vigumu kutofautisha Chadema na Kanisa
 

we ritizi una matatizo yako,ni wapi na ni mchangia yupi kasema waislam hawakusoma?na nani kaweka neno kunywa/kahawa?? Kweli? Au ndugu unataka kutueleza reality? Aya endelezen chuki na ligi zenu!
 
Wakristo watalalama saaaana kwa sababu walisha zoea kubebwa na kujiona wo ndio wenye haki zaidi a waislam wa tanganyika.

Siku zote wanasahau kuwa nchi ni ya wote na kila mtu ana haki sawa. KUTESA KWA ZAMU , kwani nani mlitesa sana enzi za Nyerere na Mkapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…