Raia 25 wa Ethiopia wakamatwa Kilimanjaro

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
kamata.jpg

Jeshi la Polisi Kilimanjaro linawashikilia raia 25 wa Ethiopia miongoni mwao tisa ni watoto wenye umri chini ya miaka 18 wakiwa katika kichaka eneo la Himo wakisubiri gari kwa ajili ya kuwavusha kuendelea na safari yao ya Afrika Kusini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Maidizi wa Polisi,Hamis Issah amesema raia hao wa Ethiopia walikamatwa na askari Polisi wakati wa doria wakiwa na kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Baraka itema (25) aliyejitambulisha kama fundi ujenzi.

Raia hao 25 wa Ethiopia wanaendelea kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji kwa kusaidiana na jshi la Polisi na kwamba mara baada ya taratibu kukamilika watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili za kuingia nchini bila ya kibali.

Chanzo: ITV
 
View attachment 843073

Ethiopia hihi yenye bidege ya bombadia au yingine!??
 
Ndoto ya muethiopia ni kwenda kuishi Sauzi.
Sio TANZANIA.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa natamani sana wasiwafunge jela bali wawarudishe tu kwao. Ukisikiliza stori za hao jamaa zina sikitisha sana. Wanalipishwa hela nyingi kufikia hadi dollar elfu nne kwa mtu mmoja ili tu waondoke nchini mwao kupitia nchi jrani wakatafute maisha mahali pengine hasa huko Soth Africa, na huwa hawana shida ya uhalifu au hata kujihusisha na vitendo vya kigaidi kama Wasomali

Lakini wakifika Tanzania hukamatwa wakashtakiwa na kisha kufungwa jela hadi miaka mitatu! Japo ni sheria halali ya nchi yetu lakini nadhani mamlaka zingelifikiria upya suala hili. Angalia hapo kwenye picha utaona wengine ni vijana wadogo kabisa na kosa lao ni kupita nchini kwenda kutafuta maisha ya jasho lao halali mahala pengine maana nchini mwao fursa zimebana sana na maisha kwa raia mmoja mmoja ni magumu

Kenya hawana sheria ya kuwakamata maana nchi zao zimepakana na viza za kuingia zinapatikana mpakani tu. Sisi japo hatuna mkataba huo na hao Wahabeshi tungetumia busara zaidi ili kwanza kuokoa rasilimali za nchi za kuhudumia idadi kubwa ya watu huko magerezani, pia itasaidia kupunguza idadi ya wafungwa na mahabusu kwenye magereza zetu, kwani pia pamoja na ukali wa sheria zetu haija saidia kuondoa tatizo hilo, kwahiyo ni bora busara ingetumika zaidi
 
Chakuchekesha ni kwamba waetheopia huwa hawajitambulishi kuwa ni Waafrika eti wao ni wahabeshi na wana damu ya warabu na wazungu kwa hiyo sisi wabantu ni watumwa wao.Lakini maisha wanayopitia hao watu wangeacha habari ya kuukata uafrika, maana wanatia huruma.Kwashakoo iliwahi waua sana miaka ya nyuma.
 
Ethiopia wana mtandao mmoja wa simu ambao ni 3G .. serikali ikichefukwa inauzima.. kkuna kipindi magufuli aliusifia sanaaaaaa.
 
Hii njia ya Rombo Himo ni ya kale sana. Kupitia njia hii Northerners( Ethiopians Hammites ,Sudan Nilotics) Wali migrate south to the new lands. Ni kupitianjia hizi Makabila kama Mbulus&Iraqis, Nyirambas, Maasai, Chaggas .etc yaliji form. Ila leo hii ni njia haram. Na hao wahamiaji nao wanaitwa wahamiaji haram, Sasa kwanini hizi kabila zilizojiform Kupitia route hii ,Zisingeitwa kabila haram?? Maana zimepatikana Kupitia njia haram?? Na Hao walioingia Kupitia Tunduma (Ngoni,Makonde etc.)Pia Na Hao walioingia Rusumo,Mutukula Na kwingineko Nao je ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakuchekesha ni kwamba waetheopia huwa hawajitambulishi kuwa ni Waafrika eti wao ni wahabeshi na wana damu ya warabu na wazungu kwa hiyo sisi wabantu ni watumwa wao.Lakini maisha wanayopitia hao watu wangeacha habari ya kuukata uafrika, maana wanatia huruma.Kwashakoo iliwahi waua sana miaka ya nyuma.
Wana laana ya kumua haile selasie aliwalaani km alivoilaani Ghadafi libya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom