Raia wa China mbaroni kwa rushwa

Raia wa China mbaroni kwa rushwa

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,361
Reaction score
4,816
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, imemkamata raia wa China Bwana SHENG BING LIN (40) kwa kosa la kushawishi na kutoa rushwa kiasi cha shilingi laki moja (100,000/=) ambapo ni kinyume na Kif cha 15 (1) (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Raia huyo wa China ambaye ni Msimamizi (Supervisor) wa kampuni wa JX BETTING alishawishi na kutoa rushwa ya shilingi 100,000/= kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Calfonia-Nyegezi (jina limehifadhiwa) ili aweze kumrejeshea mashine yake ya kuchezeshea mchezo bahati nasibu.

Mchina huyo alishawishi na kutoa rushwa baada ya mashine yake ya kuchezeshea bahati nasibu (Betting) kukamatwa kwa kosa la kutokuwa na kibali, kuchezesha nje ya muda uliopangwa na serikali pamoja na kuwahusisha watoto chini ya umri wa miaka 18 katika mchezo huo.

Mashine hiyo ilikamatwa mwanzoni mwa mwezi Juni, 2020 katika maeneo ya Nyegezi Calfonia na kupelekwa katika kituo cha polisi Nyegezi. Hata hivyo, Mchina huyo alipokuwa akitakiwa kufika kituoni kutoa maelezo kuhusiana na kosa hilo hakuweza kutii amri hiyo badala yake alipiga simu na kumshawishi Afisa mtendaji ampe rushwa ili amrejeshee mashine yake.

Hapo ndipo mtego ulifanyika, mnamo tarehe 2 Juni 2020 Mchina huyo alikamatwa na Maafisa wa TAKUKURU katika maeneo ya Lakairo Hotel - Kirumba wakati anatoa rushwa ya shilingi laki moja kwa Afisa huyo wa serikali.

Bwana SHENG BING LIN (40) anafanya kazi hii ya kuchezesha mchezo huo wa bahati nasibu (Betting) katika maeneo mbalimbali ya mjini na vijijini katika Mkoa Mwanza.

Uchunguzi wa tuhuma hii umekamilika na leo tarehe 06 Juni,2020 Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Aidha, tunampongeza mtumishi huyu mzalendo ambaye ametimiza wajibu wake wa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa, kwa kutoa taarifa na kufanikisha kukamatwa kwa mchina huyo. Tunaendelea kuwahimiza wananchi wote wasikae kimya, wawe tayari kukemea vitendo vya rushwa pindi vinapojitokeza kwa kutoa taarifa TAKUKURU.

Kwa pamoja tutashinda vita dhidi ya rushwa

“Kwa taarifa za vitendo vya rushwa fika ofisi ya TAKUKURU iliyo karibu nawe, tumia TAKUKURU APP, piga simu ya dharura namba 113 au tuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 113 au Piga *113# fuata maelekezo” Huduma hii ni ya BURE.
 

Attachments


Kwanza tuelezwe huyo mchina aliingia Tanzania kufanya nini. Maana hili sio tu suala la kutumia mashine isiyo na kibali bali pia kufanya kazi bila kibali. Je ana kibali cha kuchezesha kamali?

Pili, kama alipewa kibali cha kuchezesha kamali, basi kuna wendawazimu pale Uhamiaji wanata vibali kwa mchina kuja nchini kuchezesha kamari ndogo, kitu ambacho hakina msaada wowote kuchangia uchumi wetu bali kuharibu maisha ya watu wenye kipato cha chini.

Tatu, serikali ya China ina tabia ya kushinikiza wananchi wake waachiwe wanapokamatwa kwa makosa ya jinai. Huko kwao mtu mweusi akitongoza mchina anauwawa, na wanatubagua sana. Sasa hii ni nafasi ya kuwaonyesha kuwa hawawezi kutuchezea kwenye nchi yetu wenyewe. Huyu aswekwe ndani tu, hakuna faini kwenye rushwa. TAKUKURU msifanye mzaha hapa.
 
Back
Top Bottom