Raila Odinga ' Kuapishwa' Tarehe 30/01/2018?

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,957
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amesisitiza kuwa ataapishwa, kutwaa madaraka na kuunda baraza lake la mawaziri hata kama ikimlazimu kufanya hivyo akiwa mafichoni.

Katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, Bw. Odinga amefuta uwezekano wa kufanya mazungumzo na rais aliyepo mamlakani Uhuru Kenyatta ili kuweza kupatikana kwa suluhu ya kisiasa kati ya wawili hao.

Bw. Odinga amesema kuapishwa kwake kutafanyika Januari 30 kama ilivyopangwa awali na kila mkenya amealikwa kuhudhuria hafla hiyo na kueleza kuwa huenda ikamlazimu afanye hivyo akiwa mafichoni.

Rais Kenyatta kwa upande wake amekuwa akiuhimiza upinzani wa NASA kuachana na siasa kwani kipindi cha siasa tayari kimekamilika kwa mujibu wa kalenda ya matukio nchini Kenya.

Matamshi ya Bw. Odinga kuwa ataapishwa na kuwa rais wa wananchi yamekuwa yakiibua hisia mbali mbali miongoni mwa wakenya wengi wakijiuliza kule anapoelekea kutekeleza majukumu ya urais wakati ikulu ya Kenya ina mwenyeji ambaye ni Uhuru Kenyatta, Odinga hakubaliani na hilo.

Wachambuzi wa siasa za Kenya wamekuwa wakitofautiana kwa kauli kuwa huenda Odinga na vinara wenzake wanatumia kisingizio cha kuapishwa kama chambo cha kutaka mazungumzo na Bw. Kenyatta na vile vile kujumuishwa katika serikali, lakini Bw. Odinga anasema hilo si kweli hata kidogo.
Chanzo: VOA
 
Hii ilitokea Uganda, sasa Kenya, what next
 
Atakuwa anahudumu kama rais wa Kenya..!?
Au huku kuapishwa kumekaaje maana Kenya itakuwa na marais wawili.
 
Mmmh hivi huyu R hana kazi zingine jamani?aache watu watulie wafanye kazi zao.
 
Musyoka, Wetangula na Orengo hawaungi mkono huu mpango wanasisitiza mazungumzo.. Tayari NASA ina mpasuko na kwa kawaida ya kisaikolojia na kisiasa huu mpango haupo
 
Atakuwa anahudumu kama rais wa Kenya..!?
Au huku kuapishwa kumekaaje maana Kenya itakuwa na marais wawili.
Kasema akiwa mafichoni sasa kama rais akiwa mafichoni ataapishwa nanani? Au atajiapisha maana sidhani kama jaji mkuu ataenda huko kinyemela na kumwapisha.
 
Musyoka, Wetangula na Orengo hawaungi mkono huu mpango wanasisitiza mazungumzo.. Tayari NASA ina mpasuko na kwa kawaida ya kisaikolojia na kisiasa huu mpango haupo
James Orengo ndio mchora ramani
lkn nyuma ya huo mpango ni kumshinikiza Kenyata
aridhie mazungumzo
 
Orengo anajifanya yuko smart sana ila kwa sasa kule Jubilee Samoe R ndio anaongoza jahazi na huyu anajulikana kwa misimamo na siasa za kimafia
 
Jee ukawa wanasemaje kuhusu hili? Jee Upinzani kenya unaminywa? Jee Uchaguzi wa Kenya ulikuwa halali?
 
Orengo anajifanya yuko smart sana ila kwa sasa kule Jubilee Samoe R ndio anaongoza jahazi na huyu anajulikana kwa misimamo na siasa za kimafia
Ofcourse Orengo yupo smart.
infact he is one of the top lawyer in Kenya
pia siasa za mapambano/upinzani ameanza zamani sana
1980s huko wakiwa na kina Paul Muite jamaa aliyewatetea IEBC kwenye
kesi ya uchaguzi
 
Anachotafta atakipata...
Walisema watachukulia ni kosa la uhaini na adhabu yake ni Kunyongwa
 
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga amesisitiza kuwa ataapishwa, kutwaa madaraka na kuunda baraza lake la mawaziri hata kama ikimlazimu kufanya hivyo akiwa mafichoni.

Katika mahojiano maalum na Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika, Bw. Odinga amefuta uwezekano wa kufanya mazungumzo na rais aliyepo mamlakani Uhuru Kenyatta ili kuweza kupatikana kwa suluhu ya kisiasa kati ya wawili hao.

Bw. Odinga amesema kuapishwa kwake kutafanyika Januari 30 kama ilivyopangwa awali na kila mkenya amealikwa kuhudhuria hafla hiyo na kueleza kuwa huenda ikamlazimu afanye hivyo akiwa mafichoni.

Rais Kenyatta kwa upande wake amekuwa akiuhimiza upinzani wa NASA kuachana na siasa kwani kipindi cha siasa tayari kimekamilika kwa mujibu wa kalenda ya matukio nchini Kenya.

Matamshi ya Bw. Odinga kuwa ataapishwa na kuwa rais wa wananchi yamekuwa yakiibua hisia mbali mbali miongoni mwa wakenya wengi wakijiuliza kule anapoelekea kutekeleza majukumu ya urais wakati ikulu ya Kenya ina mwenyeji ambaye ni Uhuru Kenyatta, Odinga hakubaliani na hilo.

Wachambuzi wa siasa za Kenya wamekuwa wakitofautiana kwa kauli kuwa huenda Odinga na vinara wenzake wanatumia kisingizio cha kuapishwa kama chambo cha kutaka mazungumzo na Bw. Kenyatta na vile vile kujumuishwa katika serikali, lakini Bw. Odinga anasema hilo si kweli hata kidogo.
Chanzo: VOA
Huyu jamaa kumbe naye ni mpumbavu kabisa, rais yuko ikulu, mihimili yote ya nchi inamtambua,arafu yeye anataka ajiepushe ili amtawale nani na kwa ofisi ipi ya umma,?
 
Back
Top Bottom