Rafiki yangu anatafuta kazi

Rafiki yangu anatafuta kazi

the maze

Member
Joined
Aug 14, 2015
Posts
40
Reaction score
23
Nina rafiki yangu wa kike nilisoma naye shule ya msingi. Hakufanikiwa kujiunga na masomo ya sekondari, hivyo akaamua kuolewa tu. Kutokana na changamoto mbalimbali, ndoa yake imevunjika mwaka jana. Sasa amekuja mjini kutafuta kazi yoyote halali. Naomba kama kuna mtu anaweza kumpa kazi ya kufanya/ kibarua chochote, tuwasiliane. PM kwa mawasiliano zaidi.

Umri: Miaka 28
Jinsia: Ke
Elimu: Darasa la saba
Anakoishi: Ukonga, Dar es Salaam
Yuko vizuri kiafya, mnyumbulifu, mwaminifu na ni mtunza muda mzuri.
 
Ameniomba nimsaidie kutafuta kazi. Bahati mbaya sana kuna watu wa humu niliochukua mawasiliano yao na kumwambia awatafute wanatumia hiyo nafasi kumfanyia harassment. Inasikitisha mnoo. Tuache huu upuuzi.
Unauhakika gani kwamba amefanyiwa unyanyasaji nawatu wa humu..??
 
Nina rafiki yangu wa kike nilisoma naye shule ya msingi. Hakufanikiwa kujiunga na masomo ya sekondari, hivyo akaamua kuolewa tu. Kutokana na changamoto mbalimbali, ndoa yake imevunjika mwaka jana. Sasa amekuja mjini kutafuta kazi yoyote halali. Naomba kama kuna mtu anaweza kumpa kazi ya kufanya/ kibarua chochote, tuwasiliane. PM kwa mawasiliano zaidi.

Umri: Miaka 28
Jinsia: Ke
Elimu: Darasa la saba
Anakoishi: Ukonga, Dar es Salaam
Yuko vizuri kiafya, mnyumbulifu, mwaminifu na ni mtunza muda mzuri.
Mimi natafuta mhudumu wa vinywaji kama atataka, au kusaidia kazi za nyumbani. Kama yuko tayari kati ya hizo nicheki 0713322856
 
Ameniambia baada ya kukutana na mtu niliyempa namba zake.
Ni ainagani ya unyanyasaji alifanyiwa...??
Maana isije ikawa ametongozwa tu, then anakuja kushtaki kwako kwamba amenyanyaswa...
 
Back
Top Bottom