Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 3,791
- 3,360
Nimefanya utafiti mdogo ktk maeneo mbalimbali hapa nchini kuhusu bei za vyakula hasa nafaka aina ya mahindi na mchele.
1. Kanda ya Kaskazini, maeneo mengi ya Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha na Manyara bei ya mahindi imefikia hadi 120,000/= kwa gunia la kg 100. Bei inaendelea kuongezeka.Hii ni kutokana na mvua za masika kukatika mapema.
2. Kanda ya Ziwa kwa mikoa ya Shinyanga na Mwanza, gunia la mahindi ni Tsh 100,000/= na bei inaongezeka kwa kasi. Bei ya mchele ni Tsh 1500/= hado 2000/= kwa kilo na bei inapanda kwa kasi.
Baadhi ya wafanyabiashara wamedai kuwa mazao hayo mawili mahindi na mpunga uzalishaji wake ulikuwa mdogo mwaka huu kwa baadhi ya maeneo.
Hivi karibuni, kupitia vyombo vya habari, taarifa zimetolewa na mamlaka husika kuwa mipaka iko wazi kupitisha mazao kuuza nje ya nchi. Hili ni jambo jema, lakini tuhakiki kiasi kilichopo maeneo mbalimbali kwanza. Lengo liwe ni kuhakikisha maeneo yenye upungufu kama niliyotaja,yanasambaziwa kwanza kabla ya kuruhusu mahindi hayo kwenda nje.
Sipingani na mipango ya Serikali kuruhusu mipaka kuwa wazi, lakini iwe ni baada ya kujiridhisha kuwa mikoa yote nchini haina uhaba, na bei yake inakuwa reasonable fair!
Mfano bei ya Mahindi Rukwa na Songea ni Tsh 50,000 hadi 55,000/= kulingana na utafiti wangu wa wiki hii.
Si ajabu kutokana na tamaa ya wafanyabiashara wetu kutaka faida kubwa yakapelekwa nje ya nchi na siyo kanda ya Ziwa au Kanda ya Kaskazini. Hivyo, udhibiti wa Serikali ni muhimu sana.