Raia Mwema: Zitto kuchukua maamuzi magumu...

Raia Mwema: Zitto kuchukua maamuzi magumu...

lutondwe

Senior Member
Joined
Dec 20, 2010
Posts
150
Reaction score
74
Wahe.wanaJF,

Leo kwa kweli nimebahatika kusoma kwa kina Gazeti la Raia Mwema.

Katika gazeti la leo kuna mambo mawili yamenishtua.
1.....zito asepa
2. uhuru wa fikra utawang'oa madikteta.

Kilichonivutia katika gazeti hili ni juu ya mahusiano ya taarifa zote ambazo zimeandikwa. Mwandishi wa habari ya kwanza simfahamu ila mwandishi wa habari ya pili ni Zito mwenyewe. Katika habari ya kwanza hapo juu inaelezwa kuwa Bwana Zito yuko Kigoma anatarajia kufanya maamuzi magumu. Na habari ya pili ambayo mwandishi ni yeye mwenyewe sehemu ya mwisho anaandika: "wakati mwingine ni vema kuwapa maadui zako watakacho na wewe kubaki mwananchi,mwanasiasa wa kitaifa na mpinzani wa status quo"

Kwangu binafsi nadhani kuna kila dalili ya kufanyika turning point ndani ya CDM siku chache zijazo. Hongereni sana CDM kwa misimamo isiyoyumba.
 
Mi naomba atuachie panya wetu tu; paka wasijekukosa msosi
 
Ki msingi zito hana maadui ndani ya CDM,bali kauli zake zinatupa mashaka na uroho wake wa madaraka na kiburi cha rusifa!
 
Ki msingi zito hana maadui ndani ya CDM,bali kauli zake zinatupa mashaka na uroho wake wa madaraka na kiburi cha rusifa!

ndugu yako sema wewe si Adui wa Zitto usijivike dhamana ya kusema hana Maadui, wapo wengu tena wengine wamejidhirisha humu mitandaoni na wengine kwenye Vikao kwa Kifupi usiwasemee watu iwe wana hoja au hawana hoja hata ikitokea chance ya Kum Poison Zitto they kan du!!
 
Zitto tubu dhambi za uasi kamanda kwan bado tunakupenda ila tatizo ww ndio hutupendi kwan ungetupenda usingetusaliti kamanda.
 
Last edited by a moderator:
Taarifa nilizonazo amezungumza jimboni kwake leo lakini sijui kama aliyoeleza ni maamuzi magumu.

Amesema migogoro inayotokea Chadema inapikwa ili chama kionekane kuwa na migogoro, sasa haya ndo maamuzi magumu!

Mzee wa mnyama! Asante kwa kuweka usawazo!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Zitto tubu dhambi za uasi kamanda kwan bado tunakupenda ila tatizo ww ndio hutupendi kwan ungetupenda usingetusaliti kamanda.

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema katika moja ya hotuba zake kwamba "Dhambi ya ubaguzi ukishakuitenda haikuachi, lazima ikutafune". Mimi nasema "Dhambi ya usaliti ukitenda lazima ukutafune haijalishi wewe ni nani katika jamii hiyo". Hakuna msaliti wa raia wa Tanzania atakayedumu bila adhabu. Mwalimu aliongeza kuwa "wakati mwingine adhabu hazisubiri, huja wakati ule ule wa Kitendo". TUSUBURI TUONE Maana naona kama nchi INATIKISIKA kadri miaka inavyosonga mbele.
 
binafsi sina tatizo na maamuzi ya aina yeyote atakayochukua, hatakuwa na madhara yeyote akiwepo asiwepo CHADEMA inayoyoma kuelekea magogoni 2015
 
Zitto tubu dhambi za uasi kamanda kwan bado tunakupenda ila tatizo ww ndio hutupendi kwan ungetupenda usingetusaliti kamanda.


Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema katika moja ya hotuba zake kwamba "Dhambi ya ubaguzi ukishakuitenda haikuachi, lazima ikutafune". Mimi nasema "Dhambi ya usaliti ukitenda lazima ikutafune haijalishi wewe ni nani katika jamii hiyo". Hakuna msaliti wa raia wa Tanzania atakayedumu bila adhabu. Mwalimu aliongeza kuwa "wakati mwingine adhabu hazisubiri, huja wakati ule ule wa Kitendo". TUSUBURI TUONE Maana naona kama nchi INATIKISIKA kadri miaka inavyosonga mbele.
 
Utakuwa ni uamuzi wa kusamehe panya wetu!
Hana lolote huyo kaona cdm mipango na ni mwaka wa nguvu ya umma sasa anataka kutupoteza kwenye mstari!

Huyu ni wa kupuuzwa hawezi kuchukua maamuzi magumu ni kigeugeu!
 
Alikua kigoma akijenga chama haya magazeti yaache habari ya kuuzia magazeti yao.
 
Niliacha kumwani Zitto tangu awekwe kwenye kamati ya Madini enzi zile..siyo yule tunayemjua...
 
Zzk abaki tu cdm ili wachinjaji kwenye sherehe za chama wasikosekane
 
Back
Top Bottom