Raia wa Zambia afia hotelini Dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141
Wambura-July22-2014(1).jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura

Watu wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti, akiwamo raia wa Zambia, Bryton Chimidu (45), aliyekutwa amekufa akiwa katika chumba alichopanga katika hoteli moja, jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema katika upekuzi, raia huyo wa Zambia alikutwa na hati ya kusafiria iliyotolewa na Jamhuri ya Zimbabwe.

"Alikutwa amefariki, huku amekaa sakafuni na kuegemea ukuta akiwa uchi majira ya saa 4:00 asubuhi. Pembeni yake kulikuwa na dawa mbalimbali za hospitali pamoja na chupa tupu tatu za pombe aina ya Peronastroo na kopo tupu la kinywaji aina ya Redbull," alisema Kamanda Wambura.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na uchunguzi unaendelea kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo, alisema mkazi wa Kizota-Tungi, Kigamboni, Amini Mwakibala (55), ambaye ni mkulima, alifariki dunia juzi majira ya saa 10.00 usiku, baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya vipande vya maturubai.

Alisema marehemu alikuwa akiishi na familia yake na kwamba, inasemekana alikuwa na mgogoro na mke wake, Frida Samweli (44), ambaye anashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo na kwamba, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Vijibweni.

Pia Kamanda Wambura alisema mkazi wa Kibaha, Wille Emanuelly (35), amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akivuka barabara, majira ya saa 4:00 usiku, maeneo ya Kibamba na kwamba, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya taifa Mhimbili.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema mkazi wa Mazizini, Alfonce Adolf (23), amefariki dunia baada ya kugongwa na gari, majira ya saa 10.30 alfajiri wakati akivuka barabara.

Alisema dereva wa gari lililomgonga, Shomari Hassan (35), anashikiliwa na polisi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom