gambada ynwa
JF-Expert Member
- Nov 24, 2014
- 390
- 371
Wakuu habarini za kushinda!
Mimi nina rafiki yangu ambae tunafahamiana tangu muda mrefu sana. Alikuwa ameolewa lakini bahati mbaya mume wake alitangulia mbele ya haki.
Wakati mume wake anafariki alimuacha na mimba ya miezi mitatu, sasa kutokana na mshituko wa msiba ile mimba ikawa imeharibika. Na akaenda hospital kutoa japo ilimsumbua sana.
Lakini baada ya wiki kama mbili hivi kaniambia eti mimba ilikuwa ya mapacha na walifanikiwa kutoa mtoto mmoja ila mwingine hajatoka hadi sasa na kasema anategemea kufanyiwa upasuaji (kulingana na maelezo yake).
Sasa kutokana na ukaribu wetu mimi nimekuwa nikimsaidia msaada ya kimawazo na kifedha pia.
Lakini kinachonishitua ni pale anaponiambia mtoto mmoja hajatoka bado na yeye naona yupo poa kabisa na katika mazungumzo ya kawaida akawa anaumwa tumbo sana na mimi nikajua ni kwa ajili ya matatizo aliyonayo na nikamwambia twende hospital lakini alikataa lakini baada ya kumdadisi akasema anaumwa tumbo la mwezi yaani mp.
Sasa wakuu naomba mnisaidie ushauri, hivi inawezekana mtu akawa katika hali hiyo na akaingia period?
Au ndo anataka atupige mpunga tu ajidai anaenda kufanya operation kumbe hakuna kitu.
Ushauri wenu ni muhimu sana wakuu