Rai Yangu kwa Usalama Wa Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rai Yangu kwa Usalama Wa Taifa

Discussion in 'Great Thinkers' started by Ernesto Che, Jul 19, 2012.

 1. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wadau.
  NIMEKAA nikitafakari utendaji wa idara yetu ya Usalama wa Taifa. Hii ni taasisi muhimu sana kwa usalama wa nchi na wananchi wake, nchi zote idara hii ina heshima kubwa ndani ya jamii.
  Kwa miaka mingi tangu uhuru wan chi yetu imekuwa na taasisi ya Usalama wa Taifa iliyo imara. Japokuwa mengi mabaya yalifanywa kipindi hicho na idara hii, lakini muktadha wangu naujenga kuhusu Hadhi na Heshima ya idara hii nyeti.
  Hivi karibuni Usalama wa Taifa (idara) imeingia katika misukosuko kadhaa na wananchi wakiwemo wanasiasa. Mifano michache ni:

  1. Mwaka 2010 baada ya uchaguzi, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema Dr Slaa alitoa shutuma za waziwazi kwa idara ya Usalama wa Taifa kuhusu kuhusika na wizi wa kura na kuingilia mchakato mzima wa uchaguzi ili kuipendelea CCM. Siku chache baadae Afisa mmoja wa Usalama wa Taifa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari AKIKANUSHA.
  2. Tukio la Dr ulimboka limeiingiza idara ya Usalama wa Taifa tena ikiwataja moja kwa moja maafisa wake kutoka Ikulu, hakuna maelezo ya kutoka toka Ikulu kwenye hili
  3. Mbunge wa chadema (aliyevuliwa) Mh. Godbless Lema alitoa tuhuma kwamba hukumu ya kumvua ubunge ilitokana na maagizo ya Ikulu (Usalama wa Taifa ndio wahusika)
  4. Dr Slaa/ Mnyika wametoa shutuma za waziwazi wakiwataja maafisa wa Usalama wa Taifa kutaka kuwadhuru kwa staili mbalimbali

  Hoja yangu
  Idara hii ni muhimu sana, tena yenye heshima na hadhi kwa jamii, ifanye kazi ya kuhakikisha nchi iko salama ili matukio yanayoonyesha udaifu wa mfumo wa kuilinda nchi yetu yasitokee. Mfano Waethiopia wanavuka mpaka na kufia Dodoma katikati ya nchi, je wangekuwa maadui nchi ingesalimika? Je meli zetu zinapata ajali kila mara hakuna hujuma? Madini yanaibiwa na wahujumu uchumi wao wanafanya nini?
  Rai yangu kwa usalama wa taifa ni kutoa kipaumbele maslahi ya Taifa sio kulenga kuwaua viongozi wa upinzani (kama kweli madai ya Dr Slaa)
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe mkuu,wafanye kazi kwa maslahi ya Taifa.
   
 3. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Mawazo ni mazuri sana, lakini hao unaowaambia sasa, mh!
   
 4. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu ni kweli lakini tukiwa kama thinkers walau tuwafikishie ujumbe
   
 5. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #5
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Tuombe mungu idara ya usalama wa taifa iwepo tena tanzania. watu wetu wahakikishiwe usalama wa maisha na mali zao pia, siku hizi ambapo ni kitu kingine kabisa.
   
 6. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #6
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  For the first time mimi nimeona maajabu ofisa wa ngazi ya juu wa usalama akijitokeza hadhara kufanya PR ya kutokuhusika kuiba kura. Image ya kampuni mfano ikituhumiwa kwa bidhaa feki kinga yake ni kuleta bidhaa bora ili kulinda image yake.

  Na kama imechafuliwa ni kudai fidia. Chombo kama hiki kama kilikuwa hakihusiki walitakiwa kumkamata Dr. slaa na kumshtaki. kukaa kimya na kutoa press release sanasana iliwasaidia watu kuiona sura ya kigogo yule. Ajabu mbona mambo ya ajabu? au mi ndo sielewi?
   
 7. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #7
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  haya maswala yako mahakamani huruhusiwi kuyaongelea
   
 8. Asa'rile

  Asa'rile JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 426
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ...wajirekebisheje sasa....ndani ya mfumo huo.?
   
 9. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hapo ndio wanapokosa muelekeo, wanageuka asasi ya chama tawala
   
 10. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #10
  Jul 19, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mawazo ni mazuri lakini pengine jambo la kuzingatia hapa ni nini hasa maana ya usalama wa taifa kwa mujibu wa taasisi hiyo nyeti; nijuavyo mimi kazi ya idara ya usalama wa taifa hasa ni kuhakikisha usalama wa serikali iliyoko madarakani na sivinginevyo. Muono wangu huo unaweza ukawashutua baadhi ya wana-JF lakini ndiyo hali halisi. Dhana hii ya usalama wa taifa inalandana na dhana ya maslahi ya umma, ambayo nayo pia inampa rais aliyoko madarakani turufu ya kuamua ni mambo yapi yapewe hadhi ya kuwa ni maslahi ya umma
   
 11. koo

  koo JF-Expert Member

  #11
  Jul 19, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndugu sio kwamba kila agent wa TISS ni undercover agent wengine niwatumishi wa kawaida ambao kutambulika sio vibaya mfano director wa cia ni General David Howell Petraeus aliye jitokeza wakati ule nikiongozi ambaye lazima ajulikane mfano generali kombe alikuwa mkurugenzi pale tena kwakuteuliwa hadharani.

  Tatizo la hawa usalama wetu sikuizi wanafanya kazi kwa kuiga yanayotendeka kwenye sinema za kijasusi na kulinda viongozi kunapelekea ukaribu mkubwa na viongozi kiasi cha kuacha majukumu yao na kufanya matakwa ya wale wanaowalinda nakuambatana nao kwenye safari za nje ya nchi ingefaa iundwe taasisi nyingine ya kulinda vigogo haw usalama wabaki namajukumu ya msingi ya kukusanya taarifa za kiintelijensia katika nyanja za uchumi ulinzi na nyanza za mahusiano ya kimataifa.
   
 12. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  UWT na Rais aliyepo Ikulu unatumika ku...
  (1) Nyerere:
  • Kudhibiti watu wanaoisema vibaya serikali na siasa ya ujamaa
  • kulinda nchi dhidi ya ugaidi wa maghalibi uliokuwa ukiangusha nchi nyingi za ki-Afrika
  • Kudhibiti wanaofanya magendo, rushwa na kuhujumu uchumi wa nchi
  (2)Mwinyi:
  • Haukuwa na kazi maalumu na wengine walianza kujiuzuru (mf Mh. Lyatonga Mrema).
  • Usalama ulianza kufarakana kwa sababu za ubaguzi wa kidini ..
  (3)Mkapa:
  • Ulianza kuwa na nguvu tena
  • Ulitumika kuwaondowa waliokuwa wanatowa siri za serikali kv Afande Kombe na waliopinga utandawazi mf. Mwl N.
  (4)Kikwete:
  • Chini ya huyu jamaa UWT umekuwa na kazi kubwa ya kulinda ufisadi wa mtandao wa rais na chama.
  • UWT umegawanyika na siri nyingi zipo mitaani.
  • Mauwaji yanayopangwa na UWT ili kuzima mwendokasi wa upinzani na mashinikizo ya wafanyakazi yanaanza kukithiri
   
 13. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  pia na tukio la mwakiembe kulishwa sumu nalo linawausu. Pia nikupe big up kwa uchambuzi wako yakinifu kwani kweli wameshindwa kuwa usalama wa taifa bali sasa wamekuwa janga la taifa na wapigania haki za wananchi
   
 14. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Na siyo kwa maslahi ya ccm!
   
 15. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  washakuwa mabongo lala!
   
 16. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mawazo yako ni mazuri sana ,lakini sina uhakika kama yatafanyiwa kazi!
   
 17. O

  OPTIMUS TZ JF-Expert Member

  #17
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inabidi mbegu ife ili izaliwe tena hakuna kisichowezekana, M4C ni dawa ya kuuwa wadudu waharibifu wa taifa weka gamba,leta uhasama wa taifa jumlisha na Kova ongeza msagi na yule mjeshi wa kutishia wapiga kura shimbo tutapiga dawa kila mahali na hakuna atakayepona ...............mwone lau masha au getrudi mongela kama ukimkosa batilda buriani kwa maelezo zaidi; 2015 tutakuja mlangono kwako jiandae!
   
 18. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  kwani hao ni usalama wa taifa au ni usalama wa CCMabwepande?
   
 19. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  tatizo umeingiza siasa kwenye suala la kitaifa.

  umeegemea zaidi kwenye hoja za chadema kama ndio ushahidi wa taasisi hiyo kutowajibika.

  matamshi ya chama unachokipenda yameweka hitimisho kwa kila kitu.
   
 20. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Usalama wa Taifa kumpeleka Dk. Slaa mahamakani ingekuwa kujivunjia heshima na ingepandisha chati ya juu Dk Slaa.

  Tangu uhuru hata duniani kote sijaona kesi za majasusi na Raia.

  sababu kuu ni kwamba majasusi hawawezi kutoka katika kificho chao na kujiachia wazi mahakamani itakuwa hakuna mantiki ya wao kuitwa taasisi ya siri.

  Ni majasusi wangapi wangeumbuka kupitia kesi na raia kama ingekuwa rais hivyo.
   
Loading...