Rage akinukisha tena simba

Rage akinukisha tena simba

Chang'o

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
105
Reaction score
21
Akizungumza leo makao makuu ya club amesema kuwa TFF hawana mamlaka ya kuagiza kuitishwa mkutano wa simba kwa hiyo hakuna mkutano wowote utakaofanyika ndani ya hizo siku 14. Pia amesema ameivunja kamati yote ya utendaji na amemteua Richard Michael Wambura kufanya shughuli zote za klabu. Nawasilisha jamvini tujadiliane.
 
Mpaka sasa jukwaa ambalo halina stress ni MMU peke yake. Naweka kambi kule
 
Akizungumza leo makao makuu ya club amesema kuwa TFF hawana mamlaka ya kuagiza kuitishwa mkutano wa simba kwa hiyo hakuna mkutano wowote utakaofanyika ndani ya hizo siku 14. Pia amesema ameivunja kamati yote ya utendaji na amemteua Richard Michael Wambura kufanya shughuli zote za klabu. Nawasilisha jamvini tujadiliane.

Je katiba inamruhusu kufanya maamuzi hayo?
Ngoma bado mbichi Simba. Nyuma ya pazia ni mauzo ya Okwi. Siku ya siku atasema alichukua mzigo aliotumia kuwasajili wachezaji nyumbani kwake.
 
Huyo ndo @Rage hataki masihara na mtu,
wafanye mapinduzi sasa wakati yupo tuone.
 
Wambura akikubali atakuwa msaliti.
Unadhani Rage ni mpuuzi kiasi cha kumteua mtu bila ya kushauriana naye kwanza? Unadhani Wambura halisini sawa na wa maneno yake, hana njaa? Kama Rage, kama Wambura. Nzi hafuatani na nyuki, ila na nzi mwenziwe!
 
Rage kawashika masikio mashabiki wa simba wote, akisema kimya wote kimya hakuna hata wa .!!
 
Huyu jamaa ni fighter. Toka jela straight bungeni na mwenyekiti simba? Kweli determination ni kitu muhimu.
 
Hiyo ndio faida ya kumchukua ex jailbird kukuongoza. Haogopi jela huyoo anatembea nayo kiunoni tena mi mwanachama hai wa kile chama cha msitu na nyika. Pesa anazopata akitokea huko mbugani si mchezo. Ogopa kitu pesa.
 
siasa every where inawezekana Rage yuko sawa au asiwe sawa,pia wanaomksoa hawajui wanastaili kufanya nini
 
Rage asiigeuze Simba yetu kuwa ni taasisi yake ya mfukoni! Ajue Simba ina wanachama wanaolipia kadi zao, na wanahitaji kuona utulivu ndani ya Simba. Rage anangembe sana na kila akizungumza na watu hutoa maneno ya dharau ambayo hayalingani na hadhi ya wanaSimba wala hadhi yake kama mtu mzee na mbunge! Mbona anakuwa kama Ndolanga wakati wa FAT ? Watu wameshakuchoka Rage, wasikilize au waachie timu yao! Hii siyo CCM ni Simba! Wacha bwana nenda zako umewaudhi mpaka mpira pesa ambao wanamchango mkubwa sana kwa Simba kifedha! Mpira bila pesa utafika wapi wewe Rage???
 
Damu gani unaisema wewe...!??

aaaaah mkuu unaniangusha, huko si ndio kuna ma-serial killers!!!? Mie natarajia kuchumbia soon, natafuta mguu wa kuku niwe nao kabisaaa. Kama unao tuongee mkuu.
 
Hahhahaaaa Mpwa wengu Demba umenena vyema, ngoja nikatie nanga kule, nimegundua MMU kumejaa stress za kufa mtu, hakuna anemsifia mpenzie kila mtu analalamika utadhani kalazimishwa kuwa nae huyo alienae, ukiangalia upande wa pili hawa nao form four leaver wanasumbua kweli mara oooh dushelele kubwa sijui dogo mara vitumbua aaaahhgg
haaa haaa Elli bora hata ungesema chit chart.
 
Back
Top Bottom