Raha ya ndoa mmoja asafiri...

Raha ya ndoa mmoja asafiri...

Mkuu Tuko wengine wakisafiri muda mrefu wanapata muda mzuri wa kurukia wahudumu wa hotel ua wale wadawa wa usiku!! Ha ha ha!! Na aliyebaki naye anapata muda wa ku-relax na kale kakidumu chake kama si houseboy!! Yote haya ni kwa sababu ndoa nyingi ni ndoana, hakuna mapenzi ila wanafungwa na kiapo cha ndoa eti hadi kifo kiwatenganishe!! Ni ndoa chache kweli akisafiri mwenzako una-mmiss!!! Tuwe wakweli!
 
Bra-joe, kama yalivyo maisha siku zote haziwezi kuwa sawa, namaanisha hakuna mwenye raha kila siku wala mwenye shida kila siku.
 
Last edited by a moderator:
Safari katika ndoa ni kitu cha muhimu sana kwani wakati mwingine mnapeana nafasi ya ku explore mbinu mpya na vingine vinakuwaje ndo maana mnapokutana tena unakuta mwenzako ana maujuzi yameongezeka, mnakuwa wapyaaaaaa.Lakini huwa hatuulizi vipi mwenzangu mbona ujuzi mpya huu? umeutoa wapi? huwa tunachanganywa na haya mapya mazuri. lakini ukweli ni nafasi tuliyoitoa kwa kusafiri kwetu wenzetu wakaitumia kujifunza
 
wewe! Mimi ni mtu ninayejifunza kutokana na makosa ya watu wengine. Usidhani nipo ndani ya ndoa.

Kumbe!!!!! huwezi jifunza ndoa kupitia ndoa ya mwingine, ukija oa/olewa utakuwa tofauti na ndoa unazosema unajifunza.......!
 
Hawa watu waliokuwa wanapiga story wako sahihi kwa kiasi fulani na pia wako wrong kwa upande mwingine, hapa ninachomaanisha ni kwamba huo upya ama utofauti unategemea hali ya ndoa hasa swala zima la amani katika familia husika.

Kwa ndoa yenye amani, furaha, upendo wa dhati nk, pindi mmoja wa wanandoa anaposafiri na kuwa nje ya familia kwa muda mrefu hakika hicho huwa ni kipindi kigumu sana kwa wanandoa hao na hasa kwa mwanaume. Ni kipindi kigumu kwa sababu ya kuwa mbali na familia yako (mke na watoto) na hasa mke maana kukosa zile huduma za mke (tendo la ndoa) huchangia matatizo mengi ambayo ni unnecessary kama hasira, kushindwa kutekeleza majukumu yako ipasavyo, mwili kuwa ovyo, mawazo mabaya, nk (mnaweza tafuta ref za mtambuzi). Hapa naomba kueleweka vema kwamba ni kwa wale ambao ndoa zipo katika amani, furaha, upendo wa dhati nk na ambao kwao kuvunja amri ya sita na tisa ni dhambi kwelikweli (Wakiristu hapo tupo pamoja). Ndoa za namna hii wakati hawako pamoja kuna uwezekano mkubwa amani hiyo kupotea (rejea mtambuzi) na itarudi wakiwa pamoja katika maisha yao ya kila siku, hivyo hili kundi la namna hii kuna upya kidogo, lakini wana haki pia ya kusema ya kwamba wao kwao siku zote ni mpya.

Aidha pia kuna kundi lingine ambao kwao ndoa ni mzigo, hakuna amani, kelele, vurugu, nk hili nalo linaweza kutoa shuhuda tofauti kabisa na hilo kundi la kwanza. Hawa mmoja wao akisafiri hakika amani hutawala na kama ni kipindi kirefu usistajabu kukuta hata mmoja wa wanandoa akapata afya ya mwili na roho kwa muda huo na hivyo upya huo kujitokeza.

Mwisho kabisa, niseme tu hali ya ndoa ni tosha kutoa jibu sahihi kwa mazungumzo hayo. Tuzitunze ndoa zetu katika upendo wa dhati na kwa kufanya hivyo tunatimiza mapenzi ya Mungu kwa kuitika wito wetu hapa duniani na kwa kufanya hivyo tunaongeza siku za kuishi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom