Rai ya wazi kwa Zitto Kabwe

Rai ya wazi kwa Zitto Kabwe

zitto anajipambanua kuwa ni mjamaa lakini
anatembelea gari la kifahari aina ya
Hummer wakati watu wa jamii yake hawana
huduma ya maji safi na salama...huyo
inawezekana kwamba haielewi dhana yenyewe
ya ujamaa au kwa makusudi tu ameamua
kuzikopesha akili zake kwa wajinga

kilaza
 
Naona soni kuwa nawe chama kimoja. Kweli CCM imebeba mengi

Mzee Tupatupa

Zitto kawaachieni chama chenu lakini bado mnamsakama tu, mlidhani angepotea katika ramani ya siasa? Sasa wewe ya ACT yanakusumbua nini? Mmeshindwa kuwdhibiti Baba Mkwe na Mkwewe wasimiliki chama, matokeo yake Mkwe kanyofoa kipengele cha kumzuia kugombea, kila anapopata mpinzani ndani ya chama Baba Mkwe anaingilia.

Aisee mwacheni Zitto apumzike.
 
Kibaraka wenu K. Limbu hana pa kutokea safari hii.
Zitto ana haki ya kikatiba kugombea nafasi yeyote ndani ya ACT.

Kumbuka kuwa hiki ni chama cha Siasa na CCM, CDM na vinginevyo ni vyama vya siasa!! sasa sijui kama unajua dhana ya Rivalry party???
 
Acha ushauri wa kimburula ACT sio chama kinachobaka demokrasia kama chadema na cuf ukitaka kugombea unaundiwa zengwe. Yupo huru kugombea nafasi yryote ili mradi havunji kanuni na taratibu za chama.
 
zitto anajipambanua kuwa ni mjamaa lakini
anatembelea gari la kifahari aina ya
Hummer wakati watu wa jamii yake hawana
huduma ya maji safi na salama...huyo
inawezekana kwamba haielewi dhana yenyewe
ya ujamaa au kwa makusudi tu ameamua
kuzikopesha akili zake kwa wajinga

kilaza

Wakati wa ujamaa nyerere alitembelea Landrover tu maisha yote lakini zitto ana Nissani ya kukodi kutoka kwa mkono analipia laki kila siku, ana hammer, ana gari ya ubunge land cruiser ya mkopo yote haya anayatumia kwa kazi gani mjamaa huyu, sie tanzania hatutaki ujamaa kwa sababu hata ubepari hatujaufikia.
 
wewe tupatupa huna maana tena ni bonge la ROFA hivi unawezaje kuzuia mafuriko kwa mikono? utakuwa wazanga mmekwisha sema zzk ni msaliti, sasa ni vema muendelee na shughuli zetu ili atimize malengo yake,zzk ni msaliti sawa, ni muhujumu ni sawa, mroho wa madalaka ni sawa, hana subila ni sawa, aliuza chama nisawa sasa kashatoka endeleeni na shughuli zenu yaani aache kutimizi malengo yake kwasababu ya umbea wenu? achana naye habari zakuchora michoro sijui kachora nini kasha zimaliza mteegeni sehemu nyingine acheni upekupeku na wivu wa kike watu watimize ndoto zao.
 
Kweli zitto kiboko maana humu JF hakuna habari nyingine ni zitto zitto zitto zitto zitto
 
Hasiiki huyu, alihusishwa act lakini Leo kang'atuka cdm kesho huyooo kwenye chama lake na uenyekiti atagombea

Tena kajiunga ACT usiku muda ambao wanga wanafanya kazi.
ACT = Acha Ccm Tule.
 
Hivi jamani, Tanzania hatuna topiki ntingine muhimu zaidi ya hii ya Zitto Kabwe? Hii korasi ishanikinai miye, na tuanzisheni wimbo mwingine. Tuna mambo mengi sana ya kujadili kuhusu taifa hili, hasa mkizingatia huu ni mwaka wa uchaguzi. Kuendelea kumjadili Zitto Kabwe ni kudhihirish a mtazamo wake (au pengine wa mashabiki wake) kuwa yeye alikuwa mtu muhimu na maarufu kuliko Chadema.
Kweli baba...tufanye mambo ya maana.Tuachane naye
 
Mkuu huu ni ushauri mzuri sana!,Ila hofu yangu kwa zzk na ACT yake sio mahala sahihi.Yani kumshauri zzk asigombee nafasi yoyote ndani ya ACT yake! Nafananisha ACT itakuwa na mfumo wa boti au mtumbwi,Injini na naodha nyuma halafu abiria mbele.Yani unamaanisha Mwigamba awe mbele zzt nyuma!? Hawa wenyewe hawaaminiani wote wanapenda unaodha! Thubuutuuuu kwani zzk mjinga kiasi hicho! Yani akubari kupakiwa? Kwani alichowekea mpira kwapani CDM nini? Zzk yeye lazima awe nahodha ili maagizo na maelekezo atakayokuwa anapewa kutoka kwa msoma ramani wake(ccm) hayafanyie kazi mara moja! Kama kuhairisha safari au hata kupindua au kutoboa boti ktk ya bahari ikibidi (maamuzi ambayo anaweza yeye tu zzk hana huruma huyu hata watu wakijaa) na sio na yeye ampelekee mwigamba kichwa maji yule akimchomolea? Yeye atawajibu nini wanaomuweka mjini?.Ngoja tuone! Ila kwa ninavyomuona zzk kwa uroho wa madaraka na anavyojiona yeye ndo kila kitu nahisi yeye kutokuwa mwenyekiti wa ACT hataona maana ya yeye kuendelea kuwepo ACT.
 
Kwako Zitto,

Najua kuwa sasa wewe ni mwanachama wa chama kipya kitakachozinduliwa tarehe 29 mwezi huu kiitwacho ACT-Tanzania. Najua pia kuwa umekuwa ukihusishwa na chama hiki tangu kilipopata usajili wa muda na baadaye wa kudumu chini ya Mwenyekiti Kadawi Limbu,ambaye pia alianzisha chama cha ADC. Najua tena kuwa wewe Zitto umekuwa ukikanusha na kukana kuhusika na ACT-Tanzania wakati ukiwa CHADEMA. Ukajiunga mara tu ya kufukuzwa uanachama CHADEMA.

Zitto,

Chokochoko za tuhuma dhidi yako za usaliti zilihusishwa na mkakati na jitihada zako za kuwania Uenyekiti wa CHADEMA. Imeaminishwa hivyo ingawa yawezekana isiwe kweli. Mchoro wako unaochorwa ni mtu mzalendo,mpenda mapambano ya kidemokrasia na unayechukia rushwa na ufisadi. Mchoro wako hauoneshi usakatonge wako. Wewe na wapambe wako mmekuwa mkiufurahia mchoro huu. Yaweza ukawa si mchoro sahihi. Onesha ukweli wa mchoro huo sasa.

Zitto,

Tafadhali usigombee nafasi yoyote ya uongozi ndani ya ACT-Tanzania hapo tarehe 29 Machi, 2015. Jioneshe kuwa wewe si msaka madaraka;hukuwa unahusika na ACT-Tanzania tangu mwanzo na kwamba wewe si mpenda vyeo na msakatonge. Ukigombea chochote au kudai umeombwa kugombea chochote, Tanzania itathibitisha pasi na shaka kuwa wewe ndiye mchoraji bora wa michoro ya kisiasa ikuhusuyo ingawa huchori kitu sahihi.

Ni ushauri na rai tu!


Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Ushauri ni nzuri, lakini si kila ushauri lazima uukubari.
 
Thibitisha. Chunga kauli zako. Zitakuliza na kukuua njaa kwenye kitengo ulichopo.

Mzee Tupatupa
Unazidi kujidhalilisha kama mwehu, Kitengo gani? Unaandika kama vile unanifahamu kumbe hata kwa rangi hunijui, si uchizi huo?
 
Back
Top Bottom