Rage hapo vip? Bado unataka tukutajie namba yako?

Rage hapo vip? Bado unataka tukutajie namba yako?

ngomicom

Senior Member
Joined
Jul 6, 2012
Posts
123
Reaction score
19
Nianze kwa kutoa pole kwa wapenzi, mashabiki na wananchama wenzangu wa Simba, kimsingi yaliyotokea jana si mazuri kwa wapenda soka wote duniani kwani hakuna anayejiandaa kupoteza mechi ktk ulimwengu wa soka.
Ninaloomba kwenu wadau wapenda soka, ni kupata majibu ya kauli ya kiongozi mkuu wa klabu ya simba aliyoitoa siku chache zilizopita kufuatia madai ya wadau wengi kuwa anastahili kuachia ngazi katika nafasi yake ya Uenyekiti. Ndugu Mwenyekiti Rage aliuliza kuwa yeye anacheza namba ngapi mpaka ajiudhulu madarakani. Swali la msingi kwake ni hata kufuatia matokeo ya jana bado anahitaji tumtajie yeye ni namba ngapi?
Maswali mengine mengi yanajitokeza ikiwemo;
  • Usajili ulifanyika chini ya Uongozi gani?
  • Mabadiliko ya Kocha na Benchi la Ufundi yalisimamiwa na nani?
  • Mabadiliko ya benchi la ufundi yalibarikiwa na nani?
  • Wewe si ndiye kiongozi wa juu unayesimamia mipango na mikakati ya timu?
Rage wewe ni Kocha namba 1 wa maendeleo ya timu hivi naamini sasa inapaswa ukae pembeni kuruhusu mawazo mapya ya kuijenga timu. Hatuhitaji kuanza kuchambua umefanikiwa nini na umetuangusha nini wala tusianze kujadili tuhuma zako hapa za mambo mengi ya awali hata zinazokuhusisha na Marehemu Mafisango.
 
Rage hana ujanja this time. Ni lazima akae pembeni ili watu wanaojua kuendesha klabu kwa mafanikio waingie. Hakika akiendelea kuwepo kwenye uongozi hata zile goli 5 tulizowapiga Yeboyebo zinaweza kurudi. Ameishia maarifa na hajui alifanyalo. Kwa nini timu iliyofanya vizuri sana miezi sita iliyopita leo iwe hoi hivi? Hebu kaa pembeni mkuu kabla wenye klabu yao hawajakushikia virungu.
 
Ni mtu mzima,apime mwenyewe,akikaa pembeni itakuwa bora zadi,make mpira na maneno mengi yasiyopimika ni kama mwanasiasa anayewaadaa wapiga kura wake
 
mi nimeamua kusitisha ushabiki na uanachama wangu simba mpaka HAWA TYRANTS RAGE NA KABURU WANG'OKE
 
hahahahah SIMBA BWANA mbona mmechelewa sana kumto mtu huyu, mpaka apigewafuasi wa CHADEMA dodoma ndo mnafikilia kumtoa? Mwambieni na Samweli Sitta na Zitto Kabwe
 
Last edited by a moderator:
Nianze kwa kutoa pole kwa wapenzi, mashabiki na wananchama wenzangu wa Simba, kimsingi yaliyotokea jana si mazuri kwa wapenda soka wote duniani kwani hakuna anayejiandaa kupoteza mechi ktk ulimwengu wa soka.
Ninaloomba kwenu wadau wapenda soka, ni kupata majibu ya kauli ya kiongozi mkuu wa klabu ya simba aliyoitoa siku chache zilizopita kufuatia madai ya wadau wengi kuwa anastahili kuachia ngazi katika nafasi yake ya Uenyekiti. Ndugu Mwenyekiti Rage aliuliza kuwa yeye anacheza namba ngapi mpaka ajiudhulu madarakani. Swali la msingi kwake ni hata kufuatia matokeo ya jana bado anahitaji tumtajie yeye ni namba ngapi?
Maswali mengine mengi yanajitokeza ikiwemo;
  • Usajili ulifanyika chini ya Uongozi gani?
  • Mabadiliko ya Kocha na Benchi la Ufundi yalisimamiwa na nani?
  • Mabadiliko ya benchi la ufundi yalibarikiwa na nani?
  • Wewe si ndiye kiongozi wa juu unayesimamia mipango na mikakati ya timu?
Rage wewe ni Kocha namba 1 wa maendeleo ya timu hivi naamini sasa inapaswa ukae pembeni kuruhusu mawazo mapya ya kuijenga timu. Hatuhitaji kuanza kuchambua umefanikiwa nini na umetuangusha nini wala tusianze kujadili tuhuma zako hapa za mambo mengi ya awali hata zinazokuhusisha na Marehemu Mafisango.

RAGE Simba ikishinda, yeye wa kwanza kwenda kuongea na vyombo vya habari na ku-credit uongozi kwa mafanikio na huwa anatoaga hata technical analysis ya ushindi.

Lakini.................................... kikinuka, zigo analidondosha miguuni mwa technical bench. Kichekesho!

Simba amkeni....shauri yenu!

Wenzenu Yanga walichukuwa swift action na kumng'oa mwenyekiti..matokeo yake wakachukua Kagame cup na sasa wanakimbila taji la 24 la uchampioni wa TZ. Kuna harufu kuwa mwaka huu Yanga watafika mbali sana kwenye CAF champions league na huenda waka-retain Kagame cup for 3 years on the trot. ...unprecedented!!!
Na hiyo ni baada ya boldly kumng'oa yule mwenyekiti wao aliyekuwa akisinzia-sinzia!!

Simba igeni vitu vizuri msione haya!!
 
Apime mwenyewe maana Uongozi si wa kuridhishana anachong'ang'ania nini.

Aende ili wengine waje pia kuepusha Vurugu
wakati mambo mabovu yanaonekana bayana.
 
Jamani hawa Libolo wasituvuruge, mkumbuke Rage bado hajamalizia uwanja wa Bunju, Birmingham bado hawajatua na Mbuyu Twite bado hajakatwa hivyo tumpe muda kidogo.
 
Kazi wa kuwapa ulaji wezi wa ndovu!! Unafikiri atagawaje muda wake kwa club na wa deal? Wekeni mtu serious pale Msimbazi.
 
Back
Top Bottom