jang
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 1,413
- 1,180
Nawasalimu wote, moja kati ya changamoto kubwa duniani na kwa nchi yetu ni tatizo la ajira. Takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka wanazuoni zaidi ya laki moja wanahitimu kutoka katika vyuo mbali mbali hapa nchini na katika fani mbali mbali. Nimewaza njia ambayo serikali yetu itumie ili kutunusuru wasomi wake. Serikali ianzishe mfumo wa taasisi zote kufanya kazi masaa 24, hii itasaidia kuongeza ajira mara tatu zaidi ya sasa hivi. Kwa vipi?? Tuchukue mfano tanesco, wakifanya kazi saa 24 hii inamaana kwamba kutakuwa na shift 3. So kama imeajiri watu 70 elfu itatakiwa iongeze watu wengine mara tatu zaidi ili ziwepo shift 3. Njia hii pia itakuza pato la taifa na kuinua uchumi wa nchi mara tatu zaidi ya unavyokuwa. Mheshimiwa raisi, serikali yako imetusomesha kwa gharama kubwa na elimu zinapotelea mitaani. Okoa uchumi wetu na Okoa wasomi wetu, unaweza kunikosoa kwa hoja kama nimekosea. Thanks