Rais ajizuie kutamka baadhi ya mambo hadharani

Kuna mambo Mheshimiwa Rais hapaswi kuyatamka hadharani hasa anapotamka mambo ambayo kiuhalisia ni tofauti na anachokisema.

Nimemsikiliza Mheshimiwa Rais, huwa namsikiliza kama Rais na Mgombea Urais. Wapinzani wake huwa nawasikiliza kama Wagombea Urais, zaidi sana Mgombea Urais wa CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu. Hawa wawili ndio wenye uchaguzi kwa Tanzania Bara na Uchaguzi wa Muungano.

Nimemsikiliza Mheshimiwa Mgombea Urais wa CCM kwa sura ya Rais wetu, kuna mambo amejaribu kumjibu Mgombea Urais hasimu wake Tundu Lissu wa CHADEMA. Bahati mbaya ni kwamba, lolote linalotamkwa na Mgombea Urais wa CCM, linasimama kama tamko la Kiongozi wa Nchi. Hii inatokana na shida iliyopo kwenye Katiba yetu. Kutokana na ukweli huo, kuna mambo Mheshimiwa Rais na Mgombea Urais wa CCM hapaswi kuyatamka hadharani. Nitafafanua.

Haifai kusema hadharani kwamba SADC walimchagua Mheshimiwa Rais kuwa Mwenyekiti wa SADC kwa sababu walimuona anafaa. Ukuu wa SADC ni wa kupokezana miongoni mwa wanachama wake, haupigiwi kura, Dunia nzima inafahamu hilo, vinginevyo tuambiwe alikuwa anagombea na nani na alipata kura ngapi. Na je, kwa sasa wamemuona hafai wakamchagua mwingine na yeye kutakiwa kukabidhi Uongozi kwa huyo alochaguliwa badala yake?

Sio kila shughuli za uwakilishi wa Nchi zinaweza kufanywa na mabalozi.. Tuchukulie mfano aliousema wa SADC, kwa nini hao anaowasema walimchagua hawakutuma mabalozi waje Tanzania kumchagua? Si wana balozi zao hapa kwetu?

Baba wa Taifa hili kila mwaka alikuwa akihudhuria mikutano ya Umoja wa Mataifa, si kwa sababu hatukuwa na mabalozi, au si kwa sababu hakuwa na kazi za kuwafanyia Watanzania, bali aliheshimu mifumo iliyowekwa Kimataifa.

Duniani kuna Viongozi mahasimu, huwa hawasalimiani wala kutembeleana, lkn inapofikia kalenda ya mikutano ya Kimataifa, mahasimu hao hukutana huko bila kujali misimamo yao.

Mnapokutana Viongozi wa Nchi, huwa ni fursa muhimu sana ya kuimarisha mahusiano ya kutegemeana katika mambo mbalimbali.

Kwa sasa Mheshimiwa Rais analiongoza Taifa kuanzisha na kujenga miradi mbalimbali mikubwa inayohitaji mapesa mengi. Endapo angeshiriki mikutano hii, na kwa kusaidiana na mabalozi wetu, angeweza kukutana na Viongozi wenzake wenye uwezo kiuchumi na pengine angewaomba na kuwashawishi wamsaidie na kuwasaidia Watanzania kufanikisha malengo yao.

Baba wa Taifa alifanya hivi, Mzee Mwinyi alifanya hivyo, Mzee Mkapa pia, Mzee Kikwete nae alipitia njia hiyo. Leo Watanzania tunanufaika na matunda ya Viongozi hao. Kuanzia huduma zetu za Afya, Elimu, Miundombinu kadhaa, ni matokeo ya ushirikiano huu. Hii reli ya Kati tumejengewa, TAZARA tumejengewa.

Kwa wasiojua, hata hiyo meli tuloikarabati ya MV Victoria ni ya Waingereza.. Ilikuwa inatumiwa na Malkia alipokuwa akija kutembelea Tanganyika na Kenya. Ni kabla hata haijawa mali ya Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki. Ziwa Tanganyika kuna meli kongwe ya MV Liemba, ni ya Wajerumani. Wakati wa vita kuu ya dunia, waliizamisha meli hiyo ili isishambuliwe, na baada ya vita wakaiibua tena na ikaendelea kutumika. Meli hizo zote zipo kwetu kwa sababu Viongozi waliotangulia walikutana na wenzao na kuzungumza.

Kwenye Afya, kuanzia dawa za malaria, chanjo za watoto na wajawazito, dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi, zote tunazipata bure ama kwa gharama nafuu sababu ya Viongozi wetu wakuu kukutana na kuzungumza na wenzao wa nje.

Katika mambo ambayo Mheshimiwa Rais anapaswa kuyafanyia marekebisho endapo atachaguliwa tena, ni hilo la mahusiano na Mataifa mengine hasa Nchi marafiki zetu. Kwanza haifai kuwaita mabeberu ilihali wanatusaidia kwa kila kitu mpaka usalama wetu.

Wakati mwingine yatupasa kuwaheshimu manake wanatumia mapato ya Kodi za Raia wao kutusaidia Sisi ilihali sisi hatuna uwezo wa kuwasaidia lolote zaidi ya neno Asante.

Kama Mtanzania, namshauri ajizuie kutoa matamshi yanayokinzana na uhalisia. Hii itamsaidia yeye mwenyewe kutojibebesha mizigo ya mawazo na hata soni inapotokea amekwama na anawahitaji Viongozi wenzake wa Kimataifa kumsaidia.

Lkn zaidi itasaidia kuendelea kuijenga heshima ya Tanzania Kimataifa kama ilivyokuwa tangu enzi za Baba wa Taifa hadi wakati wa Mzee Kikwete.
Aksante sana mkuu,very objective analysis post of the week.

Aksante sana kwa haya madini chakula cha UBONGO. 🙏🙏🙏🙏
 
Pumba zako ndio umejaza kurasa kubwa hivi?
Kwani Mv Victoria kuachwa na wakoloni ndio iwe sababu serikali isijisifu kuwa imeikarabati kuwa kama meli mpya?

Unapotosha kuwa dawa zote tunapat bure kwa hiyo hiyo bil 450 inayonunua madawa huwa unatoa wewe na baba yako?

Rais anaposema alikuwa Chairman Sadcc sio kwamba hajui namna gani chairman anapatikana bali anasema Tanzania ina mahusiano mazuri ya kidiplomasia ndio maana aliaachiwa kuwa chairman. Kama huna mahusiano mazuri majirani zako watakuachia? Jinga wewe.
Inakuuma,jamaa kaporomosha nondo, very objective.

Kiongozi hajui SADC leader criterion za kuiongoza? 🤣🤣🤣🤣🤣 mkuu aksante sana kwa MADINI uloshusha,
 
Kikwete alikuwa anasafiri mlikuwa mnakasirika,huyu hasafiri mnakasirika ! wananzengo mnaniconfuse
 
Rais wa tz ni kituko. Anashindwa kujua hata mwenyekiti wa SADC anapatikanaje kitu ambacho hata mtoto wa Darasa la sita A anakijua.
No wonder anaogopa kuhudhuria mikutano ya kimataifa na marais wenzake.
Hivi ni kweli Mh Rais hajui analolifanya ila wewe ndio unajua kwelii?!!!!
Au wewe unamtazamo ambao unataka yeye aufuate? Shauri kiungwana .. Yule ni Rais anajua nini anafanya, wapi na kwanini. Alaf hata kama humpendi, yule anaweza kua babaako, so kua na Adabu
 
Hana exposure hawezi kujenga hoja mbele ya vichwa vyenye akili,anaonea tu watanzania makondoo,pilli lugha shida anajefeel inferior kutojua lugha
Huu ndiyo ukweli wenyewe. Kichwani kweupe.
 
Hivi ni kweli Mh Rais hajui analolifanya ila wewe ndio unajua kwelii?!!!!
Au wewe unamtazamo ambao unataka yeye aufuate? Shauri kiungwana .. Yule ni Rais anajua nini anafanya, wapi na kwanini. Alaf hata kama humpendi, yule anaweza kua babaako, so kua na Adabu
Rais wako anatuona watanzania wajinga eti alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa SADEC ,uwezo wa magu uko chini ni basi tu ana bahati au anatumia ndumba
 
Ahaaaa ahaaaa, eti anatumia ndumba. I wish aende na hizo ndumba kwenye mdahalo, tuone kama zitamtoa.
 
Mama : Raisi bara bara ni mbov na nyembamba sana hivyo tunaomba ipanuliwe ili kurahisisha usafirishaji tunateseka sana.

Raisi wa ccm: mama umesema unataka kupanuliwa , kwa hiyo apa ni kupanuliwa mataka kupanuliwa .

Ccm mbele kwa mbele . Acha tuisome namba
 
Ili andiko nikwa wenye akili tu.kama unajijua akili zako ni chache wala usijisumbue kusoma maana hautaelewa.
 
"Tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea"...TAML

Sasa unategemea mtu kama huyu Kuna analolijua kuhusu masuala ya mahusiano ya kimataifa?

Haendi hata kuhudhuria mikutano ya kimataifa kwasabb ya ushamba na ulimbukeni.
Mnamuonea atatumia lugha gani kuongea na viongozi wenzake
 
Niwe mkweli, sijaelewa umeandika nini. Najua utasema ni wenye "akili kubwa" tu ndio wataelewa, lakini mimi nafikiri tofauti!

Aisee, hujaelewa??

Labda hujasoma. Na kama hujaisoma article vizuri kwa utulivu wa akili utawezaje kuelewa?
 
Kuto kwenda nje kuhudhuria mikutano sio kubana matimizi bali ni dalili za woga.

Kama ni kubana matumizi kile kiwanja cha ndege kisinge jengwa kule porini.

Back
Top Bottom