Raia Mwema latibua njama za vigogo uchimbaji Bauxite | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raia Mwema latibua njama za vigogo uchimbaji Bauxite

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 29, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Habari
  Mwandishi Wetu

  Toleo la 251
  25 Jul 2012


  • Walipanga kumrejea kibali mchimba bauxite kinyume cha agizo la Pinda
  • Baada ya mwandishi kumpigia Waziri Dk. Huvisa, mpango wao wayeyuka

  SAKATA la uchimbaji madini ya Bauxite katika Kijiji cha Marien, wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro limechukua sura mpya baada ya kuibuka utata kuhusu uhalali wa Kampuni ya Willy Enterprises kuendelea kuchimba madini hayo.


  Kauli mbili zinazokinzana kutoka kwa viongozi wa kitaifa ndizo zinazothibitisha utata huo. Ukinzani huo wa kauli umejitokeza kati ya Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC), Boneventura Baya na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dk. Terezya Huvisa.


  Awali, Baya alimweleza mwandishi wetu ya kuwa kampuni hiyo imeruhusiwa kuendelea kuchimba madini hayo lakini baadaye, Waziri Dk. Huvisa alimweleza mwandishi huyo huyo kwamba, hakuna uchimbaji unaoendelea.


  Waziri Dk. Huvisa alitoa msimamo wake huo unaokinzana na taarifa za awali za Mkurugenzi wa NEMC, alipozungumza na mwandishi wetu Jumatatu wiki hii, akisisitiza kuwa amri ya zuio la uchimbaji kuhusu kampuni hiyo iko pale pale.


  Serikali ilizuia uchimbaji wa madini hayo kuanzia Juni 27, mwaka huu, na Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwaeleza wabunge wakati wa kikao cha Bunge kwamba serikali kupitia NEMC ilisitisha uchimbaji wa madini hayo kutokana na athari za kimazingira.


  Pinda alikaririwa akisema; "Mheshimiwa Spika, aidha, hatua za haraka zifuatazo zimechukuliwa dhidi ya uharibifu uliojitokeza: Serikali imesitisha shughuli zote za uchimbaji wa madini ya Bauxite katika eneo la Mlima Shengena kupitia barua kumbukumbu namba NEMC/366/1/Vol.10/17, NEMC/366/1/Vol.10/18, NEMC/366/1/Vol.10/19 za tarehe 27 Juni 2012."


  NEMC waliandika barua hizo za zuio kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wake Dk. Robert Mtakamalenga na zililenga kampuni tatu zilizokuwa zikichimba Bauxite katika vijiji vya Marien na Mhero. Kampuni hizo mbili ni Willy Enterprises na Halima Mamuya & Others (Mamuya ni aliyepata kuwa mbunge wa vitimaalumu mkoani Arusha).


  Aidha, katika kusisitiza umuhimu wa agizo hilo, Waziri Mkuu kupitia Katibu wake, Paniel Lyimo aliandika barua nyingine Julai 5, mwaka huu, akitaka kufahamu hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa agizo lake.


  Katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba 1/EA.273/349/01 kwenda kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula anaeleza: "Ningependa kupata uthibitisho kama uchimbaji umesimama baada ya katazo hilo".


  Hata hivyo, pamoja na juhudi zote hizo za Waziri Mkuu taarifa zinaeleza kuwa kamati ya wataalamu na viongozi wa serikali ilikutana Ijumaa (Julai 20), iliyopita mjini, Same na kuridhia kuwa Kampuni ya Willy Enterprises iruhusiwe kuendelea na shughuli za uchimbaji wa Bauxite.


  Kamati hiyo ambayo hata hivyo bado haijafahamika iliundwa kwa maelekezo ya nani, iliundwa na wajumbe kutoka NEMC, Idara ya Misitu na Idara ya Madini. Wajumbe wengine katika kamati hiyo ni Mkuu wa Wilaya pamoja na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango.


  Taarifa zinaeleza kwamba kabla ya kufanya kikao na kufikia uamuzi wa kuruhusu uchimbaji kuendelea, kamati hiyo ilitembelea eneo la uchimbaji huku wakiwa wameambatana na mwekezaji huyo anayelalamikiwa na wananchi kwa uharibifu wa mazingira.


  "Baadaye kamati hiyo ilikwenda kufanya kikao cha mwisho katika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi. Wajumbe walionekana kuwa ‘wameshawishiwa' na mwekezaji ili kukubaliana kuwa mradi huo uendelee," anaeleza mtoa habari wetu.


  Katika kikao hicho inadaiwa ya kuwa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango, alisema hana tatizo na mradi huo na "kelele" zake bungeni zilikuwa kwa ajili ya "political management" kwani suala hilo lingewafikia wapinzani wake kisiasa, basi wapiga kura wake wangekosa imani juu yake.


  Kilango anadaiwa kuwa karibu na mwekezaji huyo kwa sasa kinyume cha hoja zake za awali bungeni kuhusu mradi huo.

  Madai hayo ya kamati ambayo hata hivyo haijafahamika bado iliundwa kwa ridhaa ya nani serikalini ya kukubali shughuli za uchimbaji ziendelee yanaweza kuwa na ukweli, hasa kwa kuzingatia kauli ya Mkurugenzi wa NEMC, Boneventura Baya kuwa NEMC imeridhia uchimbaji wa madini hayo uendelee.

  Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu Jumamosi (Julai 21), iliyopita Baya awali alieleza kuwa ndiyo kwanza alikuwa amerejea kutoka nchini Namibia kikazi na suala hilo lilikuwa linashughulikiwa na maofisa wake na hivyo apigiwe simu baada ya saa moja.


  Baada ya muda huo kupita, mwandishi wetu aliwasiliana naye. Katika mawasiliano hayo Baya alisema ni kweli wameridhia kampuni hiyo iendelee kuchimba Bauxite kijijini Marien.


  Alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya mwekezaji kukata rufaa kwa Waziri wa Mazingira (Dk. Huvisa) ambaye naye aliiagiza NEMC kushughulikia malalamiko ya mwekezaji huyo.


  Alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu maagizo hayo ya Waziri yalikuwa kwa maandishi au la, mkurugenzi huyo alikuja juu na kutishia kukata simu kwa kuulizwa maswali aliyoyaita ya ‘kuchokonoa".


  "Suala la mimi kuzungumza na Waziri ambaye ni bosi wangu halikuhusu na si suala la chombo cha habari. Usiniulize maswali ya kuchokonoa kama unataka uendelee kuzungumza na mimi subiri nikueleze," alisema mkurugenzi huyo kwa ukali na kuongeza;


  "Mwekezaji ali-appeal kwa Waziri (kukata rufaa) na Waziri aliiagiza NEMC na wataalmu wengine tushughulikie tatizo hilo na kabla ya uamuzi, kamati ilitembelea eneo la machimbo na kukagua shughuli zinazoendelea."


  Alisema kamati hiyo ilibaini kwanza uchimbaji wa madini hayo unafanywa nje ya eneo la Hifadhi ya Msitu wa Shenghena hivyo haiwezi kuathiri mazingira ya msitu huo kwa namna yoyote.


  "Pia mwekezaji alikuwa na mkataba na kampuni za nje (ya nchi) na alishafanya marekebisho ya awali, hivyo kamati iliona aendelee na uchimbaji wakati akikamilisha taratibu nyingine za msingi," aliongeza Baya.


  Hata hivyo, katika mazungumzo yake na mwandishi wetu Waziri Huvisa alisema hana taarifa za kamati hiyo kwa kuwa hakuwahi kupata rufaa ya mwekezaji, taarifa ambayo NEMC wanadai ilitumwa kwake.


  "Kwanza hizo taarifa ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako, uamuzi wa kuzuia uchimbaji haukuwahi kubatilishwa uko pale pale hadi hapo Enviromental Audit itakapofanyika na kujiridhisha kuwa mradi huo hauna athari za kimazingira,"


  "Huyo mwekezaji mimi sijawahi kukutana naye kwa njia yoyote ile ninachokumbuka ni kwamba kuna wakati alitaka kuja kuniona na alinipigia simu, nikamweleza sina haja ya kuonana naye ila atekeleze yale anayoelezwa na wataalamu," alisema Dk. Huvisa.


  Alisema msimamo wa serikali uko pale pale kuhusu suala hilo na aliahidi kutembelea eneo hilo baada ya kuhitimishwa kwa vikao vya Bunge la bajeti vinavyoendelea mjini Dodoma kwa sasa.


  "Kwanza nitafuatilia kama kweli maofisa hao wameruhusu uchimbaji uendelee na wametumia vigezo gani. Lakini pia nitatembelea eneo husika baada ya vikao vya Bunge," alisema.


  Aidha, katika kile kinachoonekana kama mkanganyiko katika suala hilo, mwandishi wetu aliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi, ambaye awali alidaiwa kuwa kinara wa kutaka mradi huo utekelezwe.


  Katika mawasiliano hayo Kapufi alisema; "Hapana, hicho kilikuwa kikao cha wadau ambao walipendekeza Willy Enteprises waondoe udongo wa Bauxite waliokwisha uchimbua kwa ajili ya kuusafirisha lakini mimi nasimamia ile amri ya awali ya kuzuia uchimbaji na hakuna kinachoendelea."


  Kwa upande wake, Kilango hakuwa tayari kuzungumza na mwandishi wetu kwa madai kuwa alikuwa katika kazi ya vikao vya Bunge hivyo apigiwe simu muda ambao hana kazi.


  Alipoulizwa kwamba mwandishi atafahamu vipi ni wakati gani hana kazi ili apigiwe simu, mbunge huyo alijibu kwa ukali; "Nimekuambia niko busy kama hunielewi basi" na kisha kukata simu yake.


  Taarifa zaidi zinaeleza kuwa viongozi na maofisa hao walibadilisha uamuzi wa kikao siku ya Jumatatu, baada ya Waziri Huvisa kuanza kufuatilia suala hilo, muda mfupi baada ya mwandishi wetu kumpigia simu ili kujua msimamo wake.


  "Baada ya kugundua kuwa wanafuatiliwa walibadilisha uamuzi kwani walikuwa wamepanga wamwandikie barua mwekezaji kumwarifu kuwa aendelee na uchimbaji lakini sasa wame-lie low kwanza (wamesitisha)," kilieleza chanzo chetu.


  Lakini wakati viongozi hao wakichanganyana kuhusu mradi huo, wananchi wa kijiji cha Marien wametaka serikali kuchukua hatua madhubuti kudhibiti watumishi wake wanaotaka kupotosha malalamiko yao ya msingi.


  Akizungumza na mwandishi wetu, mratibu wa kupinga uchimbaji huo, Allen Mtaita, alisema wananchi wanasikitishwa na hatua ya watumishi wa serikali kugeuka kuwa washauri, watumishi na wasemaji wa Kampuni ya Willy Enterprises.


  "Tumesikitishwa sana na hatua ya watumishi wa serikali ya kupuuza malalamiko yetu na badala yake wamekuwa wanaambatana na mwekezaji ambaye sisi tunamlalamikia," alisema huku akiwataja majina watumishi hao ambao majina yao yanahifadhiwa kwa sasa.


  Alisema malalamiko yao ya msingi bado ni yale yale kuwa mradi huo hauna tija kwani machimbo hayo yako katika kilele cha milima ya Shenghena na wanahofu kuwa kunaweza kutokea maporomoko ya ardhi na kufunika makazi ya watu zaidi 3000, wanaoishi chini ya mlima huo ambao pia una historia ya maporomoko.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Dr.Huvisa mtoto wa Marehemu Dr. Lawrence Gama kaisha nusa raha za Ufisadi? Uwaziri wa TZ mbaya hivi?
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  nathani uelewa wako ni mdogo sana mtu anayesimamia maslahi ya nchi ndo unamwita fisadi? wewe kweli una upungufu wa uelewa
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,770
  Likes Received: 6,103
  Trophy Points: 280

  Dah! Kweli sisiem ina wenyewe! Dr. Lawrence Gama alikuwa Katibu Mkuu wa chama nadhani kabla ya Philip Mangula. Inaonekana huko sirikalini wamejipanga wenyewe tu. Haya bana.
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hauelewi kweli Mimi nasema nini... I was far away from U... kwanini CCM ni kama CULT; ni wao kwa Wao

  HUVISA ni MTOTO wa Lawrence GAMA, ni kama

  January Makamba wa Mzee Makamba

  NI UCHANGAJI wa UFISADI wa CCM
   
 6. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  CCM ina wenyewe....:wacko:
   
 7. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  kuna wa akina kawawa, mzindakaya, kirigini, hapo hatujaingia kwenye mademu wa vigogo humohumo

  CCM ina wenyewe, :A S cry:
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Makamba, Kawawa, Mwinyi, Mongella Hao wote watoto wao wameshika Madaraka na wanakuja juu taratibu
   
 9. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  hii ndio serikali MAKINI ya CCM bwana....
   
Loading...