Raia mmoja akamatwa akihusishwa na mauaji Pwani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mwananchi mmoja mkazi wa kijiji cha Mchukwi yalipotokea mauaji ya watu wawili usiku wa kuamkia leo, (jina linahifadhiwa kwa sababu maalumu) amekamatwa na Jeshi la Polisi kufuatia taarifa kwamba aliwatangazia wanakijiji kwamba baada ya mwezi wa Ramadhani yatatokea mambo ya hatari.

Taarifa kutoka kijijini hapo zinasema kuwa baada ya taarifa za maujai hayo mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro alifika eneo la tukio leo.

Waliouawa ni mwenyekiti wa kijiji cha Mangwi kata ya Mchukwi wilaya ya Kibiti Hamis Bakari Mkima na mtendaji wa kijiji hicho Shamte Rashid.
 
Kinachotakiwa pale siyo presence au utisho wa IGP bali thorough investigation tofauti na kamatakamata ya kizembe inayooendelea. Hivi hatuna wabobezi kwenye mambo ya upelelezi jamani au tunataka tufike mahali tuite FBI?.
 
Huenda akawa anahusika..

Swali tatanishi: Haya mauaji yanatotokea pande zile yana mlengo gani na yanatuma ujumbe gani kwa nchi na jamii kiujumla?
 
Polisi wawahoji kwa kina wanaofanya uchochezi kwenye futari yamkini wanayajua hata haya
unaona sasa

unafhani wana usalama wakifuata ushauri huu watafanikisha adhma ya kuwakamata hao wauwaji?

umetoa maoni kiitikadi zaidi
 
Kinachotakiwa pale siyo presence au utisho wa IGP bali thorough investigation tofauti na kamatakamata ya kizembe inayooendelea. Hivi hatuna wabobezi kwenye mambo ya upelelezi jamani au tunataka tufike mahali tuite FBI?.
Investigation ni process hata FBI wakija haitakuwa fumba na kufumbua wote wamekamatwa!! Ndo maana hata Osama ilichukuwa miaka mingi kumbaini na kumuua mkuu!!
 
unaona sasa

unafhani wana usalama wakifuata ushauri huu watafanikisha adhma ya kuwakamata hao wauwaji?

umetoa maoni kiitikadi zaidi
watafanikiwa sana maana uvunjifu wowote wa aman unaanza kwa maneno ya kuukuma kundi fulan lisitii sheria au litumie njia zisizo sahihi kutaka matakwa yao yatimizwe
 
Back
Top Bottom