Raia wanapaswa kuiogopa serikali yao au kuiheshimu?

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,655
Raia wanapaswa kuiogopa serikali au kuiheshimu?

Raia hapaswi kuiogopa serikali yake bali kuiheshimu atakapoiogopa serikali yake atakuwa anauza uhuru wake na kuwa mtumwa.

Hivyo raia wasiogope kutoa maoni yao na kuikosoa serikali. Kinyume chake watakuwa wameuza utu wao na uhuru wao. Watu lazima waongee wanapoona wanavyoongozwa sio. Hii ni haki yao ya kimsingi. Waongee bila uoga.

Bila uhuru wa kuongea na kutoa maoni jamii inakuwa ni ya mdumao. Fikra hazitakua.

Lakini pia tunapaswa kutumia uhuru huu kwa kuwajibika.

Raia wanapaswa kukataa mambo ya kipuuzi yanayofanywa na serikali yao kwasababu inahusu maisha yao ya sasa na ya baadae ya watoto wao. Kama kuna jambo la kipuuzi linafanywa na serikali wasiogope kupinga.

Raia kama wanaona serikali inakowapeleka siko wanakotaka kwenda Kwanini wasinyanyue sauti na kuongea?

Na kama kwa kuongea kwake anakandamizwa kulikuwa na umuhimu gani wa kudai uhuru kwa wakoloni? Wakati hayuko huru kutoa maoni kwenye taifa lake mwenyewe na kukosoa anapoona Mambo hayaendi sawa?

Kuwa raia huru kwenye taifa lolote ni lazima pia uwe na uhuru wa kutoa maoni ya jinsi unavyoongozwa bila uoga wala hofu.

Lakini pia raia wakawa responsible kwa kile wanachoongea. Tutajengaje hii kuwajibika kwa watu wetu? Ili wawe na uhuru wa kuongea na kuutumia responsibly? Hatuwezi kuwanyima uhuru huu ni haki yao lakini tutawajengaje kuwa responsible citizens wanaojua cha kuongea chenye manufaa kwa taifa lao?

Tunakubaliana wote uhuru wa kuongea bila kuwa na mipaka na wajibu kwa taifa unaweza pia kuharibu taifa.

Lakini bado sio busara kuwanyima watu uhuru huu au kuwafanya watu kuwa na hofu kutoa maoni yao au kukosoa serikali yao.

Raia wana haki ya kumsema kiongozi yoyote lakini wanawajibika pia kumtendea haki kwa yale ambayo ni ya kweli.

Na msingi ambao utajenga taifa hili ni kijadiliana kwa hoja na kuheshimiana

Watu wasiogope kwenda jela kwa kuongea ukweli.Ni bora kufungwa kwa kuonewa kuliko kufungwa kwa Makosa. Usiposema ukweli usaliti utakusuta.

Na utakuwa hujalisaidia taifa lako kusonga mbele. Kwasababu taifa lolote linatakiwa kutafuta ukweli utakaofanya taifa hilo kuendelea hatupaswi kuficha ukweli kwa hofu.

Kama Unajua ukweli na unataka kurekebisha taifa lako simama ongea utakuwa umelifanyia huduma bora taifa lako na utakuwa mwenye faida. Kinyume na hapo hatutafika kama taifa kwa kuogopa kusema ukweli na kukumbatia uongo na matendo maovu.
 
Back
Top Bottom