Rais ajizuie kutamka baadhi ya mambo hadharani

Chikumba one

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
1,012
Reaction score
1,647
Kuna mambo Mheshimiwa Rais hapaswi kuyatamka hadharani hasa anapotamka mambo ambayo kiuhalisia ni tofauti na anachokisema.

Nimemsikiliza Mheshimiwa Rais, huwa namsikiliza kama Rais na Mgombea Urais. Wapinzani wake huwa nawasikiliza kama Wagombea Urais, zaidi sana Mgombea Urais wa CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu. Hawa wawili ndio wenye uchaguzi kwa Tanzania Bara na Uchaguzi wa Muungano.

Nimemsikiliza Mheshimiwa Mgombea Urais wa CCM kwa sura ya Rais wetu, kuna mambo amejaribu kumjibu Mgombea Urais hasimu wake Tundu Lissu wa CHADEMA. Bahati mbaya ni kwamba, lolote linalotamkwa na Mgombea Urais wa CCM, linasimama kama tamko la Kiongozi wa Nchi. Hii inatokana na shida iliyopo kwenye Katiba yetu. Kutokana na ukweli huo, kuna mambo Mheshimiwa Rais na Mgombea Urais wa CCM hapaswi kuyatamka hadharani. Nitafafanua.

Haifai kusema hadharani kwamba SADC walimchagua Mheshimiwa Rais kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa sababu walimuona anafaa. Ukuu wa SADC ni wa kupokezana miongoni mwa wanachama wake, haupigiwi kura, Dunia nzima inafahamu hilo, vinginevyo tuambiwe alikuwa anagombea na nani na alipata kura ngapi. Na je, kwa sasa wamemuona hafai wakamchagua mwingine na yeye kutakiwa kukabidhi Uongozi kwa huyo alochaguliwa badala yake?

Sio kila shughuli za uwakilishi wa Nchi zinaweza kufanywa na mabalozi.. Tuchukulie mfano aliousema wa SADC, kwa nini hao anaowasema walimchagua hawakutuma mabalozi waje Tanzania kumchagua? Si wana balozi zao hapa kwetu?

Baba wa Taifa hili kila mwaka alikuwa akihudhuria mikutano ya Umoja wa Mataifa, si kwa sababu hatukuwa na mabalozi, au si kwa sababu hakuwa na kazi za kuwafanyia Watanzania, bali aliheshimu mifumo iliyowekwa Kimataifa.

Duniani kuna Viongozi mahasimu, huwa hawasalimiani wala kutembeleana, lkn inapofikia kalenda ya mikutano ya Kimataifa, mahasimu hao hukutana huko bila kujali misimamo yao.

Mnapokutana Viongozi wa Nchi, huwa ni fursa muhimu sana ya kuimarisha mahusiano ya kutegemeana katika mambo mbalimbali.

Kwa sasa Mheshimiwa Rais analiongoza Taifa kuanzisha na kujenga miradi mbalimbali mikubwa inayohitaji mapesa mengi. Endapo angeshiriki mikutano hii, na kwa kusaidiana na mabalozi wetu, angeweza kukutana na Viongozi wenzake wenye uwezo kiuchumi na pengine angewaomba na kuwashawishi wamsaidie na kuwasaidia Watanzania kufanikisha malengo yao.

Baba wa Taifa alifanya hivi, Mzee Mwinyi alifanya hivyo, Mzee Mkapa pia, Mzee Kikwete nae alipitia njia hiyo. Leo Watanzania tunanufaika na matunda ya Viongozi hao. Kuanzia huduma zetu za Afya, Elimu, Miundombinu kadhaa, ni matokeo ya ushirikiano huu. Hii reli ya Kati tumejengewa, TAZARA tumejengewa.

Kwa wasiojua, hata hiyo meli tuloikarabati ya MV Victoria ni ya Waingereza.. Ilikuwa inatumiwa na Malkia alipokuwa akija kutembelea Tanganyika na Kenya. Ni kabla hata haijawa mali ya Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki. Ziwa Tanganyika kuna meli kongwe ya MV Liemba, ni ya Wajerumani. Wakati wa vita kuu ya dunia, waliizamisha meli hiyo ili isishambuliwe, na baada ya vita wakaiibua tena na ikaendelea kutumika. Meli hizo zote zipo kwetu kwa sababu Viongozi waliotangulia walikutana na wenzao na kuzungumza.

Kwenye Afya, kuanzia dawa za malaria, chanjo za watoto na wajawazito, dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi, zote tunazipata bure ama kwa gharama nafuu sababu ya Viongozi wetu wakuu kukutana na kuzungumza na wenzao wa nje.

Katika mambo ambayo Mheshimiwa Rais anapaswa kuyafanyia marekebisho endapo atachaguliwa tena, ni hilo la mahusiano na Mataifa mengine hasa Nchi marafiki zetu. Kwanza haifai kuwaita mabeberu ilihali wanatusaidia kwa kila kitu mpaka usalama wetu.

Wakati mwingine yatupasa kuwaheshimu manake wanatumia mapato ya Kodi za Raia wao kutusaidia Sisi ilihali sisi hatuna uwezo wa kuwasaidia lolote zaidi ya neno Asante.

Kama Mtanzania, namshauri ajizuie kutoa matamshi yanayokinzana na uhalisia. Hii itamsaidia yeye mwenyewe kutojibebesha mizigo ya mawazo na hata soni inapotokea amekwama na anawahitaji Viongozi wenzake wa Kimataifa kumsaidia.

Lkn zaidi itasaidia kuendelea kuijenga heshima ya Tanzania Kimataifa kama ilivyokuwa tangu enzi za Baba wa Taifa hadi wakati wa Mzee Kikwete.
 
Niwe mkweli, sijaelewa umeandika nini. Najua utasema ni wenye "akili kubwa" tu ndio wataelewa, lakini mimi nafikiri tofauti!
 
"Tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea"...TAML

Sasa unategemea mtu kama huyu Kuna analolijua kuhusu masuala ya mahusiano ya kimataifa?

Haendi hata kuhudhuria mikutano ya kimataifa kwasabb ya ushamba na ulimbukeni.
 
Usitufokee...we are on the right track ndio maana kila kitu sasa tunafanya kwa pesa zetu, mabeberu walizoea kutuibia mtu anakupa mkopo wa riba nafuu wa dola million 15 anakulazimisha unune kwake bidhaa zenye thamani ya dola million 20, na tenda zote kubwa uwape wakandarasi wao hapo bado mkopo tunalipa kama si wehu huu ni nini, ni bora tufe njaa lakini tubaki na uzalendo wetu, nyie utopolo mliowaidi nchi mabeberu mtajijua mnawalipa nini mabeberu!!! Maana uchaguzi hamshindi ng'oo hata kwa bao la mkono.
 
Usitufokee...we are on the right track ndio maana kila kitu sasa tunafanya kwa pesa zetu, mabeberu walizoea kutuibia mtu anakupa mkopo wa riba nafuu wa dola million 15 anakulazimisha unune kwake bidhaa zenye thamani ya dola million 20, na bado mkopo tunalipa kama si wehu huu ni nini, ni bora tufe njaa lakini tubaki na uzalendo wetu, nyie utopolo mliowaidi nchi mabeberu mtajijua mnawalipa nini mabeberu!!! Maana uchaguzi hamshindi ng'oo hata kwa bao la mkono.
Kila kitu sasa mnafanya kwa pesa ya naniii?
 
Yuko live muda huu kutoka Kagera. Mambo ni yale yale. Hakuna jipya. Eti watu wa Kagera wana akili sana!! Kwa hiyo watu wa Mikoa mingine hawana akili?

Kazi kweli kweli. Ngoja Lissu aendelee tu kumnyoosha ili akili ikae sawa.
Nimemsikiliza sana imetosha. Huwa nabadili channel siku hizi

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kuna mambo Mheshimiwa Rais hapaswi kuyatamka hadharani hasa anapotamka mambo ambayo kiuhalisia ni tofauti na anachokisema.

Nimemsikiliza Mheshimiwa Rais, huwa namsikiliza kama Rais na Mgombea Urais. Wapinzani wake huwa nawasikiliza kama Wagombea Urais, zaidi sana Mgombea Urais wa CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu. Hawa wawili ndio wenye uchaguzi kwa Tanzania Bara na Uchaguzi wa Muungano.

Nimemsikiliza Mheshimiwa Mgombea Urais wa CCM kwa sura ya Rais wetu, kuna mambo amejaribu kumjibu Mgombea Urais hasimu wake Tundu Lissu wa CHADEMA. Bahati mbaya ni kwamba, lolote linalotamkwa na Mgombea Urais wa CCM, linasimama kama tamko la Kiongozi wa Nchi. Hii inatokana na shida iliyopo kwenye Katiba yetu. Kutokana na ukweli huo, kuna mambo Mheshimiwa Rais na Mgombea Urais wa CCM hapaswi kuyatamka hadharani. Nitafafanua.

Haifai kusema hadharani kwamba SADC walimchagua Mheshimiwa Rais kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa sababu walimuona anafaa. Ukuu wa SADC ni wa kupokezana miongoni mwa wanachama wake, haupigiwi kura, Dunia nzima inafahamu hilo, vinginevyo tuambiwe alikuwa anagombea na nani na alipata kura ngapi. Na je, kwa sasa wamemuona hafai wakamchagua mwingine na yeye kutakiwa kukabidhi Uongozi kwa huyo alochaguliwa badala yake?

Sio kila shughuli za uwakilishi wa Nchi zinaweza kufanywa na mabalozi.. Tuchukulie mfano aliousema wa SADC, kwa nini hao anaowasema walimchagua hawakutuma mabalozi waje Tanzania kumchagua? Si wana balozi zao hapa kwetu?

Baba wa Taifa hili kila mwaka alikuwa akihudhuria mikutano ya Umoja wa Mataifa, si kwa sababu hatukuwa na mabalozi, au si kwa sababu hakuwa na kazi za kuwafanyia Watanzania, bali aliheshimu mifumo iliyowekwa Kimataifa.

Duniani kuna Viongozi mahasimu, huwa hawasalimiani wala kutembeleana, lkn inapofikia kalenda ya mikutano ya Kimataifa, mahasimu hao hukutana huko bila kujali misimamo yao.

Mnapokutana Viongozi wa Nchi, huwa ni fursa muhimu sana ya kuimarisha mahusiano ya kutegemeana katika mambo mbalimbali.

Kwa sasa Mheshimiwa Rais analiongoza Taifa kuanzisha na kujenga miradi mbalimbali mikubwa inayohitaji mapesa mengi. Endapo angeshiriki mikutano hii, na kwa kusaidiana na mabalozi wetu, angeweza kukutana na Viongozi wenzake wenye uwezo kiuchumi na pengine angewaomba na kuwashawishi wamsaidie na kuwasaidia Watanzania kufanikisha malengo yao.

Baba wa Taifa alifanya hivi, Mzee Mwinyi alifanya hivyo, Mzee Mkapa pia, Mzee Kikwete nae alipitia njia hiyo. Leo Watanzania tunanufaika na matunda ya Viongozi hao. Kuanzia huduma zetu za Afya, Elimu, Miundombinu kadhaa, ni matokeo ya ushirikiano huu. Hii reli ya Kati tumejengewa, TAZARA tumejengewa.

Kwa wasiojua, hata hiyo meli tuloikarabati ya MV Victoria ni ya Waingereza.. Ilikuwa inatumiwa na Malkia alipokuwa akija kutembelea Tanganyika na Kenya. Ni kabla hata haijawa mali ya Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki. Ziwa Tanganyika kuna meli kongwe ya MV Liemba, ni ya Wajerumani. Wakati wa vita kuu ya dunia, waliizamisha meli hiyo ili isishambuliwe, na baada ya vita wakaiibua tena na ikaendelea kutumika. Meli hizo zote zipo kwetu kwa sababu Viongozi waliotangulia walikutana na wenzao na kuzungumza.

Kwenye Afya, kuanzia dawa za malaria, chanjo za watoto na wajawazito, dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi, zote tunazipata bure ama kwa gharama nafuu sababu ya Viongozi wetu wakuu kukutana na kuzungumza na wenzao wa nje.

Katika mambo ambayo Mheshimiwa Rais anapaswa kuyafanyia marekebisho endapo atachaguliwa tena, ni hilo la mahusiano na Mataifa mengine hasa Nchi marafiki zetu. Kwanza haifai kuwaita mabeberu ilihali wanatusaidia kwa kila kitu mpaka usalama wetu.

Wakati mwingine yatupasa kuwaheshimu manake wanatumia mapato ya Kodi za Raia wao kutusaidia Sisi ilihali sisi hatuna uwezo wa kuwasaidia lolote zaidi ya neno Asante.

Kama Mtanzania, namshauri ajizuie kutoa matamshi yanayokinzana na uhalisia. Hii itamsaidia yeye mwenyewe kutojibebesha mizigo ya mawazo na hata soni inapotokea amekwama na anawahitaji Viongozi wenzake wa Kimataifa kumsaidia.

Lkn zaidi itasaidia kuendelea kuijenga heshima ya Tanzania Kimataifa kama ilivyokuwa tangu enzi za Baba wa Taifa hadi wakati wa Mzee Kikwete.
Tulia dawa iwaingie barabara
 
Back
Top Bottom