Raia Mwema: Ya first lady, kufuru na anguko la Dk. slaa

Incredible

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,031
Reaction score
1,603
"Enyi wake, watiini waume zenu, kwa maana mume ni kichwa cha mkewe….Enyi waume, wapendeni wake zenu" (Waefeso 5: 22, 25)

YAMEKWISHASEMWA na kuandikwa yote; tena kwa ufasaha, vina, mizania na kwa wino wa kukoleza, kwamba Dk. Willbrod Slaa hakujivua Ukatibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa hiari kama alivyodai, bali kwa shinikizo na vitisho kutoka kwa mkewe (wa pili), Josephine Mushumbusi.

Vyombo vya habari vimedadisi na kutamka, wakati "baba" msimamizi wa kiroho wa "familia" ya Dk. Slaa, Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima naye amethibitisha hivyo na kwa Dk. Slaa kutupiwa virago nje na kulala nje kwenye gari kufanya shinikizo limwingie.

Sababu za shinikizo la mama huyo ni baada ya Dk. Slaa kukubaliana na Ukawa unaoundwa na vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, National League for Democracy (NLD) na CUF, kumwachia Edward Lowassa kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Umoja huo badala ya yeye (Slaa) na kufifisha matumaini ya Josephine ya kuwa mama Rais au "First Lady".

Awali, Slaa alitoa sababu za kujing'atua Chadema na Ukawa, kuwa ilikuwa ni kupinga kuruhusiwa kwa Lowassa kugombea urais kupitia Chadema akimwita "fisadi" aliyekubuhu, na kwamba yeye Slaa hakuwa tayari kusaliti nafsi na dhamiri yake kwa kukaa meza moja na mtu ambaye alikwishamtema moyoni kama fisadi. Hata hivyo, inadaiwa kwamba Slaa ndiye aliyependekeza kwa Ukawa Lowassa aombwe kujiunga na Chadema ili aweze kugombea urais, tofauti na sababu alizotoa kuonesha kwamba alificha ukweli.

Alichokiita "kusaliti nafsi" si usahihi wa jambo lenyewe, bali alichofanya ndio usaliti na anguko lake kiutashi (moral) na kwa kuchukua uamuzi uliopingana na dhamiri (conscience) yake kwa shinikizo la ubavu wake, huku akitibu majeraha moyoni kwa kujaribu kuuwa taasisi ya umma (Ukawa) kwa kusema uongo kuficha udhaifu na chimbuko la kweli la anguko lake.

Na kwa sababu amejaribu kuficha udhaifu wake kwa kutuipa madongo wengine, basi ajiandae kwa adha ya usemi kwamba, "Kama unaishi kwenye nyumba ya vioo, fikiria hima kabla ya kurushia mawe wapiti njia". Na kwa sababu pia Slaa wetu amekubali kujiingiza kwenye mchezo mchafu na hatari wa kisiasa kwa lugha chafu na kwa kujikweza kwa tabia, afahamu hakuna fidia kwa mtu ajitiaye kwenye mazingira ya hatari kwa hiari yake mwenyewe – "volent non fit injuria"; na kwa kujikweza kwake kitabia, ajue amejinadi kwa mashambulizi.
Lakini hilo lisituchukulie muda wetu kwa sababu udhaifu wa mwanaume kwa mwanamke, haukuanzia kwa Slaa, bali kwa babu yetu Adamu pale Eden, alipoamua kujirahisi na kukubali kudanganywa na mkewe, Hawa kula tunda walilokatazwa na Mungu na kusababisha anguko la mwanadamu kufikia kuhitaji kukombolewa, kama ambavyo tu Slaa anahitaji kukombolewa kwa anguko lililomfika.

Pia tunasoma na kuonywa juu ya ulaghai wa mwanamke, kwa namna Nabii Samson alivyodanganywa na Delillah, amwambie asili ya nguvu zake zilizompa ushujaa wa vita, Delillah akijinyenyekeza kwa mahaba na kutishia kumwacha kama asingefanya hivyo. Hatimaye Samson akalainika, akatoa siri kwamba, ni nywele zake ambazo hakupata kuzinyoa tangu kuzaliwa, zilizompa ujasiri na nguvu. Kisha Delillah, haraka haraka, akaitoa siri hiyo kwa maadui (Wafilisti); wakatumwa wapelelezi wanyatiaji, wakamkamata na kumnyoa; akaishiwa nguvu, wakamtoboa macho asiwe shujaa tena.

Hadithi za kimisahafu juu ya maanguko ya wanaume kwa ulaghai wa "wanandani" wao ni nyingi kutoa fundisho inapotokea mke kutawala mume. Lakini kubwa na lenye kushabihiana na yaliyomkuta Slaa, ni lile la Jenerali mmoja wa Ki-Skochi, Macbeth, ambaye kwa kuamini utabiri wa Wachawi, ukipewa nguvu na shinikizo la mkewe, aliamua kumuua Mfalme wake, Duncan ili avae taji la Ufalme, na mke apate kuwa "first lady" kwa udi na uvumba.

Katika tamthiliya hii iliyotungwa mwaka 1506, gwiji la Fasihi la Kiingereza la miaka ya 1500, William Shakespeare, anaelezea jinsi tamaa ya Macbeth ya kutawala ilivyopandikizwa kwake na viumbe wa giza (Wachawi) na tamaa hiyo ikapandikiza tamaa juu ya tamaa ya mkewe ya kuwa "first lady", kufa na kupona na kwa njia chafu.Ni katika kitabu "Macbeth".

Jenerali Macbeth, shujaa wa vita, kama Dk. Slaa alivyokuwa shujaa na mwanaharakati wa siasa za "ukombozi"; alikuwa akirejea nyumbani, yeye na Jenerali mwenzake, Banquokutoka uwanja wa vita. Nyikani akakutana na wachawi watatu (Weird Sisters) waliowasubiri, wakamwita, Macbeth, akasimama kuwasikiliza; wakamtabiria mambo makubwa, wakisema, "Usifiwe, Macbeth kwa ushujaa; utakuwa mtawala wa Glamis".Mchawi wa pili akasema, "Utakuwa mtawala wa Cawdor"; na wa tatu akamtabiria ufalme akisema, "utakuwa Mfalme baada ya hapa". Cawdor lilikuwa moja ya "majimbo" ya Scotland chini ya Mfalme Duncan, ambako Macbeth aliwanyuka vibaya kwa ushindi, Waasi wa mtawala wa Cawdor na wavamizi kutoka nje dhidi ya Ufalme.

Wakiwa bado njiani, muhudumu wa Mfalme Duncan aliyeitwa Ross, akatumwa kwa Macbeth kumpa ujumbe kwamba, Mfalme alimteua Macbeth kuwa mtawala wa Cawdor. Kuanzia hapo, Macbeth akaanza kuamini utabiri wa wachawi hao watatu; akajawa matumaini kwamba, hata ule utabiri uliobakia, kuwa "atakuwa Mfalme baada ya hapo", nao ulikuwa wa kweli na kujijengea kile Shakespeare anasema, "vaulting ambition, which overleaps itself/And falls on the other"; yaani, "tamaa ya makuu ya mruko, yenye kujipaaisha na kuangukia juu ya nyingine.

Kwa furaha ya kupagawa, Macbeth alimwandikia mkewe kumfahamisha juu ya utabiri wa wachawi, na jinsi alivyokuwa na imani nao akasema: "They met me in the day of success; and I have learned by the perfectest report, they have more in them than mortal knowledge of what greatness is promised thee". Kwamba, "Nilikutana nao siku hiyo ya ushindi; nimejifunza kwa utabiri wao ulio sahihi, kwamba wana uwezo na elimu zaidi ya kiumbe wa kawaida kwa kutabiri kwa usahihi ukuu unaotungojea".

Ndivyo ilivyokuwa kwa Slaa, kwamba baada ya kudhihirisha ushupavu wake katika siasa za upinzani na mabadiliko, washabiki wake na wapima mzani wa siasa nchini walimtabiria na kumpa ujasiri kuwa ndiye pekee aliyestahili kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano. Naye haraka haraka, kama Macbeth, akampa matumaini mke wake ya kuwa "first lady" wa tano tangu nchi kupata uhuru; Josephine akaidaka tamaa ya mumewe, akaipandikiza moyoni mwake na kuitia mbolea ikaendelea kukua ndani mwake.
Jioni hiyo, Mfalme Duncan aliwapokea Macbeth na Banquo Ikulu kuwapongeza, na akachukua fursa hiyo pia kumtangaza mwanae wa kiume, kijana mdogo, Malcom, kuwa mrithi mtarajiwa wa Ufalme wa Scotland. Duncan akatangaza pia kuwa mgeni nyumbani kwa Macbeth jioni hiyo.

Macbeth aliondoka hima kwenda nyumbani kwake kuandaa mapokezi ya Mfalme jioni hiyo.Na alipomjulisha mkewe juu ya kuteuliwa kwa Malcom, mama Macbeth alichukia kama ambavyo tu alivyochukiamumewe juu ya uteuzi huo uliowazibia nafasi ya Mfalme na "first lady". Wawili hao wakapanga kumuua Mfalme Duncan usiku huo atakapokuwa usingizini nyumbani kwa Macbeth.

Na ndivyo ilivyotokea kwa Slaa, kwamba baada ya kumweleza mkewe juu ya Ukawa kumteua Lowassa kugombea urais kwa tiketi ya Umoja huo badala yake, mama huyo alichukia na kupigwa na butwaa, kwamba "U-first lady" kwake ulikuwa umeota mbawa; na kwa hasira na kukata tamaa,akamwamuru mumewe ajitoe Chadema na Ukawa ili kuelekeza mashambulizi kwa Lowassa wakose wote.

Mama Macbeth akasema: "O never shall [the] sun that tomorrow see/he [Duncan] that's coming/must be provide for", kwamba "na asilione kamwe jua la kesho huyo [Duncan] ajaye; lazima amalizwe tu", aliapa mama huyo, kama tu alivyoapa mama Josephine Mushumbusi, kwamba Lowassa hatauonja kamwe urais wa nchi, na kwamba Ukawa lazima usambaratishwe.

Na pale Macbeth alipoonesha kusita kuendelea na mpango wa mauaji ya Duncan, mkewe alimkemea, kisha akamjaza ujasiri na matumaini kwamba mpango wao usingegundulika kabla na baada ya kutenda.
Msimamo wa Josephine Mshumbusi, kama ulivyokuwa msimamo wa mama Macbeth, umeripotiwa kwa ufasaha na Askofu msimamizi wa kiroho wa mama huyo, Josephat Gwajima alipomwambia akisema, "Mimi nilishajiandaa kuwa "first lady" na nilishaandaa biashara zangu huko nchi za nje, hivyo siwezi kubadili msimamo wangu" kwa Slaa kutoka Ukawa.

Na hapa ndipo ilifikia Slaa kutupiwa virago nje; wakati Macbeth alitukanwa na mkewe akiitwa "Pakashume mwenye ndevu za kijasiri lakini mwoga wa kutupa, asiye na ujasiri wa kutenda". Ni baada ya Macbeth, kukataa kuchafua mikono yake kwa damu ya Mfalme Duncan, akisema, "we shall proceed no further in this business", kwa kuhofia pia kugundulika.

Mama Macbeth alijichukulia jukumu la kutekeleza mauaji yeye mwenyewe akiomba msaada wa pepo wabaya na mizimu, impe ujasiri na ukatili kumwondolea tabia ya kike akisema, "Come you spirits, that tend on mortal thoughts, unsex me here, and fill me from the crown to the tree top-full; of cruelty, make thick my blood that my keen knife see not the wound it makes/Nor heaven peep through the blanket of the dark….".
Kwa uamuzi huo, alimkanya mumewe afunge mdomo, ajifanye kutulia, awe mpole wa kupendeza kama ua, lakini mjanja kama nyoka chini yake: "look like innocent flower/But be the serpent under it".

Kuamini mizimu na pepo wabaya kwa mama Macbeth kunajidhihirisha pia kwa Josephine. Kwa Askofu Gwajima, ambaye yaelekea uhusiano wake na familia ya Slaa umetokana na uteja wa mama huyo kwake wa kufukuza mapepo yanayomsumbua, amesema: "Mke wa Slaa ana viashiria vyote vya matendo ya kishetani. Ni dhahiri Slaa anayoyafanya yote sio akili zake, anamwendesha vibaya".

Mfalme Duncan aliwasili kwa kina Macbeth akiambatana na wanae wawili, Malcolm (mrithi mtarajiwa, kwa chukizo la Macbeth) na Donalbain, walinzi na maofisa wengine na kupokelewa na mama Macbeth. Wakati huo, Macbeth alikuwa chumbani mwake akizozana na dhamiri yake, kama aendelee na mpango wa kumuua Duncan au hapana. Kwa mara ya pili; akamwambia mkewe wasiendelee na mpango huo.

Hali hiyo, ya kuzozana na nafsi na dhamiri, ndiyo iliyomkumba pia Slaa wakati akikabiliwa na uamuzi wa kujitoa au kutojitoa Ukawa chini ya shinikizo la mkewe ambapo ilimchukua karibu mwezi mzima kufikia kutamka uamuzi aliofikia.

Mama huyo "jasiri" na shetani nyumbani mwa Macbeth alimtukana mumewe akimwambia "amejaa maziwa ya wema wa binadamu wa kijinga kushindwa kuchukua uamuzi kwa njia ya mkato, kwa maana ya kuua;kisha akatishia penzi lao akisema: "Hunipendi, wewe ni mwoga, zezeta kwa tabia/pamoja na kwamba mimi ni mwanamke, lakini ni shupavu"; kisha akatishia, kama alivyotishia mama Josephine Mshumbusi, kuvunja unyumba na nyumba akidai hawezi kuolewa na mwanaume mwoga.

Na pale Macbeth alipoonesha kutishika, taratibu mama Macbeth alimsogelea kumjaza ujasiri na jinsi mpango utakavyofanyika bila kugundulika; kwamba, angewalewesha kwa mvinyo walinzi wote wawili wa mfalme na ambao watalala chumba kimoja na mfalme, mithili ya watu waliokufa kisha Macbeth atanyatia; na kwa kutumia upanga wa walinzi hao, kumuua Duncan. Na akiisha kutenda, atawapaka damu walinzi ionekane wao ndio wameua.

Macbeth,kwa shingo upande akakubali kutenda akisema, "I am settled, and bent up/each corporal agent to this terrible feat", kwa maana ya kuridhika na mpango huo, huku dhamiri ikiendelea kumtesa, na dhamira kumsuta.

Kuanzia hapo, Macbeth alikuwa kwapani mwa mkewe, kwamba kila kitu kilikwenda kadri mwanamke alichosema. Huko ndiko kunakoitwa "Mke kutawala mume" kukidhi matakwa yake lakini kwa anguko la mume, familia au utawala, hata kama matakwa hayo yanasigana na dhamiri ya mume.Ni kufuru dhidi ya msahafu, kwamba "Enyi wake watiini waume zenu, kwa maana mume ni kichwa cha mkewe".
Baada ya chakula cha jioni, kwa uchovu wa safari na usingizi, Mfalme Duncan alikwenda kulala; Macbeth na mkewe wakabakia sebuleni wakiongea kusubiri saa ya kutenda.

Macbeth, huku akiwa bado katika fikra nzito, aliona kama ndoto, jambia likielea hewani; na baada ya luweluwe hilo kupita, akaamua kuua kwa haraka na kwa ukamilifu; "nakwenda, na kazi itafanyika; kengele yanialika…..nitende kishujaa kukupeleka mbinguni au motoni, ewe Duncan mtukufu". Akaingia na kutekeleza mauaji, wakati huo mama Macbeth akisubiri matokeo kwa hamu.

Macbeth alitoka chumbani amechanganyikiwa, kwamba badala ya kuyaacha majambia ya Walinzi aliyotekelezea mauaji, yeye alitoka nayo yametapakaa damu; mkewe akamwamuru anawe haraka kupoteza ushahidi na ayarudishe lakini akakataa kata kata akisema, "Siwezi kwenda humo tena; naogopa nikifikiria nilichotenda". Ndipo mama Macbeth mwenyewe alipochukua majambia hayo kuyapeleka ndani, akawapaka damu nyuso Walinzi waliokuwa hoi kwa ulevi, na kuyalaza pembeni mwao.
Kutokana na kugundulika kwa mauaji hayo, na Macbeth kisha kuwaua Walinzi hao wawili; wana wa Mfalme, Malcolm na Donalbain walihofia usalama wao na kutorokea Uingereza; Macbeth akijivika taji la Ufalme wa Scotland na mkewe akawa "first lady".

Utawala wa Macbeth ulikabiliwa na upinzani kutoka ndani na nje ya Scotland kutimia ule usemi kwamba, "kilichopatikana kwa upanga lazima kilindwe kwa upanga".Na kadri kalamu ya upanga wa damu ilivyozidi kuandika hadithi yake juu ya kurasa ngumu za ukatili, kwa kuchochewa na mizimu ya kishirikina; chuki na hofu zilimwandama muuaji. Kwa sababu ya mitafaruku, afya ya mama Macbeth ikazidi kudhoofu, maasi yakaenea, huku wafuasi wa Macbeth wakizidi kumkimbia, kama ambavyo tu Slaa atakavyozidi kupoteza wafuasi.
Jeshi la Malcolm akitokea uhamishoni Uingereza, kwa kuungana na la Waskochi lilimpa kipigo Macbeth; akauawa kwenye vita ya Dunsinane; Malcolm akatangazwa Mfalme baada ya nchi kumwaga damu, kisababishi kikiwa tamaa ya kupandikizwa, ya Macbeth na mkewe.

Anguko la kwanza la Slaa ni pale akiwa Padri, aliposaliti maisha ya useja kwa kuoa mke na baadaye, kama ilivyokuwa kwa Mfalme Henry VIII wa Uingereza (1491 – 1547) kwa Catherine wa Aragon, kupewa idhini maalumu (specal dispensation) na Baba Mtakatifu, Papa kufanya hivyo.
Lakini pamoja na ridhaa hiyo, kwa tamaa hai na endelevu, kama ilivyokuwa kwa Mfalme Henry VIII aliyelazimisha talaka kwa Catherine ili amuoe Anne Boleyn, Slaa vivyo hivyo amelazimisha talaka kwa mkewe wa ndoa, Rose Kamili ili amuoe Josephine kwa njia ya kukwapua katikati ya kadhia zinazojitokeza kushinda dhamiri yake. Kutaliki na kuoa kinyume cha maandiko, ni anguko la pili na la tatu kwa Slaa.

Tamaa ya mama Macbeth kutaka kuwa "first lady" ilisababisha umwagaji damu Scotland, kama ambavyo tu tamaa ya Mfalme Henry VIII, ya kuoa na kutaliki ilivyosababisha umwagaji damu Uingereza. Kwa tamaa ya Josephine Mshumbusi, kama ya mama Macbeth, iliyopandikizwa kwa mumewekufanya atunge uongo kuchafua hali ya kisiasa nchini katika kipindi cha harakati za uchaguzi imezua mifarakano, taharuki na chuki kwa tishio la amani na utulivu wa kisiasa nchini. Udhaifu alioonesha Slaa, wa kusalimu amri kwa shinikizo, ni mfano mbaya kwa mtu wa aina yake; na hilo ni anguko kwake la nne la kujitakia.

Na kwa nini Slaa amejiruhusu kutumika kwa nguvu ya mizimu ya "mama Macbeth" wa enzi zetu na kushindwa kumkumbusha "Delilllah" huyo kufuru aifanyayo dhidi ya Waefeso 5: 22, 25?.Na mbona wawili hao sasa wanakimbia kivuli chao kwa kuhamia ughaibuni kuficha nyuso zao?.

Hukumu ya BWANAkwa wasiotenda haki na wenye majivuno haikimbiwi, kama ambavyo Nabii Mussa, kwa majivuno yake, hakufaulu kukanyaga nchi ya ahadi, Kanaani; akafia njiani, kwenye mlima Nebo. Hatima ipi, Dakta Slaa?. - See more at: Raia Mwema - Ya First Lady, kufuru na anguko la Dk. slaa

Chanzo: Raia mwema

To Slaa and those alike, things will fall apart for ever and ever! and will come to their mind that immortality lies not in the things one shall leave behind rather in the people that the lifeline has gone through.

Thank you Incredible and Joseph Mihangwa for this delicious and wonderful news
 
Last edited by a moderator:
trust me if Josephine will read this article, suicide is a probable consequence of it.
 
Naona sasa Raia Mwema litaanza kusifiwa tena na wale waliokuwa wameanza kuiponda kwa kudhani linapendelea chama tawala na kuanza kuitwa gazeti saliti,sasa UKAWA watafurahi kisa limemnanga Dr Slaa,tulisema hapo mwanzo Raia Mwema halipendelei upande wowote muhimu kwao ni habari na kuelemisha wananchi,tuelewe ya kwamba ni mtu mwenye akili finyu amabaye anaamini wote tutakuwa upande mmoja,kuwa tofauti sio uhasama,kila mtu ana haki na anavyoamini,wana UKAWA tuache kulazimishana kushabikia UKAWA kisa tunataka mabadiliko au mnaichukia CCM,kumbuka CCM nayo ina mazuri yake na mabaya yake kama kilivyo Chadema,au kama tulivyo wanaadamu,hata vyama vinaongozwa na binadamu ambao ni mimi na wewe,inakera unapoona wahuni wakianza kulazimisha kupenda chama chao kwa kutoa matusi na kejeli kwa wapinzani wao,hata ukiwauliza hicho wanachoshabikia wanakuwa kama kasuka hawajui.Tuwe wastaarabu kejeli,matusi havisadii hakuna mwenye haki zaidi,hii nchi ni yetu sote iwe CCM au Chadema.
 
Waraka ameandikiwa dr.Slaa na mchumba wake wa kudumu Mushumbusi. Anaetakiwa auone na kuuelewa ni mzee Mwanakijiji anaekesha mitandaoni kujaribu kumsafiaha shemeji yake dr. Slaa eti alijitoa chadema baada ya uongozi wa chama kumkaribisha Lowassa kwenye chama huku akiwa anaeleweka ni fisadi. Tena kibaya zaidi kuteuliwa kugombea nafasi ya uraisi. Eti hadi leo hajui kuwa dr.Slaa alilazimishwa na mchumba wake Mushumbusi kujitoa ukawa baada ya kujua hataupata tena u-first lady na kwamba usiku aliporudi Slaa nyumbani alifungiwa nje na kulala kwenye gari. Kwa akili za Mushumbusi alijua Lowassa amejiunga chadema kumpigia debe mchumba wake. Wala wanachadema au ukawa hawakumbuki tena uwepo wa mtu huyo kwenye siasa za ukawa.
 
Last edited by a moderator:
"Enyi wake, watiini waume zenu, kwa maana mume ni kichwa cha mkewe….Enyi waume, wapendeni wake zenu" (Waefeso 5: 22, 25)

YAMEKWISHASEMWA na kuandikwa yote; tena kwa ufasaha, vina, mizania na kwa wino wa kukoleza, kwamba Dk. Willbrod Slaa hakujivua Ukatibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa hiari kama alivyodai, bali kwa shinikizo na vitisho kutoka kwa mkewe (wa pili), Josephine Mushumbusi.

Vyombo vya habari vimedadisi na kutamka, wakati "baba" msimamizi wa kiroho wa "familia" ya Dk. Slaa, Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima naye amethibitisha hivyo na kwa Dk. Slaa kutupiwa virago nje na kulala nje kwenye gari kufanya shinikizo limwingie.

Sababu za shinikizo la mama huyo ni baada ya Dk. Slaa kukubaliana na Ukawa unaoundwa na vyama vya Chadema, NCCR-Mageuzi, National League for Democracy (NLD) na CUF, kumwachia Edward Lowassa kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia Umoja huo badala ya yeye (Slaa) na kufifisha matumaini ya Josephine ya kuwa mama Rais au "First Lady".
Wajameni, ingawa hii issue ni ya longi, na muda mrefu imepita, ila issues za uongo na ukweli zinatumia kanuni ya criminal liabilities, hazifi hata ipite miaka 💯!.

Hoja za makala hii ni uongo kabisa wa mchana kweupe kwasababu ukweli kuhusu Dr. Slaa kugombea urais Chadema, mimi naujua from the horses mouth kwa kuzungumza naye akiwa na mkewe Josephine, ni Josephine ndiye alimzuia Dr. Slaa kugombea, hivyo sii kweli huyu Mama ndio sababu!. Hapa Raia Mwema limeingizwa chaka na 'Mshenga'.

Baada ya kuupata msimamo huu wa Dr. Slaa kutohombea urais niliuweka humu jf, ile ile 2012 nilipoupata Urais 2015 tusimlaumu Zitto: Nani anaujua Msimamo wa Dr. Slaa? hivyo baada ya Lowassa kutua Chadema nilisema Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM!

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!. Dr. Slaa alisusa kwasababu za integrity naombeni msimsingizie mkewe.
P
 
Back
Top Bottom