Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,291
- 2,466
Nimesoma baadhi ya makala kutoka gazeti la Raia Mwema. Kati ya hizo ni ya Jenerali Ulimwengu na ya Ahmed Rajab. Rajab anazungumzia pamoja na mambo mengine, suala la kijana Isack wa Arusha kutumia neno 'bwege'. Anasema Isack alipewa hukumu ya kulipa shilingi mil 5 na adhabu ya miaka mitatu. Hivi si alipewa adhabu ya kulipa mil 7 au kifungo cha miaka mitatu? Pia Rajab anasema kuwa Isack alipunguziwa fine na kufikia mil 3. Hilo sina hakika.
Jenerali nae anazungumzia usultani vs demokrasia. Anatumia neno 'mzuanda' (au mziwanda?) Kumaanisha mzaliwa wa kwanza ambaye atarithi kiti cha kifalme. Najiuliza tu, kuna usahihi katika hizi makala?
Jenerali nae anazungumzia usultani vs demokrasia. Anatumia neno 'mzuanda' (au mziwanda?) Kumaanisha mzaliwa wa kwanza ambaye atarithi kiti cha kifalme. Najiuliza tu, kuna usahihi katika hizi makala?